Alibaba na wezi 40

Alibaba na wezi 40

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
ALIBABA NA WEZI 40
SURA YA KWANZA:
HAZINA KATIKA PANGO


Hapo zamani za kale katika mji wa persia waliishi ndugu wawili mmoja aliitwa Kasim na mwengine aliitwa Alibaba, ndugu hawa wawili walikuwa na baba yao ambae alikuwa na uwezo wa kifedha kidogo ambae alipokufa waligawana mali zake mgao sawa kwa sawa bila kumzidishia yeyote baina yao, na wala hawakuwa na muda wa kupoteza na kuzitumia mali zile zote.

Mkubwa kati ya wale vijana wawili ambaye ni Kasim alioa mwanamke ambae ni mtoto wa mfanya biashara tajiri, hivyo basi, baba mkwe wake alipotangulia mbele ya haki (kufa) alimiliki duka kubwa lililokuwa na bidhaa adimu pamoja na bidhaa zenye thamani kubwa na pia alimiliki bohari kubwa iliyokuwa na vyombo vyenye thamani kubwa ukiachilia mbali dhahabu nyingi sana ambazo zilikuwa zimefukiwa ardhini.

Hivyo basi alijulikana karibuni mji mzima kama mtu aliye thabiti au imara mwenye nguvu lakini mke aliyemuoa Alibaba alikuwa masikini na tegemezi hata hivyo waliishi katika kibanda duni.

Alibaba alijikimu maisha yake kwa kuuza kuni alizokuwa akikusanya kutoka msituni na kupeleka mjini sokoni kwa kutumia punda wake watatu.

Ilitokea siku moja Alibaba alikuwa akikata matawi yaliyokufa na kukausha kuni zilizotosheleza kwa mahitaji yake, na baada ya hapo akaweka mizigo yake juu ya wale wanyama wake (punda).

Mara ghafla akaona kama wingu la vumbi likiwa linapanda juu angani kwa mbali upande wake wa kulia huku likiwa linakuja upande alioko, lilipofika karibu aliona kundi la waendesha farasi wakiwa wanakuja upande alioko na walikuwa karibuni kumfikia.

Kwa muda huo alikuwa kakata tamaa na kuogopa huenda wale wakawa ni majambazi ambao wanaweza kumuua na kuchukua punda wake, kwa uwoga wake akaanza kukimbia. Lakini kwakuwa walikuwa tayari wamefika karibu na hakuweza kutoka nje ya ule msitu, aliwaficha wanyama wake vichakani naye kujificha kwenye mti mkubwa ambapo alikaa kwenye tawi ili aweze kuona kila kinachoendelea pale na wakati huo hakuna yeyote chini aliyeweza kumuona huko juu aliko. mti ule uliota pembeni kidogo ya mwamba ambao ulikuwa mrefu.

Waendesha farasi, vijana, wenyenguvu na mashujaa walikuja karibu na uso wa ule mwamba na wote wakashuka kwenye farasi wao kitendo ambacho kilifanya Alibaba awaone vizuri watu wale na mara akapata hisia kutokana na muonekano na mwenendo wa tabia za wale watu kwa jinsi alivyowaona ni waporaji ambao wamepora na sasa wameleta mali za uporaji kuja kuziweka katika eneo lile kwa nia ya kuzificha, vilevile aligundua kuwa idadi ya wale watu ilikuwa arobaini (40).

Alibaba aliwaona wale majambazi na walipofika chini ya ule mti kila mmoja alimfunga farasi wake pale, halafu kila mmoja alishusha mizigo yake ambayo Alibaba aligundua kuwa kulikuwa na madini ya dhahabu na fedha ndani yake. Mtu mmoja kati yao ambae alionekana kuwa ndiye kiongozi wao aliendelea mbele huku akiwa na mzigo kwenye bega akipita kwenye mibamiba na vichaka mpaka alipofika sehemu moja kwenye alama chini kama doa hivi akasimama pale halafu akatamka maneno fulani akisema “ Funguaaaaa, Sesmiii!!” na mara moja ukafunguka mlango mkubwa kwenye uso wa ule mwamba, baada ya hapo wezi wote wakaingia mle ndani na mwisho akaingia kiongozi wao kisha lile lango likajifunga lenyewe.

