Alexander the great, Mfalme aliyepania kuitia dunia kwenye kiganja

Alexander the great, Mfalme aliyepania kuitia dunia kwenye kiganja

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Jina lake kamili ni Alexander Philip, wazungu wao humuita Alexander the Great (yaani Alexander mwenye nguvu) mtoto wa kwanza wa mfalme Philip II wa Macedonia (Ugiriki) na Malkia Olympias binti wa mfalme Neoptolemus aliyetawala eneo la Epirus (Ugiriki).

Alexander alizaliwa mwaka 356 BC katika mji wa Pella nchini Ugiriki akifuatiwa na dada yake, Cleopatra aliyezaliwa mwaka 355 BC.

ELIMU:
Alexander alipoifikisha umri wa miaka 13, Baba yake, Mfalme philip II aliamua kutafuta Mwalimu atakayemfundisha mwanaye na hatimaye akamchagua Mmoja wa wanafalsafa nguli kwa jina Aristotle awe mwalimu wa kijana wake. Kutokana na sababu za kiusalama. Mfamle Philip alitenga eneo maalumu liitwalo Mieza akajenga shule ya bweni ili mwanaye na watoto wengine wa viongozi na watumishi wa mji wa Macedonia waweze kusoma hapo.
Katika shule hiyo, Alexander alifundishwa mambo mengi yakiwemo; kusoma, kuandika, kucheza, kupigana, kuendesha farasi na kupiga zeze la jadi.
Mwanafalsafa Aristotle alimfundisha Alexander the great hadi kufikia umri wa miaka 16 na akawa ameiva kweli kweli.

NDOTO ZA UONGOZI:
Wahenga wanasema Nyota njema huonekana asubuhi, naam siku moja Alexander akiwa na miaka 10 baba yake alimuagizia farasi mdogo kutoka kwa mfanya biashara wa mji wa Thessaly ndani ya Macedonia kwa thamani ya talanta 13. Farasi huyo alipofika nyumbani aligoma kabisa kupandwa na Baba yake Alexander akataka kumrudisha.
Lakini Alexander alimsihi baba yake amnunue tu kwani aligundua kuwa farasi yule aligoma kupandwa kwa hofu ya kutazama kivuli chake. Hivyo akamfundisha na ndani ya saa chache tu farasi akaelewa somo na akakubali kupandwa kisha akampa farasi huyo jina la Bucephalus na akawa ndiye farasi wake aliyemtumia kwa safari zake zote mpaka farasi huyo alipokufa baada ya kuzeeka.
Kitendo hicho cha kishujaa kilimshtua sana Mfalme Philip II na akamkumbatia mwanaye kwa machozi ya furaha huku akimwambia "kijana wangu, nimegundua una akili sana, naona hata huu mji wa Macedonia hautakutosha, hakikisha unatafuta himaya kubwa ya kutawala katika siku zako"
Maneno hayo yalitia chachu ya ujasiri wa Alexander katika makuzi yake kwani daima alijituma sana katika mafunzo yote aliopewa na mwalImu wake hata hivyo alitumia muda mwingi sana kukaa na baba yake ili ajifunze mambo ya uongozi. huku akijiandaa kuja kukalia kiti cha enzi baada ya hatima ya Baba yake Mfalme Philip II.
Ulipofika mwaka 336 BC, Alexander akiwa na umri wa miaka 20 tu, Baba yake mfalme Philip II aliuawa na maadui zake, Hivyo ikamlazimu Alexander kushika hatamu ya Utawala wa Macedonia mara moja akiwa angali kijana mdogo. Na akaitwa Mfalme Alexander II

UTAWALA:
Mfamle Alexander the Great alipoikamata Macedonia alionekana kuwa na akili, hivyo Macedonia ikawa ndogo sana kuitawala, ikabidi kutanua mipaka ili apate milki kubwa kadri alivyoweza kama baba yake alivyomuasa enzi za uhai wake.
Aliunda jeshi lenye nguvu huku akiwa yeye ndio kamanda muongoza njia katika vita zote alizopigana. Mfalme Alexander na jeshi lake alivamia maeneo mengi ya Dunia huku akisambaratisha tawala zote alizozikuta katika maeno hayo.
Mfano; Mwaka 330-323 BC alikuwa Mtawala Mkuu wa Asia (Lord of Asia), huku Afrika aliivamia Misri na akafanikiwa kuwa Firauni (Pharaoh of Egypt) kuanzia mwaka 331-323 BC na mwaka 334 aliivamia Persia na kumng'oa Mfalme Darius III akajitwalia Ufalme (King of Persia) kuanzia mwaka 332-323 BC

