Al Merrekh 0-0 Simba | Al Hilal Stadium | CAF

Al Merrekh 0-0 Simba | Al Hilal Stadium | CAF

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
El Merreikh leo wanaangazia kujaribu kurudisha tumaini baada ya kupoteza michezo yake miwili ya kwanza ikiwemo mchezo wa nyumbani.

Simba ikiwa imeshinda michezo yake miwili ya kwanza na kuongoza kundi, leo inataka kuweka mguu mmoja kuelekea kufuzu hatua ya makundi kwa kuifunga El Merrikh.

Kuwa nami kukujuza yatakayojiri Sudan

========

00' Mwamuzi anapiga filimbi kuashiria mwanzo wa mchezo

11' Mabadiliko kwa upande wa El Merrikh, Ramadan Agaba anaingia baada ya kuumia Hamza Daud

13' Simba wanajaribu kucheza pasi nyingi kuelekea lango la Al Merrikh lakini beki anatibua mpango wao

18' Almanusura Al Merrikh waandike bao la kwanza baada ya faulo maridadi kumkuta mchezaji wa Al Merrikh na kupiga kichwa kilichoenda nje kidogo ya goli

25' Ramadhan Agabu wa Al Merrikhanapiga kichwa mpira uliotokea kona lakini unagonga mwamba

27' Tony anajaribu kupiga shuti kuelekea lango la Simba lakini Benn Kakolanya anaukamata barabara

37' Mugalu anawekwa chini, mpira wa adhabu kuelekea Al Merrikh

38' Chama anapiga free kick lakini mlinda mlango anaudaka na kulala chini kuashiria kuumia

45' Bwalya anapiga shuti kali lakini unakwenda nje kidogo ya lango

45+1' Mpira mapumziko, Al Merreikh 0-0 Simba

46' Mpira umesharejea kutoka mapumziko

48' Kadi ya njano kwa Shomari Kapombe baada ya kuangusha Tony wa Al Merrikh

60' Mabadiliko upande wa Simba, Dilunga anachukua nafasi ya Bwalya na Nyoni anaingia kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin

72' Al Merrikh wanapata kona pacha lakini zote zinashindwa kuzaa matunda

76' Franscis Kahata anaingia kuchukua nafasi ya Chama

77' Lwanga kadi ya njano

88' Meddie Kagere anachukua nafasi ya Mugalu

90+4' Mpira umekwisha, Al Merrikh 0-0 Simba
 
Back
Top Bottom