MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,607
Nimetumiwa maelezo yaliyopo chini ambayo ningependa kugawana nanyi kwa wale wenye kuamini tiba ya mitishamba. Huu mmea unaitwa Aloe saponaria (Soap aloe), ambao licha ya kuwa unafanyakazi zile zile za aloe vera tuliyoizowea, huu unatibu kensa pia. Kwa hivyo kama unaujua, utunze na utumie.
Mmea huu wa aloe saponaria unajulikana pia kama aloe soap kwa sababu majani yake yanatoa povu linalongarisha nguo (ngozi) na hutumika kama sabuni ya kukfulia na kukogea bila ya kuharibu ngozi yako, kinyume chake. Na sio tu unaweza kuutumia kwa ajili ya ngozi, bali unaweza kuutumia kwa kula/kunywa kwa sababu una tija nyingi mwili. Na kama ilivyo mimeana miti mingi niliyoiona Afrika, mmea huu unaopatikana zaidi kusini ya Afrika unaua kansa. Na wala sio aina moja tu ya kensa bali unatokomeza kabisa aina nyingi za seli za kansa, hasa seli za lymphoma.
Lymphoma ni kansa ya T-lymphocytes, ambayo ni moja ya seli muhimu sana ya kukinga ya maradhi mwilini. Na aloe saponaria inaua aina nyingi za seli za lymphoma na huzuwia aina nyengine zisikue kabisa. Sababu kubwa ya tiba ya mti huu ni kijenzi chake kinachoitwa mannan. Katika tafiti, mannan kutoka aloe saponaria ina athari mbili, kuzuwia seli za kansa na kuboresha kazi za seli nyengine za kawaida.
Vile vile aloe saponaria ina nguvu kubwa ya kuzuwia kutu mwilini (antioxidant), inapunguza uvimbe na hutibu magonjwa mengi ya ngozi.
Kwa maelezo zaidi juu ya mmea huu na mengine angalia hapa. Ikiwa link haikufunguka na unahitaji kujua zaidi niPM na kunipa email yako nikufawadie barua pepe niliyotumiwa.