Ali Kiba ndo kajimaliza kimuziki...

Mbona walisema eti Sold out!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Labda si show ya Manhattan. Show ya Manhattan (New York City, West Side Highway) ili flop vibaya sana mpaka ikawa aibu.

Very disorganized. Mpaka Diamond aliyetakiwa kuwa main event akawa opening act.

Halafu Diamond si professional, ana zile za kungoja watu wajae, kumbe watu hawajai mpaka mwisho.

Nishaona show ya Everton Blender Dar. Ili flop. Blender alisema show yake ikiwa na watu 10 au 10,000 anapiga vile vile.

Na kweli.

Uwanja wa taifa ulikuwa karibu mtupu, hata watu 500 sijui kama walifika, lakini Blender alipiga bonge la show.
 
Aisee uliletwa uzi humu kuhusu hizo show kama kawaida aliyesema ukweli alionekana hater......nadhani Kuna tatizo mahali!
Enzi zile diamond walikuwa level moja na davido!
Leo hii hata hapa bongo ana ugomvi na kila media!
Kwanini hawa wanaojiita mameneja hawalioni hilo?
 
Tafuta video kama unaweza kupata genuine video inayoonesha crowd katika show hiyo.
Nilikiwa naongea na dada mmoja alienda ndiyo akaniambia habari hizi. Analalamika anasema haendi show ya Diamond tena.

Nikamwambia haya mambo mengine wengine tunaweza kutabiri hata kabla hayajatokea. Unafanya show bila promo ya kutosha kwa wabongo Manhattan katikati ya wiki unategemea nini?
 
Watu watamzoea na thamani take kimuziki itapungua,kila siku tunamwona na nyimbo zake ni zile.
Nani aende kuangalia show?
 
Afu mara nyingi huwa siwapendi watu wanaochukia mafanikio ya mtu wakati wenyewe hawana hata cha kutuonesha.... duuuh wivu huu utatuua.... huyu mond anayesemwa kuwa hawezi kujaza uwanja kaenda huko MADAGASCAR kafanya kufuru.... kajaza uwanja wa mpira... one man army.... Sijui hiz fyokofyoko za nini? Go Simba goooo.....!!!!! Angalia hizo video ndo uone sio kupandikiza chuki tu kwa watu....
 

Attachments

Afu mara nyingi huwa siwapendi watu wanaochukia mafanikio ya mtu wakati wenyewe hawana hata cha kutuonesha...

Sijaongelea mtu, nimeongelea idea, kama una akili fupi lazima utaishia kuona nimeongelea mtu hata kama nimeongelea idea.

Small minds discuss people, average minds discuss events, great minds discuss ideas.

. duuuh wivu huu utatuua....

Mazee kushare habari kwamba Diamond hakupata watu Manhattan ni wivu? Mimi nashindanaje na Diamond wakati si mwanamuziki na maisha yangu na ya Diamond tofauti kabisa? Naanzaje kumuonea wivu mtu ambaye simjui? Maisha yangu yako poa, nimuonee wivu Diamond kwa nini?

Kwa kuandikwa kwenye magazeti kila siku? Wakati mimi napenda privacy katika maisha yangu?

Hizi habari za kuita criticism ni wivu ni moja ya sababu Watanzania hatuendelei, hawa wasanii wanatakiwa wajifunze kuwa professionals na kwenda kwenye standards za kimataifa, watu wakisema hilo, hilo si wivu.

Wachukulie kama constructive criticism. Unaelewa constructive criticism ni nini?

Usilete mahaba kwenye watu wanaoongea kwa principles ndefu zaidi ya mihemuko ya ushabiki.

huyu mond anayesemwa kuwa hawezi kujaza uwanja kaenda huko MADAGASCAR kafanya kufuru....

Madagascar si New York City ndugu yangu, sijataja Madagascar, sijui ya Madagascar, nmetaja ya New York City ninakokaa.

kajaza uwanja wa mpira... one man army.... Sijui hiz fyokofyoko za nini? Go Simba goooo.....!!!!! Angalia hizo video ndo uone sio kupandikiza chuki tu kwa watu....

Wwapi nimesema Diamond hawezi kujaza uwanja wa mpira?