Muda mrefu walikaa ndani ya lile pango huku Alibaba akiendelea kukaa juu ya ule mti akihofu kwamba kama akishuka huenda mude uleule na wale wezi wanaweza kutoka na kumuona kisha wakamuua. Lile lango lilipofunguka tu wa kwanza kutoka alikuwa ni kiongozi wao akaenda kwenye lile doa kisha akawahesabu wale wenzake mpaka walipoisha kutoka wote kisha akasema “ Fungaaaaaaa, Sesmiiii!!” na hapo lango likajifunga. Walipomaliza kukutana wote kila mmoja alichukua mizigo yake na kuondoka wote eneo lile wakiongozwa na kiongozi wao wakielekea kule walikotokea. Alibaba aliendelea kukaa juu ya ule mti huku akiangalia safari ya wale wezi wanapoondoka. Akaona asubiri mpaka wapotee kabisa kwa maana asije mmoja akarudi na kumkuta mahali pale.

Walipopotea kabisa mbele ya macho yake Alibaba akashuka kutoka mtini na kwenda mpaka pale kwenye lile doa kisha akajisemea mwenyewe “nitajaribu kutamka maneno yale ya ajabu nione kama kwa kutamka kwangu lile lango litafunguka na kufunga” kisha akasema kwa kelele yale maneno “Funguka, Sesame!!” alipomaliza tu kutamka mara lango likafunguka, kisha akaingia ndani yake.

Akaona pango kubwa lenye kuba likiwa na urefu upatao kadiri ya urefu wa mtu aliekuwa mrefu zaidi duniani, pango lile lilikuwa limezungukwa na mawe na lilikuwa likipitisha mwanga kupitia vitundu vidogovidogo vilivyokuwa katika pango lile na kushangazwa alipoona limejaa kila aina ya bidhaa mle ndani na kumerundikwa kutoka chini mpaka juu rundo la mizigo ya hariri na nguo nzuri zilizotiwa nakshi na matuta juu ya matuta ya makapet na mazulia yenye rangi tofauti na pia aliona sarafu za dhahabu na fedha zikiwa nyingine zimezagaa chini na nyingine zikiwa ndani ya mifuko. Kwa kuona wingi wa mali hizi Alibaba alijifikiria moyoni kuwa sio kwa miaka michache tu, hii itakuwa ni karne na karne wezi wanapora mali za watu na kuja kuzificha humu. Je nini kitaendelea humo pangoni?
 
ALIBABA NA WEZI 40
SURA YA KWANZA:
HAZINA KATIKA PANGO


Hapo zamani za kale katika mji wa persia waliishi ndugu wawili mmoja aliitwa Kasim na mwengine aliitwa Alibaba, ndugu hawa wawili walikuwa na baba yao ambae alikuwa na uwezo wa kifedha kidogo ambae alipokufa waligawana mali zake mgao sawa kwa sawa bila kumzidishia yeyote baina yao, na wala hawakuwa na muda wa kupoteza na kuzitumia mali zile zote.

Mkubwa kati ya wale vijana wawili ambaye ni Kasim alioa mwanamke ambae ni mtoto wa mfanya biashara tajiri, hivyo basi, baba mkwe wake alipotangulia mbele ya haki (kufa) alimiliki duka kubwa lililokuwa na bidhaa adimu pamoja na bidhaa zenye thamani kubwa na pia alimiliki bohari kubwa iliyokuwa na vyombo vyenye thamani kubwa ukiachilia mbali dhahabu nyingi sana ambazo zilikuwa zimefukiwa ardhini.

Hivyo basi alijulikana karibuni mji mzima kama mtu aliye thabiti au imara mwenye nguvu lakini mke aliyemuoa Alibaba alikuwa masikini na tegemezi hata hivyo waliishi katika kibanda duni.

Alibaba alijikimu maisha yake kwa kuuza kuni alizokuwa akikusanya kutoka msituni na kupeleka mjini sokoni kwa kutumia punda wake watatu.

Ilitokea siku moja Alibaba alikuwa akikata matawi yaliyokufa na kukausha kuni zilizotosheleza kwa mahitaji yake, na baada ya hapo akaweka mizigo yake juu ya wale wanyama wake (punda).

Mara ghafla akaona kama wingu la vumbi likiwa linapanda juu angani kwa mbali upande wake wa kulia huku likiwa linakuja upande alioko, lilipofika karibu aliona kundi la waendesha farasi wakiwa wanakuja upande alioko na walikuwa karibuni kumfikia.

