Mtamba wa Panya
JF-Expert Member
- Aug 6, 2017
- 764
- 1,892
Taifa la Algeria mpaka sasa limeendelea kuwa "Neutral" na limekataa kuongeza uzalishaji wake wa gesi kwa ajili ya soko la Ulaya kufidia "gepu" lililoachwa na nchi ya Urusi, Vyombo vya habari vya nchi za kiarabu vimeripoti.
Miundombinu ya LNG
Msimamo huo wa Algeria umedhihirisha umuhimu wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Algiers na Moscow tokea uhuru wa taifa la Algeria mwaka 1962 pale USSR ilipotangaza kuingia uhusiano wa kidiplomasia kati yake na Algeria.
Wakati huo huo, Algeria ilitambua Taifa la Urusi mwaka 1991 baada ya kuvunjika kwa USSR. USSR ilikuwa miongoni mwa nchi muhimu zilizosaidia Kisiasa na kivita kwenye vita ya ukombozi wa taifa la Algeria na ilikuwa nchi ya kwanza Duniani kutambua serikali iliyoundwa.
Ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili ulianza tokea miaka ya 1960 pale USSR ilipoipatia Algeria mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo wakati inatokea kutawaliwa kwa miaka zaidi ya 130.
Kwa usaidizi kutoka USSR, miradi muhimu ya kiuchumi ilianzishwa nchini Algeria ikiwemo viwanda vya steel na chuma, uzalishaji wa Umeme, bomba la gesi pamoja na bwawa la maji.
Mpaka sasa, kampuni ya Taifa ya mafuta ya Algeria, Sonatrach ina ushirikiano wa karibu na kampuni za nishati za Urusi na pia nchi hizi mbili zimesaini mikataba ya ushirikiano kwenye sekta mbali mbali.
Algeria inasambaza na kuuza gesi barani Ulaya kupitia mabomba makubwa matatu.
Akizungumzia ombi la Ulaya kufidia uuzaji wa gesi, CEO wa zamani wa Sonatrach alisema "Kiwango cha gesi kinachosambazwa na Algeria kwa mwaka barani Ulaya ni mita za ujazo billioni 42, wakati Urusi inaweza kusambaza kiwango hiki kwa bomba moja tu ".
"Kiukweli hakuna nchi yoyote inayoweza kuziba gepu la uzalishaji wa nchi ya Urusi kwa sasa, kuna mkakati wa nchi za Ulaya kupunguza utegemezi wa gesi kutoka Urusi kupitia vyanzo mbadala kama Algeria, Qatar na USA" aliongeza kusema.
Pia ikumbukwe kuwa Urusi ndio muuzaji namba moja wa silaha kwa Taifa la Algeria. Kwa miaka ya karibuni, kwa mujibu wa waangalizi, Algeria imenunua silaha kutoka Urusi zenye thamani ya mabillioni ya dola zikiwemo Sukhoi na MiG (ndege), helikopta, vifaru pamoja na submarine.