Nimesema New York City hakupata watu, tena wala sijasema hajapata watu kwa makosa yake, nimeongelea issues za lack of promotion na bad timing.

Ila mtu unayeendekeza ushabiki badala ya kujua kusoma kama wewe utaona nimemlaumu Diamond kwa kukosa watu.

Wakati Diamond si mtu anayefanya promotion ya show yake, kuna promoters na team kubwa tu ambayo ina kazi hii.

Obviously hujui kusoma, una matatizo ya elimu ya msingi na unaendekeza ushabiki zaidi ya uchunguzi wa facts.

Fact ni kwamba show ya Diamond ya New York City ime flop, na hicho ndicho nilichoandika.

Sijaandika Diamond hawezi kujaza uwanja, sijasema hajajaza uwanja Madagascar.

Sasa kwa nini unaleta mambo ambayo mimi sijasema kama mimi nimesema?

Unajua kusoma wewe?
 
@kiranga katika ubora wake, nafikiri amekuelewa...
 
Lots of words lakin nonsence kilichoandikwa...... siwezi kubishana na na wewe coz huna idea na soko la muziki unaandika kulingana na hisia zako zinavokutuma.... so fanya yako usepe....
 
Lots of words lakin nonsence kilichoandikwa...... siwezi kubishana na na wewe coz huna idea na soko la muziki unaandika kulingana na hisia zako zinavokutuma.... so fanya yako usepe....
Wewe unayesema sina idea na soko la muziki, huna idea idea ni nini.
 
achana nae shoga huyo asiejielewa
 
Wewe unayesema sina idea na soko la muziki, huna idea idea ni nini.
Mtu anayekaa new york ananiuliza mimi nini maana ya idea? Rudia tena kuzamia labda umezamia mtaa wa mateja πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Diamond majuzi kaja New York City.

Kapiga show.

Hata watu 50 hakupata.

Na kati ya hao 30 walikuja kuwaangalia ma star wa Caribbean. Wabongo walikuwa kama 20 tu.

Nikasema mi nilijua haya yatakuwa hivi kabla hayajatokea.

Diamond alikuwa na US tour?
 
Mtu anayekaa new york ananiuliza mimi nini maana ya idea? Rudia tena kuzamia labda umezamia mtaa wa mateja πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wewe ndiye unataja "idea" hapa?
 
Mtu anayekaa new york ananiuliza mimi nini maana ya idea? Rudia tena kuzamia labda umezamia mtaa wa mateja πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Duh! Unajua kusoma na kuelewa ulichokisoma?
 
achana nae shoga huyo asiejielewa
Ukiona mtu kama huyu huna haja hata ya kujiuliza mara mbilimbili.... kaja kutangaza biashara zake huku.... hakuna mabasha huku bhana kajitangaze kwingine.... Toa koment inayohusiana na mada husika sio kuleta matangazo ya biashara hapa
 
Diamond alikuwa na US tour?
Yani swali lako rais wa wabeba box linaonesha jinsi hizi shows zilivyokosa promo.

Alikuwa hapo Manhattan, show imeflop, amepata about 50 people, most of those, about 30, walikuja kuangalia ma star wengine wa Caribbean, wabongo walikuwa kama 20 hivi.

Show imewekwa katikati ya wiki halafu hakukuwa na promo ya kutosha.

Next nikawa naona message za Whatsapp tunaombwa tutokee shows zinazofuata shows zipate watu.

Nikija ku state facts hapa, washabiki wengine wanaendekeza ushabiki kuliko analysis.
 
Wewe ndiye unataja "idea" hapa?
Sawa broe nmekunyaka lakini soko la mziki ni sawa na masoko mengine tu kuna sehemu litabuma na sehemu litabamba.... katika show kumi ambazo mond kafanya US isingewezekana zote akajaza..... afu na ukiangalia ile ya New York ilisababishwa na kubadirisha ukumbi... ule wa mwanzo ilisemekana ulikuwa mdogo... walivobadirisha na idadi ikapungua sana... But nmekuelewa mzee baba
 
Katika yote uliyoyaandika hapo, kwa nini unafikiri mimi katika maneno yangu niliyoandika nimepingana na neno hata moja ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…