Ali Kiba Firdausi huwezi kufika kiki, hizi kiki mwisho wake ni Shilawadu tu

Ali Kiba Firdausi huwezi kufika kiki, hizi kiki mwisho wake ni Shilawadu tu

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Ni hivi unapofanya ibada kama kusaidia yatima then unakwenda na makamera ili uonekane na public kimsingi dini yoyote ile haikubalini na sadaka za aina hii na ukweli hupati swawabu yoyote kwa sababu Mungu anatambuwa mpaka ndani ya nafsi yako kwamba lengo lako kuu ni publicity na siyo sadaka, sadaka haitaki mbwembwe na kiki.

Firdausi ni pepo ya juu sana huwezi kuiona Firdausi kama bibi harusi tu kwa gunia la mchele na sabuni na makamera kibao.

Hii tabia naikemea kwa wote wenye huu mchezo wa kujionesha kwenye matendo ambayo inatakiwa Mungu tu ndio akuhesabie na yule unayemtendea tu.
FB_IMG_1527807463039.jpg
 
Kingine ni kwamba pesa ya sadaka inatakiwa iwe safi na iliyopatikana kwa njia za halali.
Kwa hapa bongo aina ya pesa hiyo labda uende uichukue moja kwa moja kule wanapofanya printing ya pesa yenyewe, ila ukiona imeingia kwenye mzunguko tu hiyo pesa sio safi. Haujawahi sikia pesa iliyotumika kuulia ndio hiyo hiyo ilifutwa damu kisha ikatumika kununulia Msahafu au Biblia.?
 
hakuna pesa chafu/haramu ila kuna kipato kichafu/haramu...hela inaweza kwako ikawa haramu kuitumia lakini hela hiyo hiyo ni halali kwa mwengine kuitumia..eg. pesa yako inaweza ikawa chanzo chake ni dawa za kulevya, kwako wewe hii hela ni haramu kuitumia kwani haitokani na pato halali, lakini pesa hiyo hiyo ukiichukua halafu ukawapelekea watoto mayatima wao kwao itakuwa halali kuitumia maan chumo lao ni halali (sadaka/kugaiwa/msaada)
 
Wapi nimesema Ali kiba ni jambazi??!

Unajua ni kwanini mzee Yusufu aliacha kuimba? Coz dini anayoiamini hairuhusu alichokua akikifanya,nadhani utakua umeelewa kama ulikua na lengo la kueleweshwa na si kingine.
Unajua kilicho nyuma ya pazia kuhusu kuacha mziki mzee yusuph? Tulia ukiambiwa hutaamin miaka kumi ijayo.. Ila kumbuka tu kila siri itajulikana
 
hakuna pesa chafu/haramu ila kuna kipato kichafu/haramu...hela inaweza kwako ikawa haramu kuitumia lakini hela hiyo hiyo ni halali kwa mwengine kuitumia..eg. pesa yako inaweza ikawa chanzo chake ni dawa za kulevya, kwako wewe hii hela ni haramu kuitumia kwani haitokani na pato halali, lakini pesa hiyo hiyo ukiichukua halafu ukawapelekea watoto mayatima wao kwao itakuwa halali kuitumia maan chumo lao ni halali (sadaka/kugaiwa/msaada)
Kwa hiyo ukiletewa pesa aliyohongwa binti yako baadaya uzinzi ni halali kwako kuitumia?
 
Nakuahid nitaileta lakin lazima kwanza tuwe na subira
mitanzania bana basi hapo hata kazi hataki fanya kutwa kushinda kijiweni na kila siku kuwapa watu moyo wa ntawasimulia story..we kama unajua weka madini juu ya meza zaidi ya hapo ni kuchafuana na kutafuta kiki tu...drake mwenyewe mbele wamemchana amezaa na malaya ije kua weye na story yako na mzee yusuph...shubamiit
 
huyo anajion san hat mzee wa upako kashasem firdaus ataisikia tu
 
Back
Top Bottom