Alexander Mnyeti: Ifikapo mwaka 2032 kutakuwa na upungufu wa tani 234,000 za nyama nyeupe ikiwemo nyama ya kuku kama tusipokuwa na kimkakati

Alexander Mnyeti: Ifikapo mwaka 2032 kutakuwa na upungufu wa tani 234,000 za nyama nyeupe ikiwemo nyama ya kuku kama tusipokuwa na kimkakati

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Takwimu za Kitaifa zinaonesha kuwa ifikapo mwaka 2032 kutakuwa na upungufu wa tani 234,000 za nyama nyeupe ikiwemo nyama ya kuku endapo hakutakuwa na uwekezaji wa kimkakati kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya nyama hiyo. Hii inaonesha uwekezaji wa kimkakati katika tasnia hii unahitajika ili kukidhi mahitaji.
IMG-20241019-WA0001.jpg

Hayo yamesemwa leo tarehe 18 Oktoba 2024 Mlimani City Mkoani Dar Es Salaam na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya nane ya kuku na ndege wafugwao ambayo yamebeba Kauli Mbiu ya Kuku na Mayai ni Protini inayoongoza ( Chicken and Eggs the Leading Protein).

Kwa mara ya kwanza yalianza kufanyika rasmi mwaka 2015 chini ya usimamizi wa Chama cha Wadau wa Tasnia ya kuku Tanzania (Poultry Association of Tanzania).

Maonesho yamelenga kuonesha fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa kuku na ndege wafugwao, kukutanisha wadau, kubadilishana uzoefu na kukuza soko la kuku na ndege wafugwao pamoja na bidhaa zake ambayo yametanguliwa na Mkutano wa Jukwaa la Tasnia ya Kuku na Ndege Wafugwao kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambapo wageni zaidi ya 300 kutoka Mataifa 23.
IMG-20241019-WA0002.jpg

"Asilimia 55 ya kaya nchini zinajishughulisha na ufugaji wa kuku na hivyo kurahisisha upatikanaji wa nyama ya kuku na mayai. Aidha, takwimu za Kitaifa na Kimataifa zinaonesha kuwa kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya nyama nyeupe itokanayo na kuku na ndege wengine wafugwao, kutokana na ongezeko la watu kupendelea kula nyama nyeupe kuliko nyama nyekundu. Vilevile takwimu zinaonesha ifikapo mwaka 2030, nyama ya kuku itachangia asilimia 41 ya protini itokanayo na wanyama". Amesema Mnyeti.

Ameongeza "Nichukue nafasi hiikutoa rai kwa wadau kuchangamkia fursa hii kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati. Sisi kama Serikali tupo tayari kushirikiana na wadau wa Tasnia ya kuku na ndege wafugwao ili kuhakikisha tasnia hii inakua na kuchangia ipasavyo katika Pato la Taifa, kuinua kipato cha Wadau katika mnyororo wa thamani na kuchangia katika usalama wa chakula".

Amesema pamoja na mafanikio yaliyopo katika Tasnia ya kuku, bado kuna baadhi ya wadau ambao wanafanya kazi zao kinyume na taratibu zilizopo zikiwemo uanzishwaji wa vituo bubu vya utotoleshaji vifaranga, uzalishaji wa vyakula vya kuku visivyokidhi ubora na kufanya udanganyifu kwa kutumia nembo ya kampuni nyingine.

Hivyo, ni wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa anazingatia Usalama wa chakula wanachokizaliaha kwani anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia tasnia hii nchini.

"Kwa kumpa kuku vyakula visivyo takiwa huku kuku yule akienda kuliwa na binadamu, madhara anayo yapata yule binadamu kwa sababu ya virutubisho ulivyompa yule kuku, Unaua Taifa lako. Ninatoa rai kwa wadau wa tasinia hii ya kuku na ndege wafugwao kuhakikisha usalama wa chakula wakati wa kutengeneza hao kuku." amesema Mnyeti.

Mnyeti ameongeza "Usitafute faida kubwa huku ukiangamiza taifa lako. Uwe na kiasi hata kama vyakula vipo juu, sisi kama Serikali tunaenda kuangalia namna ya kulifanyia kazi ilikuona namna bei ya vyakula vitashuka chini."

Wakati huohuo, Mnyeti amemuagiza katibu Mkuu kumhoji na kumchukulia hatua mtu aliyesema na kutangaza kwwmba kuku wanapewa ARV, ili aseme huo utafiti kafanyia wapi na ushahidi upo wapi. Isijekuwa ni mtu anataka kuharibu Soko la kuku wa Tanzania kutokana na ushindani wa kibiashara.

Naye mwenyekiti wa chama mwamvuli cha wadau wa tasnia ya kuku wafugwao Mwanamvua Kishamte amesema kuwa kama wadau wanauomba na kuishauri serikali kuanzisha minada ya kuuzia kuku kwa kila halmashauri kama ilivyo kwa mifugo mingine,na pia bidhaa za kuku ziuzwe kwa kutumia mizani na sio kukadiria kwa Macho kama ilivyo sasa

Mwamvua ameongeza kwamba Tanzania ni Nchi ambayo inaongoza kwa bei kubwa sio tu ya vyakula vya kuku bali pia ya mazao ya ndege hao wa mifugo. Hali hii inaathiri ushindani wa kikanda na wakati mwingine hupelekea uingizaji kinyemela wa bidhaa hizi kutoka nchi jirani.

"Bei ya vyakula vya kuku kwa 67% huchangiwa na mwenendo wa bei ya mahindi na Soya. Soya peke yake huchangia 28% ya gharama ya chakula cha kuku. Uzalishaji wa Soya Nchini haijawahi kuzidi tani 40 wakati mahitaji ni tani 150. Hii inafanya Tanzania kutegemea Soya kutoka Nchi za Jirani." amesema Mwamvua

Kuagiza Soya kutoka nje ya Nchi za SADC kuna ushuru wa forodha mkubwa hivyo kufanya bei ya Soya kuwa kubwa zaidi.
IMG-20241019-WA0003.jpg
IMG-20241019-WA0004.jpg
IMG-20241019-WA0003(1).jpg
 
Back
Top Bottom