Kwa muda huo alikuwa kakata tamaa na kuogopa huenda wale wakawa ni majambazi ambao wanaweza kumuua na kuchukua punda wake, kwa uwoga wake akaanza kukimbia. Lakini kwakuwa walikuwa tayari wamefika karibu na hakuweza kutoka nje ya ule msitu, aliwaficha wanyama wake vichakani naye kujificha kwenye mti mkubwa ambapo alikaa kwenye tawi ili aweze kuona kila kinachoendelea pale na wakati huo hakuna yeyote chini aliyeweza kumuona huko juu aliko. mti ule uliota pembeni kidogo ya mwamba ambao ulikuwa mrefu.

Waendesha farasi, vijana, wenyenguvu na mashujaa walikuja karibu na uso wa ule mwamba na wote wakashuka kwenye farasi wao kitendo ambacho kilifanya Alibaba awaone vizuri watu wale na mara akapata hisia kutokana na muonekano na mwenendo wa tabia za wale watu kwa jinsi alivyowaona ni waporaji ambao wamepora na sasa wameleta mali za uporaji kuja kuziweka katika eneo lile kwa nia ya kuzificha, vilevile aligundua kuwa idadi ya wale watu ilikuwa arobaini (40).

Alibaba aliwaona wale majambazi na walipofika chini ya ule mti kila mmoja alimfunga farasi wake pale, halafu kila mmoja alishusha mizigo yake ambayo Alibaba aligundua kuwa kulikuwa na madini ya dhahabu na fedha ndani yake. Mtu mmoja kati yao ambae alionekana kuwa ndiye kiongozi wao aliendelea mbele huku akiwa na mzigo kwenye bega akipita kwenye mibamiba na vichaka mpaka alipofika sehemu moja kwenye alama chini kama doa hivi akasimama pale halafu akatamka maneno fulani akisema “ Funguaaaaa, Sesmiii!!” na mara moja ukafunguka mlango mkubwa kwenye uso wa ule mwamba, baada ya hapo wezi wote wakaingia mle ndani na mwisho akaingia kiongozi wao kisha lile lango likajifunga lenyewe.

Muda mrefu walikaa ndani ya lile pango huku Alibaba akiendelea kukaa juu ya ule mti akihofu kwamba kama akishuka huenda mude uleule na wale wezi wanaweza kutoka na kumuona kisha wakamuua. Lile lango lilipofunguka tu wa kwanza kutoka alikuwa ni kiongozi wao akaenda kwenye lile doa kisha akawahesabu wale wenzake mpaka walipoisha kutoka wote kisha akasema “ Fungaaaaaaa, Sesmiiii!!” na hapo lango likajifunga. Walipomaliza kukutana wote kila mmoja alichukua mizigo yake na kuondoka wote eneo lile wakiongozwa na kiongozi wao wakielekea kule walikotokea. Alibaba aliendelea kukaa juu ya ule mti huku akiangalia safari ya wale wezi wanapoondoka. Akaona asubiri mpaka wapotee kabisa kwa maana asije mmoja akarudi na kumkuta mahali pale.

Walipopotea kabisa mbele ya macho yake Alibaba akashuka kutoka mtini na kwenda mpaka pale kwenye lile doa kisha akajisemea mwenyewe “nitajaribu kutamka maneno yale ya ajabu nione kama kwa kutamka kwangu lile lango litafunguka na kufunga” kisha akasema kwa kelele yale maneno “Funguka, Sesame!!” alipomaliza tu kutamka mara lango likafunguka, kisha akaingia ndani yake.

Akaona pango kubwa lenye kuba likiwa na urefu upatao kadiri ya urefu wa mtu aliekuwa mrefu zaidi duniani, pango lile lilikuwa limezungukwa na mawe na lilikuwa likipitisha mwanga kupitia vitundu vidogovidogo vilivyokuwa katika pango lile na kushangazwa alipoona limejaa kila aina ya bidhaa mle ndani na kumerundikwa kutoka chini mpaka juu rundo la mizigo ya hariri na nguo nzuri zilizotiwa nakshi na matuta juu ya matuta ya makapet na mazulia yenye rangi tofauti na pia aliona sarafu za dhahabu na fedha zikiwa nyingine zimezagaa chini na nyingine zikiwa ndani ya mifuko. Kwa kuona wingi wa mali hizi Alibaba alijifikiria moyoni kuwa sio kwa miaka michache tu, hii itakuwa ni karne na karne wezi wanapora mali za watu na kuja kuzificha humu. Je nini kitaendelea humo pangoni?
SEHEMU YA PILI
54831818.png


Kutoka sehemu ya kwanza:

Baada ya Alibaba kuingia pangoni na kuona mali zote zile na kujisemea moyoni kuhusu mali zile:

Kwa kuona wingi wa mali hizi Alibaba alijifikiria moyoni kuwa sio kwa miaka michache tu, hii itakuwa ni karne na karne wezi wanapora mali za watu na kuja kuzificha humu.




