Ali Seif mmiliki wa Kagera Sugar na mmiliki mpya wa Tongaat South Africa amelipa kodi Tanzania?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Mjomba mtata wa Oman,Mmiliki wa Superdoll anaacha kulipa kodi Tanzania anaenda kuwekeza Afrika kusini, je, huu ni Uzalendo?

NBC mliipiga mkapata mtaji,lakini hamlipi fadhila kwa Taifa letu.

Kila siku danadana ila kwenye majarida ya kimataifa anaandikwa kwa wino mweusi "billionaire" sasa Tanzania inanufaikaje hapo?

Seif - Kagera Sugar,Superdoll

Nassor - Mtibwa Sugar
 
Mjomba mtata wa Oman, anaacha kulipa kodi Tanzania anaenda kuwekeza Afrika kusini, je, huu ni Uzalendo?

Kila siku danadana ila kwenye majarida ya kimataifa anaandikwa kwa wino mweusi "billionaire" sasa Tanzania inanufaikaje hapo?
Mkuu, punguza hasira, kubali kwamba tushaliwa, sasa kaa utulie na uandike habari kwa kina ili tuelewe, maana hapo ni umeelewa wewe peke yako kwa kuwa tarifa yote unayo wewe
 
Mjomba mtata wa Oman, anaacha kulipa kodi Tanzania anaenda kuwekeza Afrika kusini, je, huu ni Uzalendo?

Kila siku danadana ila kwenye majarida ya kimataifa anaandikwa kwa wino mweusi "billionaire" sasa Tanzania inanufaikaje hapo?
Kagera Sugar ina wenye hisa viongozi wastaafu wa nchi hii. Usishangae kama anawatunzia viongozi hao.
 
Mtibwa Sugar.
Super Doll.
Super Star Freight.
Kilombero Sugar.
Kagera Sugar.
Bagamoyo Sugar.
Vodacom Tanzani.
Caspian Constructions.
Taifa Gas.
Lake Group.
Azam Group.

Hizo zote wamo viongozi wakuu wastaafu,waliopita na waliopo.
 
Back
Top Bottom