Alama inayokubalika wakati wa kupiga kura na kuhesabu kura

Alama inayokubalika wakati wa kupiga kura na kuhesabu kura

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
234
Reaction score
390
ALAMA INAYOKUBALIKA WAKATI WA KUPIGA KURA NA KUHESABU KURA.

Kwa mujibu wa Aya ya 3.4 ya Maelekezo kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura, 2020, alama zinazokubalika katika kupiga kura ni hizi ambazo zimeelezwa hapa kama ifutavyo;

(1) Alama inayokubalika katika chumba kilichopo wazi kwenye karatasi ya kura ni alama ya vema (√).

(2) Alama nyingine zinazokubalika ni pamoja na alama ekisi yaani “X” ilimradi tu iwe katika chumba kilicho wazi.

(3) Hatahiyo, iwapo mpiga kura atashindwa kuweka kuweka alama ya vema (√) au alama ekisi (x) kama inavyotakiwa basi alama yoyote inayoonesha wazi kwamba mpiga kura alitarajia kumchagua mgombea yupi nayo itakuwa alama halali kisheria na itakubaliwa.

⛔ N.B: Kama mpiga kura atashindwa kuweka alama katika chumba kilicho wazi na badala yake akaweka alama hiyo kwenye jina la mgombea au chama chake cha siasa au nembo ya chama chake cha siasa, alama hiyo nayo itakubalika kuwa ni kura halali kisheria.

Zingatia: "Maelekezo ya Uchaguzi" (Election Directives) ni Sheria Ndogo Ndogo ambazo zimetungwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya mashartti ya Kifungu cha 126 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343.

By Matojo M. Cosatta

(the Legal Fitnaologist of Election Law and JF Senior Member).
 
X inawakilisha nini mbona haya maelezo yanachanganya watu kwa nini alama isiwe moja tu.
 
Naona kama Jumatano haifiki aisee tena kwa ushenzi huu wa mbelgiji mimi ni kijani mwanzo mwisho sitaki kujua nani kagombea udiwani.




MAGUFULI4LIFE
 
Mbona kama unapotosha vile,maana mambo yamekaa kimtego mtego, maelekezo ya tume ni tik.
 
X inawakilisha nini mbona haya maelezo yanachanganya watu kwa nini alama isiwe moja tu.
... Chief; sio kila mtu ana uwezo wa kuandika sijui kuchora alama ya "V". Mfikirie kikongwe aliyeko kule pembezoni kabisa mwa nchi au mgonjwa; wengine wanatetemeka mikono, n.k; ni vituko! NEC wamekuwa fair kwao pia kwamba alama yoyote mradi haina utata itakubaliwa as long as iko very clear mpiga kura alilenga kumchagua nani. Kwa mfano mwingine anaweza kuchora kimstari tu juu ya picha ya mgombea, n.k.
 
Msaliti wa taifa a.k.a mbeligiji ajiandae kurudi ubeligiji
 
Back
Top Bottom