ENDELEA SEHEMU YA PILI

“Hazina nyingi kiasi gani hiki!!” alisema Alibaba. ‘na sasa nimezipata’ alifikiri kidogo. ‘wezi hawa hawawezi kukaa na mali yote hii. Lazima nichukue kiasi cha dhahabu nikajiwekee mwenyewe nyumbani.’

Alisema tena yale maneno “Fungukaa sesmiiii” na lango likafunguka, kisha akenda kuwachukua punda wake watatu aliokuwa amewaficha vichakani.

“Leo ninawapa habari njeeema” aliwaambia punda wake. “leo mtabeba dhahabu na sio kuni kama mlivyozoea kila siku. Aliwachukua punda wake mpaka karibu na lile pango na kuwaacha nje kasha yeye akaingia tena ndani. “Punda watatu na makapu sita” Alisema alibaba, “Nitajaza makapu yote haya sita dhahabu”. Alibaba alichukua makapu yale sita na kujaza kila aina ya dhahabu zilizopo ndani ya lile pango kisha akachukua baadhi ya kuni chache tu kuziweka juu ya kila kapu ili kuzificha zile dhahabu ndani ya kapu zisionekane na watu akiwa njiani, kisha akatoka na kusimama mbele ya lile pango kwa nje na kusema “Fungaaaa Sesmiii!!!” lile pango likajifunga kwa sauti kubwa, Alibaba alitabasamu na kuondoka kuelekea mjini.

73793894.png


Alibaba hakuelekea sokoni kama kawaida yake siku zote, badala yake aliwaongoza punda wake mpaka nyumbani kwake. Aliwapeleka mpaka kwenye kibanda chao na kufunga mlango, kisha akatoa zile kuni chache alizoweka juu ya kapu na kubakia na kapu zake sita zikiwa zimejaa dhahabu.

Alisubiri mpaka giza lilipoingia. Hakutaka mtu yeyote aone hazina ile. Alizichukua kutoka kwenye banda la punda wake na kuzipeleka mpaka ndani kwake kisha akazimimina zote chini fungu moja. Akamuita mke wake kutoka jikoni.

“Angalia!” alisema Alibaba kwa furaha. “sisi ni matajiri sasa mke wangu!, sitafanya tena kazi ya kukata kuni!, tutaweza kula vyakula vizuri vizuri sasa na kuvaa mavazi mazuri!”

Mke wa Alibaba alipoziona zile dhahabu, alishangaa sana. “sijawahi kuona dhahabu nyingi kiasi hiki!” alisema kwa mshangao huku akipepesa macho. ‘lakini Kassim ndiye tajiri, na sio wewe!, umezipata wapi hizi? Au umeziiba? .

Basi Alibaba alimpa stori nzima juu ya wale watu 40 na maajabu ya lile pango na mali zilizopo mle ndani.

“Umeona sasa!” Alisema alibaba “kwahiyo nimeziiba, lakini nimeziiba kutoka kwa wezi hivyo hakuna tatizo lolote. Sasa itakuwa vizuri ukiitunza siri hii, usimwambie mtu yeyote kuhusu hizi dhahabu zetu. “sawa” alijibu mke wake, “itabidi tuchimbe shimo na kuzihifadhi humo, hapo zitakuwa salama. Lakini kabla ya kufanya hivyo itabidi tuzipime ili tujue tuna dhahabu kiasi gani. Nitakwenda kwa kassim na kumuazima mke wake mizani”.

“Hilo wazo zuri sana” alisema Alibaba, “nenda kaazime hiyo mizani kwa mke wa Kassim wakati mimi huku nachimba shimo”

Mke wa Alibaba alitoka kuelekea kwa Kassim ambapo ni pembeni kidogo ya mtaa wao. Alifika na kusimama nje ya jumba kubwa la Kassim na kugonga mlango mkubwa wa mbao. Alipokuwa akisubiria kuja kufunguliwa, alisema moyoni huku akitabasamu, “ Sasa mimi na Alibaba tunaweza kununua nyumba kubwa ya kifahari kama hii”.

