LGE2024 Albert Chalamila atangaza rasmi ukomo wa muda kwa viongozi wa Serikali za Mitaa jijini Dar Es Salaam

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya zoezi la uchukuaji fomu za kugombea uongozi wa Serikali za mitaa kuanza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametangaza kuwa uongozi wa sasa umefikia ukomo leo tarehe 19 Oktoba 2024.

Wananchi wenye nia ya kugombea wamepewa muda wa kujiandaa kwani fomu zitaanza kutolewa rasmi kuanzia tarehe 26 Oktoba 2024.

Soma pia

Aidha, Chalamila amewakumbusha wananchi ambao bado hawajajiandikisha kwenye daftari la mkazi, kuwa muda unaoyoyoma na imebaki siku moja pekee kufikia mwisho wa zoezi hilo.

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya zoezi la uchukuaji fomu za kugombea uongozi wa Serikali za mitaa kuanza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametangaza kuwa uongozi wa sasa umefikia ukomo leo tarehe 19 Oktoba 2024.
Sasa mbona wengine hawakuwa namihuri tangu mwanzoni mwa mwaka huu,nilienda kijijini kwetu mwez March nikahitaji huduma ya mhuri ajabu mwenyekiti akaniambia mtendaji ameshakusanya mihuri yote kwaiyo ishu yoyote inayohitaji mhuri shart uende kwamtendaji
 
Wameikana Ile barua lakin wanatekeleza maagizo yake.😂
 
Sasa mbona wengine hawakuwa namihuri tangu mwanzoni mwa mwaka huu,nilienda kijijini kwetu mwez March nikahitaji huduma ya mhuri ajabu mwenyekiti akaniambia mtendaji ameshakusanya mihuri yote kwaiyo ishu yoyote inayohitaji mhuri shart uende kwamtendaji
Itakuwa hicho Kijiji hakina umuhimu wowote ule. Kwanza kina usajili? Tuanzie hapa.
 
Back
Top Bottom