Ali Hassan Mwinyi : Mzee rukhsa Safari ya Maisha Yangu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ALI HASSAN MWINYI: MZEE RUKHSA SAFARI YA MAISHA YANGU

Bi Lucie wa Mkuki na Nyota Wachapaji wa kitabu hiki amenifahamisha kuwa mimi hapo dukani kwao ni mtu wa pili kununua kitabu hiki.

Mtu wa kwanza yeye alilipia nakala yake kabla ya uzinduzi wa kitabu jioni hii leo.

Kitabu kimenifikia nyumbani baada ya kumaliza kufuturu tukiwa gizani ila kwa mwanga hafifu wa mishumaa kwani umeme ulikuwa umekatika.



 
Hongera.

Sasa kisome halafu utuletee Muhtasari..
 
Hongera yako kwa kupata nakala ya kitabu hicho.
 
Mzee wangu ni kwamba hatujajua tu bado bt kiukweli wewe ni hazina kubwa sana hapa jf, Mungu azidi kukulinda na kukupa maisha marefu zaidi.
 
Nina hamu kukisoma alichoandika Mzee wetu Rais mstaafu, ila bei ni kubwa mno
 
Sio vizuri kumdhihaki mwendazake hivi, sote ni mavumbi na mavumbini tutarejea.
Kuna muda Hadi mtu unabaki unashangaa Yani..tangu magu amekufa ndy nimebaini siasa ni Imani Kama km Imani zingine tu.Imani inabeba misimamo.mtu anabeba chuki juu ya mwanasiasa fulani na mwingine anampenda huyo mwanasiasa kiasi kwamba wote wanakuwa vipofu,mmoja anapinga mwingine anasifia kila lifanywalo na huyo mwanasiasa hata liwe Baya vipi

Sasa Kwa huyo jamaa yeye ameamua kuwa upande wa chuk Kwa mwendazake..Hata sasa mwendazake hayupo lkn bado wanamuatack Hadi akiwa kaburini huku wanasahau siku moja nao watakuwa usawa wa futi sita chini ya ardhi
 
Bei yake tafadhali
 
Hivi Magufuli yeye hakwandika kitabu chochote,huku ndio alikuwa Rais Msomi kuliko wote hapa Tanzania.
Acha unywanywa angeandikaje wakati hakuwa amestaafu kupata muda wa kufanya hivyo. Kama Mwinyi amekiandika miaka 30 baada ya kustaafu, ulitegemea Magufuli atende miujiza gani kufanya hivyo. Hata hivyo, tokana na rekodi yake, wapo watakaoandika tena vingi juu yake.
 
Mohammed Said malizia daku. Naamini utakuja na andiko la hekaya namna mzee Kitwana Kondo alivyomsaidia mzee baada ya kuondolewa kwenye nyumba ya serikali. Naamini mzee KK alikuachia hizi hadithi na zitafaa kizazi kijacho.

Daku njema mzee Mohamed Said.
 
Yaan wanaumiza sana mioyo ya watu hawa lol.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…