Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Urusi imesaini mikataba ya kusambaza chanjo yake virusi vya corona inayoitwa Sputnik V kwa mataifa ya Algeria na Bolivia.
Hii ni mara ya kwanza kwa Urusi kuanza kusambaza chanjo ya COVID19 nje ya taifa hilo ambapo inaiweka Bolivia kuwa nchi ya kwanza kwa mataifa ya Amerika Kusini kupokea chanjo ya COVID19 kwa wingi, ikiwafikia watu milioni 2.27 sawa na asilimia 20% ya Wabolivia.
Rais wa Bolivia, Luis Arce amesema wanatarajia kupokea dozi 6000 mwezi huu kwa ajili ya kuzigawa kwa makundi yenye uhitaji zaidi ya watu 3000, huku dozi zingine milioni 1.7 zikitarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi Machi, na kiasi kilichosalia kitawasili kati ya mwezi Aprili na Mei.
Algeria, kwa upande wake, imepanga kuanza kampeni kubwa ya kutoa chanjo kwa umma mwezi huu, ikipanga kutoa chanjo bure kwa wananchi wote.
Chanjo ya Sputnik V ina uthabiti wa asilimia 91.4, na hutolewa kwa awamu mbili kwa wagonjwa. Tofauti na chanjo za Pfizer-BioNTech na Moderna ambazo hugharimu dola za Marekani 20 na 33 kwa dozi (sawa na Tsh 46,370 na 76,511), chanjo hiyo ya Urusi itagharimu dola 10 tu (sawa na Tsh. 23,185) kwa dozi. Kwa raia wa Urusi, chanjo hiyo itatolewa bure.
Chanjo ya Sputnik V ni tofauti pia na chanjo zingine za COVID19. Wakati chanjo nyingi zinafanya kazi kwa kuchomwa sindano mara mbili za aina hiyohiyo ya dawa, chanjo ya Sputnik V hufanya kazi kwa kuchomwa sindano mara mbili ya aina tofauti za dawa.