Msanii wa bongo Fleva Alikiba amemshushia tuhuma nzito meneja wa msanii mwenzie Diamond platnumz maarufu kama Sallam.
Akizungumza na clouds FM katika kipindi cha xxl, alikiba amezumgumza kwa huzuni sana kwamba Sallam ndiye aliyehusika kufitinisha yeye kupokonywa maiki katika jukwaa hilo
Anasema wakati akiwa jukwaani alimuona sallam chini ya jukwaa, hivyo huenda amehusika moja kwa moja katika fitna hiyo.Anasema kama hawana bifu meneja huyo alikwenda Mombasa katika show hiyo kufanya nini?
Haya yamekuja baada ya Alikiba kuperform nyimbo mbili tu na kuzimiwa maiki na kupandishwa msanii mwingine Chriss brown.
Je , tuhuma hizi zinaweza kuwa na ukweli wowote?