Ali Kamwe adai taarifa za kufungiwa ni tetesi tu!

Ali Kamwe adai taarifa za kufungiwa ni tetesi tu!

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ali Kamwe amesema hajapokea taarifa yoyote ya yeye kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka, kwani bado hajapokea barua kuhusu suala hilo.

snapinst (1).jpg

Akizungumza kwenye mahojiano na Kituo cha Redio cha Wasafi FM Machi 07, 2025 Kamwe amesema hajui taarifa hizo zinazoendelea kusambaa katika mitandao mbalimbali chanzo chake ni wapi, huku akiwataka mashabiki wa Yanga kusubiri taarifa rasmi.

"Taarifa za Ali Kamwe kufungiwa miaka miwili ni tetesi, Nasema ni tetesi maana mimi, mawakili wala klabu yangu hatujapewa Taarifa za hukumu hiyo na Mamlaka zinazohusika (Kamati ya Maadili ya TFF). Taarifa hizo ni za mitandao tu "

"Ni ukweli niliitwa kwenye kamati na shtaka langu niliambiwa kuwa nimedhalilisha Mamlaka kwa maana ya TFF na Bodi ya Ligi kwa kuzungumza maneno ya Uongo yasiyo na busara kwa kutumia chapisho langu kwenye ukurasa wangu wa Instagram ambalo nilichapisha Februari 3, 2025"

Soma: Inaelezwa Ali Kamwe kafungiwa miaka 2, Ahmed Ally anusurika na rungu la TFF
 
Back
Top Bottom