Kampeni ya mapigano ya mwanaume huyu haikukomea hapo kwani alitanua Milki yake hadi kuvuka bahari ya Adriatic na kufika mto Beas Nchini India na kusambaratisha utawala wa Bonde la India (Indus Valley) mnamo mwaka 326 BC.
Mbali na ushujaa wake katika vita, inasemekana kwamba; Mfalme Alexander the Great alichangia sana kuanzisha miji maarufu zaidi ya 20 hapa Duniani, miongoni mwake ni kama; Alexandria ulioko Misri, Alexandria Bucephala uliko nchini Pakistan.
Alexandria Bucephala ulitokana na kifo cha farasi wake (bucephalus) aliyekufa baada ya kuzeeka huko nchini Pakistan na akamua kuliita eneo hilo Bucephala kama sehemu ya kumuenzi farasi wake aliyemtumia tangu enz za utotoni aliponunuliwa na baba yake.

FAMILIA:
Mfalme Alexander the Great alifanikiwa kuoa wanawake watatu ambao ni; Stateira, Roxana na Parysatis. Japo haikufahamika wazi idadi ya watoto alokuwa nao lakini mtoto pekee aliyejulikana ni Lollas ambaye mara nyingi alikuwa anamchanganyia pombe mfalme Alexander II.

KIFO:
Mfalme Alexander II alifariki mwaka 323 BC akiwa na umri wa miaka 32 katika eneo la Babiloni lililokuwa likitawaliwa na mfalme Nebukadneza II. Tukio hili lilifuata baada ya Mfalme Alexander II aliporejea mapumzikoni nyumbani kwakwe kutoka India na kafanya karamu kubwa ambayo ilichukua takribani wiki mbili.
Chanzo cha kifo chake kilizua utata wa hali ya juu na kupelekea kuwepo kwa Nadharia kadhaa zinazoelezea ukweli wa chanzo cha kifo chake.
Pamoja na uwepo wa nadharia tofauti zinazoelezea sababu ya kifo chake ila inayoaminika zaidi ni ile inayodai kuwa Huenda Alexander the Great alifariki kwa madhara ya sumu iliyochanganywa katika pombe wakati wa ile karamu aliyoifanya kwa takribani wiki mbili.

Nadharia hii huenda mbali na kutoa shutuma kuwa watu wa karibu wanaweza kuwa walihusika na kifo cha Alexander kwa kumchanganyia sumu kwenye pombe. Miongoni mwa watu wanaoshutumiwa ni Bw. Antipater aliyekuwa mtendaji mkuu katika falme ya Macedonia awali kabla ya kuvuliwa wazifa huo.
Kiongozi huyu anahisiwa kumdanganya mtoto wa Alexander aliyeitwa Lollas ambaye ndiye alikuwa mchanganyaji mkuu wa pombe ya Baba yake na akafanikiwa kumpumbaza kisha jamaa akatia sumu hiyo kijanja bila bwana mdogo kushtukia mchezo. Wengine wanaenda mbali na kudhania kwamba katika hili la sumu, huenda hata mkono wa Mwanafalsafa Aristotle ulihusika kuandaa mpango wa kumuua Mfalme Alexander II.

Watafiti wa Nadharia hii wanadai kuwa zile wiki mbili za karamu ya Alexander alikuwa hoi akiugulia maumivu makali ya tumbo na homa kali kiasi kwamba ilifikia kipindi hakuweza hata kuongea na ilipofika siku ya 12 aliishia kuwapungia mkono wanajeshi wake muda mfupi kabla ya kukata roho.
Nadharia hii ya sumu ilibakia kuwa kitendawili kikubwa akilini mwa watu kwa miaka mingi huku wengine wakifikiria kuwa ni sumu gani hiyo yenye kudumu kwa siku 12 bila kuondosha uhai wa mtu!,

hadi ilipofika mwaka 2003 Shirika la BBC lilituma jasusi kutoka Taasisi maalumu ya kitengo cha sumu kutoka nchini Newzeland Bw. Leo Schep kwenda kuchunguza kama ni kweli ni madai ya kuwa sumu ndiyo iliyomuondoa Alexander the Great?, na kama ni kweli basi inaweza kuwa ni aina gani ya sumu.
Jasusi huyo alifanya uchunguzi na akagundua kuwa ni kweli Mfalme Alexander ailiuawa kwa sumu itokanayo na mmea uitwa White Hellebore au Veratrum Album ambao huota maeneo ya Ulaya ikiwemo Ugiriki na sehemu chache za Asia
.

