Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,464
Kwa miaka mingi sana idara ya zimamoto mjini Chicago US inafuatilia alama ya mkono isiyofutika iliyobaki ukutani katika ukumbi mmoja ulioungua moto, licha ya alama hii kufutwa sana ukutani hapo lakini haijawahi kufutika. Wengi wanasema labda ni alama ya kimzimu.
Wengine waliamini kuwa labda ni alama ya mkono wa afisa wa zimamoto Francis Leavy ambaye naye alifariki kwa kuungua katika harakati za kuzima moto huo na kuwaokoa watu katika ukumbi huo uliokuwa unaungua vibaya.
Francis Leavy ni nani?
Fransis alikuwa ni afisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji mjini Chicago US katika miaka ya 1920, alikuwa anaipenda sana kazi yake hiyo, maafisa wenzake walikuwa wanampenda pia.
April 18, 1924 Francis alianza kuonekana tofauti mbele ya maafisa wenzake ofisini hapo, alikuwa kama chizi chizi hivi, kwanza asubuhi walimkuta akiwa anaosha madirisha ya ofisi yao ya zimamoto, baadaye akaanza kufanya vitendo vya ajabu huku akiropoka kuwa siku hiyo alikuwa na hisia mbaya, alikuwa anahisi kama anakufa siku hiyo.
Wakati hayo yakiendelea ofisini ghafla wakapokea simu ya dharula ikitaarifu kuwa jengo la ukumbi wa Curran lilikuwa linaungua moto, dakika chache tuu mbele Francis pamoja na maafisa wenzake wa zimamoto tayari walikuwa katika eneo la tukio kuzima moto huo na kufanya uokozi wa watu pia.
Wakati hayo yote yakiendelea ghafla paa la la jengo hilo likashuka, hawajakaa sawa kuta zikaanza kuanguka pia na kufunika baadhi ya watu ndani, Francis ndipo alipopoteza maisha kwa kuungua na mtoto akijaribu kuwaokoa wengine.
Baada ya moto kuzimika kukaonekana alama hiyo ya mkono ukutani ambayo iliacha maswali mengi, haikuweza kufutika, uchunguzi haujawahi kuja na majibu yoyote.
Written by Military Genius