Ali Kiba ni mseja

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
HUWEZI KUSHINDANA NA WANADAMU
1. Ukiwa single watakuuliza, kwanini huna Girlfriend au Boyfriend?
2. Ukiwa na mchumba, watahoji mmekaa sana mtaoana lin?
3. Ukioa utasikia, mbona hamzai nyie?sisi twataka wajomba,shangazi na wajukuu
4. Mkizaa watakuja na hii, mtoto kakua mtafutieni dada au kaka yake!
5. Ukimtafuta, utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha?maisha magumu siku hizi .....

UKIWA NA HELA
1. Ukinenepa wanakwambia we unanenepa tu hivi huogopi magonjwa (presha na kisukari)
2. Ukikonda, acha ubahili, pesa zote hizo unakuwa mbahili? wengine watasema mara alitembeaga na dada/ kaka fulani mwenye ngoma ndio imekolea sasa. Hamalizi mwaka huyu, lazima tumzike tu.
3. Ukinunua gari, unanunuaje gari wakati hujajenga? huna kiwanja? Vijana wa siku hizi bure kabisa.
4. Ukijenga huna gari, yaani na usumbufu wote huu wa madaladala huna gari? tunakushangaa sana. Nunua hata pikipiki!!

UKIFANYA MAZOEZI
1. Kama ni mwembamba, wee kimbau mbau unapunguza nini kwenye ako kamwili kako, (wanajua mazoezi ni kupunguza mwili tu!)
2. Ukiwa Mnene, yaani Mungu hakupi vyote. Ona sasa amekula mikuku yake sasa ndio anateseka nayo kupungua.

DEDICATION : HAUWEZI KUSHINDANA NA MWANADAMU MWENYE KINYWA

JALI MAMBO YAKO NA UYAFANIKISHE KWA MKONO WA MUNGU HAUTASHINDWA
 
Cha msingi, na ndio tunaimba humu kila siku, ni kwamba , MAISHA HAYANA FORMULA, ukitambulia hili, utaishi kwa raha sana. Anaejaribu kukupa kanuni /formula ameteseka sana, na ataendelea kuteseka, hivyo anatafuta wa kumtesa na yeye.
 
Alieelewa anisaidie kunichakatia au kunyambua lengo la ujumbe
 
KILA MTU ANAPASWA KUISHI ATAKAVYO ILI MRADI HAVUNJI SHERIA WALA KUWAKWAZA WENZIE
 
Ukinywa pombe watakwambia unaharibu hela, ukivuta cha Bulawayo watakwambia itakutia uchizi, sasa sijui tufanze nini?
 
Ulimwengu hadaa walimwengu shujaa
 
Wanadamu bana! Ukiishi kwa kumfurahisha mwanadamu utaharibikiwa vibaya.
Wengine oooh mbona haoi au mbovu? Mwishoweunakimbilia kuoa ili uwakomoe kumbe anangoma.Hapo sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…