Ali Choki na Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

Ali Choki na Super Nyamwela warudi Twanga Pepeta

Mjasiria Akili

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
823
Reaction score
372
Baada ya kuvimba kwa kipindi kirefu hatimaye wamebwaga manyanga na kuamua kurejea twanga pepeta

Kweli nimeamini Twanga ni Kisima cha burudani ndo maana Choki na Nyamwela wamerudi Twanga na kutambulishwa kwa wana habari leo hii pale Nemax Hotel Kinondoni.

Swali langu ni; hivi Choki na Nyamwela bendi yao wamemwachia nani?!

=============

Choki, Nyamwela watua Rasmi Twanga Pepeta

View attachment 241414View attachment 241415

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa kundi la muziki la Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’, Ali Chocky, ameamua kurudi katika bendi yake ya zamani ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayomilikiwa na Asha Baraka ambaye ni mkurungezi wa bendi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Nemax Royal, kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, amesema kurudi kwa wakongwe na waasisi kwenye bendi yao ambao ni Chocky na Super Nyamwela, kutaleta nguvu mpya na mapinduzi katika muziki wa dansi nchini kutokana na uwezo wao binafsi.

Kwa upande wake, Chocky amesema kuamua kwake kurudi katika bendi yake ya zamani ni kutokana na mapenzi yake binafsi na wala hajalazimishwa na mtu huku akisisitiza kuwa hajafulia na ndiyo kwanza moto umeanza.

“Tupunguze maneno-maneno; kurudi kwangu na Super Nyamwela ndani ya Twanga si kitu cha ajabu, tumeamua wenyewe na kila mtu ana uhuru wake binafsi wa kufanya jambo kwa muda muafaka bila kupangiwa.

“Wakati nasafiri kwenda Japan niliwaambia wanamuziki wa bendi yangu kwamba yeyote anayeweza kunisubiri anisubiri na kama wapo watakaotaka kuondoka waende, lakini niliporudi niliwakuta wameshatawanyika, sasa nipo nyumbani.

Mashabiki wangu wategemee makubwa kutoka kwangu kwani muda si mrefu nitaanza kupakua nyimbo kama vile Kichwa Chini, Usiogope Maisha na nyingine nyingi,” alisema Chocky.

Chanzo: GPL
 
HA HA hahaha Choki si ana bendi yake? iweje uhame nyumbani mwako uende kupanga?
 
Kweli nimeamini Twanga ni Kisima cha burudani ndo maana Choki na Nyamwela wamerudi Twanga na kutambulishwa kwa wana habari leo hii pale Nemax Hotel Kinondoni.

Swali langu ni; hivi Choki na Nyamwela bendi yao wamemwachia nani?!

=============

Choki, Nyamwela watua Rasmi Twanga Pepeta

2.jpg4.jpg

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa kundi la muziki la Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo', Ali Chocky, ameamua kurudi katika bendi yake ya zamani ya African Stars ‘Twanga Pepeta' inayomilikiwa na Asha Baraka ambaye ni mkurungezi wa bendi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Nemax Royal, kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, amesema kurudi kwa wakongwe na waasisi kwenye bendi yao ambao ni Chocky na Super Nyamwela, kutaleta nguvu mpya na mapinduzi katika muziki wa dansi nchini kutokana na uwezo wao binafsi.

Kwa upande wake, Chocky amesema kuamua kwake kurudi katika bendi yake ya zamani ni kutokana na mapenzi yake binafsi na wala hajalazimishwa na mtu huku akisisitiza kuwa hajafulia na ndiyo kwanza moto umeanza.

"Tupunguze maneno-maneno; kurudi kwangu na Super Nyamwela ndani ya Twanga si kitu cha ajabu, tumeamua wenyewe na kila mtu ana uhuru wake binafsi wa kufanya jambo kwa muda muafaka bila kupangiwa.

"Wakati nasafiri kwenda Japan niliwaambia wanamuziki wa bendi yangu kwamba yeyote anayeweza kunisubiri anisubiri na kama wapo watakaotaka kuondoka waende, lakini niliporudi niliwakuta wameshatawanyika, sasa nipo nyumbani.

Mashabiki wangu wategemee makubwa kutoka kwangu kwani muda si mrefu nitaanza kupakua nyimbo kama vile Kichwa Chini, Usiogope Maisha na nyingine nyingi," alisema Chocky.

Chanzo: GPL
 
"Ally Choki ni Mwanamuziki mzuri sana lakini akiwa ndani ya Twanga Pepeta, nje ya hapo si chochote"
By Matola.

Big up Mkuu wangu, nimeamini maneno yako!
 
Last edited by a moderator:
Daah kweli hakuna aijuae kesho...
Ila wengi wakishaisha makali ndio wanarudi Twanga..... Inaonekana pale twanga pana Noleo la kurudisha makali..... Ila wajue mziki siyo kuwa na uwezo wa kuimba au kunengua mauno ni kuwa na kamati bora za UFUNDI....sasa hapo ndio mgeni.
 
"Ally Choki ni Mwanamuziki mzuri sana lakini akiwa ndani ya Twanga Pepeta, nje ya hapo si chochote"
By Matola.

Big up Mkuu wangu, nimeamini maneno yako!
Umeonaee! Ali choki n mzuri akiwa twanga tu!
 
Last edited by a moderator:
Kumbe ukiongea kweli jifunze kuweka akiba.
Hivi si Choki alisema hata akifa Asha Baraka asiudhurie? Au nachanganya mambo!
 
Ila wengi wakishaisha makali ndio wanarudi Twanga..... Inaonekana pale twanga pana Noleo la kurudisha makali..... Ila wajue mziki siyo kuwa na uwezo wa kuimba au kunengua mauno ni kuwa na kamati bora za UFUNDI....sasa hapo ndio mgeni.
Ndo maana pale panaitwa kisima cha burudani! Big up Twanga na kisa cha mpemba!
 
Vita ya kuajiriwa na kujiajiri. Kuwa na kipaji cha muziki ni kitu kimoja na kuwa na kipaji cha kuongoza bendi ya muziki ni kitu kingine. Kwa sisi wapenda soka, si lazima mchezaji mahiri sana awe kocha mzuri. Ni wachache sana kama Pepe Guardiola. Sioni mfano mwingine kwa haraka haraka.

Ali Choki, concentrate on your what you can do best. Let others take care of other issues.
 
"Ally Choki ni Mwanamuziki mzuri sana lakini akiwa ndani ya Twanga Pepeta, nje ya hapo si chochote"
By Matola.

Big up Mkuu wangu, nimeamini maneno yako!

Ukweli huwa haubadiriki kamwe, na hii habari ndio naiona sasa hivi hapa kwenye thread hii.

Sasa Twanga itatisha kama zamani Ally Choki hakuwa na platform ya kuonesha kipaji chake sasa mambo ni tambarale ila Choki awe tayari kuwa chini ya Luiza Mbutu maana rekodi na utumishi uliotukuka wa Luiza Mbutu hakuna hata mwanamziki mmoja wa Twanga anayeifikia.
 
Last edited by a moderator:
Suala la kujiajiri lataka moyo sio mchezo kama ambavyo wengi wanafikiri
 
Back
Top Bottom