Mtu anakufa kwa madawa .. Maisha yake kiula mtu alikuwa anaona kuwa ni mtu wa madawa pia riport ya kifa chake ilikuwa ni madawa hayo hayo. Leo anakufa kila mtu anasikitiunakuwa kama msiba wa kitaifa.... Huu ni Upuu....zi na uzandiki mkubwa. Mnatoa fundisho gani kwa vijana wadogo.
kwani chanzo cha kifo chake ni nini?
Mi naamini ktk Biblia na
ndiyo sababu si muongo, mnafiki, waongo, wachawi, wazinzi, wafiraji
hawata ulithi uzima wa milele, ukajitenge nao wafanyao uovu.
kwani hiyo may 28 ndo kaanza kuwa teja?mbona hakufa huko nyuma?alikua teja!
Ngwea na mwenzie M2 the P walilishwa sumu....
Mkuu ndo majina ya wajapani yalivyo, yani full vituko mara Kazakuku Takombili....yaani aibu...
Hii tabia ya kuwa mna msifia mtu anapo kufa tuiache MANGWEA hakuwa mtu mzuri ninaimani watu alio washawishi kuingia kwenyekundi la kutumia madawa ni wengi sana, kama tulikuwa tunampenda kwa kiasi hiki, mbona tulimuacha na hakusaidiwa kama RC?,
acha bif na Ngwea alishasema yeye kwake ni "NO bifu" usitake bf nae bro kwan ye yuko juu zaid yako...hata iweje huwez mfikia...utakufa na wivu...mwenzio had wanamzk wa marekan wamemtakia pumziko la aman lakin wew ukifa hata balozi wa nyumba 10 hata hudhuria mazishi yako....
Mkuu hata wewe ukifanikiwa kupata wadhfa wa kuweza kutoa wasifu wa marehemu ambaye ni public figure kama usemavyo nina uhakika asilimia mia moja hutataja maovu wala sifa mbaya ya marehemu hata moja.
kuna kitu kinaitwa ustaarabu, pale unapotoa taarifa kwa njia ya wazi kwa umma kaa ukijua unapotosha kile kizazi ambacho hakijapevuka vizuri kiakili kwa kuweza kuchanganua mambo mbali mbali katika maisha.
kuna vijana watapata uelewa kutumia madawa ya kulevya (unga, bangi, n.k) ndio usanii timilifu hii ni kutokana na wao kusikia au kusoma wasifu wa marehemu kutoka kwa mtu kama wewe. Waswahili wanasema "kua uyaone" sio uzaliwe tu na kuyakuta tayari yapo wazi wazi.
unadhani ukiandika maneno makali ya dharau na kebeh ndio utaeleweka, wewe huiwezi kazi ya ushauri japo una hoja za msingi..
Na ningemshangaa angekwenda kuzika wahuni akaacha kazi yake ya safari zisizo na mwisho wala maslahi. Tusikengeuke tukawa kama wazungu, kwa akili kama hizi ndio leo tuna Sir Elton John ambaye ni mke wa mtu. Naye akifa, mtataka heshima kwake
Shida yetu Watanzania ni UNAFIKI na kupenda kuambiwa maneno matamu huku ukweli TUNAUKATAA.
Hawa watoto tabia zao tunazijua. Tuachane na marehemu, keshaenda, sasa hivi tunaye huyu Diamond anayetoboa masikio na kuvaa ------ yako nje. Hakuna anayemkemea, ni kumsifia na kumsujudia kila anapopanda jukwaani. Siku atakapokufa, ndio tunakumbuka kuwa Mungu ni mkubwa kuliko Diamond na hapo hapo tunasahau kwamba Mungu haamrishwi.
Haka kamsemo kenu kachafu ka R.I.P kwa watu ambao uchafu wao u dhahiri ni masihara. Ni vyema kumuombea rehema na sio kumwambia Mungu amuweke mahali pema peponi. Kuna mmoja wetu ana mchango wa tofali kwenye ujenzi wa hiyo pepo?
Na wewe Black Bat, unapoambiwa matatizo yako dawa ni kuyaacha na sio kutafuta mifano kwenye matatizo ya mtu mwingine. Kama Michael Jackson hakuwa mwema sio kigezo cha Mtanzania mwenzetu Diamond kuweka ------ nje na kujichubua.