Ali Kiba: Sijaachana na mke wangu, nimemruhusu arudi kwao

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
DAR ES SALAAM,TANZANIA.

Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba amesema hajaachana na mkewe bali amemruhusu arejee kwao Kenya kufanya kazi kama alivyomuomba.
Amesema licha ya uamuzi wake huo, siku za hivi karibuni walikuwa na mgogoro lakini wameumaliza.
Tetesi za kuvunjika kwa ndoa hiyo zilianza Julai, 2019 lakini hivi karibuni zilishika kasi zaidi.
Akizungumza jana Alhamisi Septemba 19, 2019 katika kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa na Redio Clouds, Ali Kiba amesema yanayosemwa kuhusu ndoa yake, yenye ukweli ni asilimia moja tu.
Amesema ukweli huo wa asilimia moja ni kuwa hivi sasa haishi na mkewe, ulitokea mgogoro kati yao lakini wameumaliza.

"Katika kila ndoa hakukosi mgogoro, na kwangu ndivyo ilivyotokea lakini namshukuru Mungu tuliyamaliza na sasa tupo sawa."
"Nawashauri watu wasipende kufurahia kuvunjika kwa ndoa za wenzao kwa kuwa jambo hilo Mungu ndio analiunganisha, " amesema Ali Kiba. .
Amebainisha kuwa amelazimika kutoa ufafanuzi kuhusu ndoa yake kwa kuwa ukimya wake unaweza kuleta athari katika familia yake.
"Mimi ninasafiri mara kwa mara na mke wangu huwa anabaki mwenyewe. Mara ya mwisho nilikuwa naenda Ulaya, hakufurahishwa na akaniuliza ninaonaje akarudi kazini kwa kuwa amesoma na ana vyeti vyake."
" Nikaona isiwe tabu nimruhusu kwani anachoongea kina ukweli. Sasa atakaa tu bila kufanya kazi hadi lini, hivi ninavyoongea yupo kwao Mombasa lakini bado tunawasiliana vizuri tu," amesema msanii huyo.
Ameongeza, "Hata leo (jana) nimeongea naye na sijawahi kumpa talaka licha ya changamoto zilizotokea hapo katikati."

Credit : Mwananchi
 
Vizuri na tunawaombea busara na upendo ktk ndoa yenu idumu.
 
Ndoa ngumu sana,jamaa kamruhusu aende Mombasa,yeye anabaki Tz... bilashaka kashaona hata akimsaliti haina shida,na mkewe kaona hata akisalitiwa na Kiba,hamna shida,ndoa bhana.
 
Ndoa ngumu sana,jamaa kamruhusu aende Mombasa,yeye anabaki Tz... bilashaka kashaona hata akimsaliti haina shida,na mkewe kaona hata akisalitiwa na Kiba,hamna shida,ndoa bhana.
Masuala ya ndoa muachie Mungu na wahusika wenyewe......
 
He does't have to explain to anyone about her private life...

Kuna watu watasema, hilo ndiyo tatizo la wanawake wasomi, ujuaji mwingi...


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…