Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ALASIRI MOJA NYUMBANI KWA CHIEF ABDALLAH SAID FUNDIKIRA 1992
(Hii makala sikuandika mimi mwandishi hataki jina lake litokee lakini siku hiyo ya mazungumzo tulikuwa pamoja ilikuwa November 1992).
Ilikuwa mnamo mwezi wa Novemba 1992, mida ya adhuhuri katika mizuguko ya kuwatembelea wakongwe walioshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza.
Safari yetu ilitufikisha nyumbani kwa Alhaj Chief Abdallah Said Fundikira eneo la Magomeni Mikumi, Dar es Salaam.
Tulipata bahati kubwa kwa kuwa tulimkuta Chief Fundikira akiwa na rafiki zake Chief Dantes Ngua na Mhe. Joseph Kasella Bantu pamoja na watu wengine wawili, wakiwa katika mazungumzo ya kawaida.
Baada ya kuwasalimia, tulikaribishwa tukaketi.
Mohamed Said hakupoteza muda.
Aliwachokoza na maswali yahusuyo mambo muhimu wanayoyakumbuka sana katika enzi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wote walitabasamu huku kila mmoja wao akimuangalia Chief Fundikira kana kwamba wakitaka Mzee Fundikira aanze yeye.
Mzee Fundikira akasema kuwa yapo mengi ya kuzungumzwa ila muda ule haukuwa wa kutosha kwa sababu alikuwa ameshauriwa asikae muda mwingi pasipo kupumzika.
Masharti hayo alipewa na daktari baada ya kutoka katika mtikisiko wa homa.
Na hapo tukatambua kuwa wale wazee walienda kumjulia hali baada ya kupata taarifa ya kuumwa kwake.
Hata hivyo, Mzee Fundikira akanyanyuka huku akisema; “Mohammed, ngoja nikuletee zawadi…”
Alipanda ghorofani na kurudi na kitabu kidogo cha kurasa 55 kiitwacho, Ukombozi wa Tanganyika kilichoandikwa na Simon Ngh’waya; na kuchapwa na Chief Printer, CCM Printing Press, Dodoma, 1991.
Mzee Fundikira akasema, “huyu mwandishi aliniletea mimi hiki kitabu.
Nimekipitia na ninaona kitakufaa.”
Mzee akaongeza kusema, “Ni vyema watu waandike watakavyoweza kuandika juu ya yale yaliyotokea wakati wa enzi za kudai uhuru.”