Ali Kiba unakwama wapi mdogo wangu?

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Hebu cheki kijana wa juzi juzi tu Harmonize anavyobamba kila kona, kachangamsha mitaa kwa album iliyosheheni mikwaju,wewe huskiki kabisa siku hizi.

Tulikutegemea uje umchalenji Diamond umetuangusha, atleast Konde anafanya kile tulichotarajia kutoka kwako japokuwa na yeye bado sana kufika level zile ila kwa kudra za Mungu atafika.

Basi tuache hilo mdogo wangu tunajua mualiko ulikataa kata kata kama ilivyo kawaida yako roho ya kukunja, basi toa hata hongera tu kwa kijana Konde kama walivyofanya wenzako wakina WCB kiroho safi kuonyesha kama unajali.

Usione wivu mdogo wangu maisha ndivyo yalivyo leo wewe kesho yeye.
 
Wabongo bana unataka mtu afanye unavyotaka wewe. Si umchukue mke wako na familia yako mtengeneze band muanze kuimba na muwe mnaenda kwenye mialiko bila kusahau kuanza kumchalenji diamond

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahhaaa...
Mbaya zaidi jamaa yupo kimyaaa anaendelea na mambo yake ila raia sasa wanavyoteseka!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…