Pia jasusi huyo alidai kuwa dalili zote alizozionesha Mfalme Alexander II kabla ya kufariki kwa siku zote 12 kama vile; homa kali, kuumwa na tumbo na hatimaye kushindwa kuongea basi zinarandana na madhara yasababishwayo na sumu ya mmea huu.

Baada ya kifo cha Alexander, majemedari wake walianza kugombanakuhusu nani atawale , miaka 22 baadae ufalme wa kiyunani uligawanyika ktk falme nne chini ya majemedari waliojulikana kama DIDOCHI yaani warithi
Majimbo haya yalidhoofika siku hadi siku na wakatawaliwa na UFALME WA RUMI, UNABII WA DANIELI ULISEMAJE?

Danieli 2:40 SRUV​

Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuviponda; na kama chuma kipondavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunjavunja na kuponda.

MWISHO:
kwa miaka 12 ya Utawala wake katika falme ya Macedonia Mfalme Alexander II, ni dhahiri kwamba alikuwa amepania kuitia dola ya Dunia kiganjani kwake kwa sababu kwa muda huo mfupi wa utawala wake alikuwa ameshatwaa maeneo mengi sana ya kila pembe ya Dunia kama sehemu ya milki yake.
Yamkini kama sio kifo kumchukua angali kijana basi nachelea Kusema kuwa mtu huyu kuna siku angeitawala Dunia nzima.

1618729135064.png
 
Ila pia kuna nasharia ilidai Alex alienda kupigana vita huko India kama sijakosea na porus. Battle ilikuwa ngumu na walipigwa mno ikapelekea kupata majeraha alivyorudi Babeli ndiyo akawa mgonjwa hadi kupelekea kifo.

Hii imekaaje mkuu?
 
Mbona mwaka wa kifo upo nyuma na miaka ya vita ipo mbele..au alipoufa mzuka waake ulifufuka na kupigana hvyo vita?
 
ni vyema waandishi wa makala mkawa mnatuwekea na vyanzo vya taarifa.
 
Bro maana ya BC ni Before Christ so miaka inahesabika katika descending order kuelekea mwaka aliozaliwa Yesu.

Hiyo miaka inayopungua (descending) reference yake ni mwaka gani. Hii ya sasa ilianzia 1 yaani mwaka wa kwanza na kuendelea huku mbele hadi tuliko sasa 2021. Je, hiyo iliyokuwa inapungua kuelekea 0 na hadi kuanza moja kuja huku karne ya 21 ilianzia wapi, au ilianza na mwaka gani?
 
Hiyo miaka inayopungua (descending) reference yake ni mwaka gani. Hii ya sasa ilianzia 1 yaani mwaka wa kwanza na kuendelea huku mbele hadi tuliko sasa 2021. Je, hiyo iliyokuwa inapungua kuelekea 0 na hadi kuanza moja kuja huku karne ya 21 ilianzia wapi, au ilianza na mwaka gani?
Swali fikirishi na zuri sana. Nadhani tukienda scientifically tutarudi mpaka mwaka ambao majority ya wana science wanakubaliana kuwa ndio dunia ilianza kuwepo ambayo miaka billioni 4.5 iliyopita.

According no NASA

"When the solar system settled into its current layout about 4.5 billion years ago, Earth formed when gravity pulled swirling gas and dust in to become the third planet from the Sun. Like its fellow terrestrial planets, Earth has a central core, a rocky mantle and a solid crust."
 
Bwana Alex inaelekea alimwachia dada yake cleopatra misri, daaah bidada alikua anaoga maziwa ngamia ndio maana akawa mzuri hahaha
 
Licha ya uwezo wake mkubwa kivita mbabe wake alikuwa ni jamaa mmoja fukara sana anayeitwa Diogenes.
 
ni vyema waandishi wa makala mkawa mnatuwekea na vyanzo vya taarifa.
Ila pia kuna nasharia ilidai Alex alienda kupigana vita huko India kama sijakosea na porus. Battle ilikuwa ngumu na walipigwa mno ikapelekea kupata majeraha alivyorudi Babeli ndiyo akawa mgonjwa hadi kupelekea kifo.

Hii imekaaje mkuu?
ni kweli kabisa wawe wanatuwekea link ay vyanzo vya habari maana huyu kijana ana story ndefu sana, lkn wao wana weka misifa tu wakati huko India alipigwa sana
bado kuna mahali wanamuelezea km Homosexually tena shoga kabisa na tumeshaijadili humu JF
Kwa hiyo kwa wageni kuturudisha nyuma sio mbaya ila kudanganya kwa kutoweka vyanzo, zipo DVD zake zilisambazwa sana na Alibaba zikionesha Historia yake kuzaliwa vita alizopigana hadi kifo
 
Back
Top Bottom