joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Kama tulivyosema siku za nyuma kwamba Tanzania ni " role model " katika ukanda huu, karibuni majirani kuja kujifunza mambo mbalimbali.
Wakenya kwenye mtandao wamechemka baada ya mvua inayoendelea kunyesha humu nchini kufichua ubovu wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Hayo yalijiri baada ya kanda kuibuka mtandaoni ikionyesha wateja wakinyeshewa wakati wa kuabiri ndege katika uwanja huo.
Video hiyo ilichapishwa kwenye mtandao na mwanaharakati Boniface Mwangi na kuuliza maswali kuhusu ujenzi wa JKIA.
Mwangi alikashifu kisa hicho na kusema uwanja huo wa ndege umejengwa kama zizi la ng'ombe.
Ni video ambayo ilileta mjadala mtandaoni huku Wakenya wakihoji kuhusu mamilioni yaliyotumika kwenye ujenzi huo.
Baadhi ya waliochangia walisema Kenya itapoteza umaarufu wake kutokana na utepetevu unaoshuhudiwa katika sekta mbali mbali.
Ni hali ambayo huenda ikachafua picha ya uwanja huo wa ndege kwenye rubaa za kimataifa nakuushukisha ngazi licha ya kuwa umewekwa katika orodha moja na viwanja vingine maarufu duniani
Kisa hicho kinajiri tu baada ya uwanja huo kuangaziwa hivi maajuzi baada ya mwili wa jamaa mmoja kuanguka kutoka alipokuwa amejificha chini ya ndege iliyokuwa imetoka JKIA kuelekea Uingereza.