Mmoja wa watumishi wa Kassim alikuja kumfungulia mlango na kumpeleka mpaka sebuleni alipokuwa amekaa mke wa Kassim.

“Tafadhali, unaweza kuniazima mizani yako?” Alimuomba mke wa kassim “ Nataka kupimia nyama na nitakurudishia baadaye usiku huu huu”

Mke wa Kassim alikunja uso kwa mshangao. “Alibaba ni masikini” Alijisemea moyoni. “Lakini mke wake anataka kupima nyama. Nyama ni ghali sana. Amepata wapi hela ya kununua nyama huyu?.

“Ndio nitakuazima mizani” mke wa Kassim alisema. “Nitaenda kukuchukulia zipo jikoni”.

Wakati mke wa kassim yupo jikoni, akazishusha zile mizani kutoka kwenye shelfu kisha akachukua asali na kupaka kwenye kitako cha mizani ile. “lazima nijue aina gani ya nyama anayopima, lazima itaganda huku chini ya mizani na nitajua ni nyama ya aina gani” Alijisemea moyoni mke wa kassim huku akielekea sebuleni kumpelekea ile mizani. “hii hapa, unaweza kukaa nayo muda wowote tu unaotaka” Alimpatia mke wa Alibaba. Kisha akaondoka.

Mke wa Alibaba alipofika nyumbani alifanya haraka sana kupima dhahabu zile na kwa furaha kubwa sana alimkimbilia mumewe kule alipokuwa akichimba shimo.

“Mume wangu!!” alisema mke wa Alibaba, “sisi kwa uhakika ni matajiri kabisaaaaa, tuna dhahabu nyingi sana za kutosha kwaajili ya maisha yetu yote yaliyobaki”.

Alibaba alipiga makofi na kucheka. “Ni furaha iliyoje” Alisema Alibaba, “mtoto wetu Khalid atakuwa tajiri na mwenye furaha pia!, zirudishe hizo mizani haraka, hatutaki Kassim na mkewe wajue siri yetu hii”

Hivyo basi, mke wa Alibaba alichukua zile mizani na kuzirudisha kwa mke wa Kassim. Hakuona dhahabu ambayo ilikuwa imeganda kwenye asali chini ya mizani ile.

“Hii hapa mizani yako” alimpatia mke wa Kassim, “ Nakushukuru sana kwa kuniazima”.

“Karibu sana” mke wa kassim alijibu. “Umeshapima nyama?”

“ooh! Ndio” alijibu mke wa Alibaba, “tena tumepata nyama nyingi”.

Mke wa Alibaba alipoondoka, mke wa Kassim akainua mizani kuangalia chini yake na kuona dhahabu imeganda kwenye ile asali aliyopaka.

“Dhahabu!!!” alisema kwa mshangao mkubwa sana. “Nilijua tu hawa walikuwa na siri!, wamepata wapi hii dhahabu
 
SEHEMU YA TATU

81175334.png

Kutoka sehemu ya pili:

Baada ya mke wa alibaba kurudisha mizani kwa mke wa kassim na kujulikana kilichotendeka huko kuwa sio nyama iliyopimwa bali ni dhahabu. “Nilijua tu hawa walikuwa na siri!, wamepata wapi hii dhahabu?” Alisema mke wa Kassim……… Endelea sehemu ya tatu:


Mumewe aliporudi, alimuonesha ile sarafu ya dhahabu iliyokuwa imeganda chini ya ile mizani. “Angalia mume wangu!” alisema mke wa kassim, “Mke wa Alibaba alikuja kuniazima mizani ili akapimie nyama, mimi sikumuamini nikapaka asali chini ya mizani, na angalia sasa aliporudisha nikaona hii sarafu ya dhahabu imenata huku kwenye asali bila ya wao kujua, na ndio imenisaidia kujua walichokuwa wanakipima”.

14099668.png


Kassim alipoangalia kwenye ile mizani na kuona ile sarafu ya dhahabu alishtuka sana. “Mimi ni tajiri!” alisema Kassim “lakini Alibaba atakuwa tajiri kunishinda mimi, lazima niende nikamuulize amepata wapi dhahabu zote hizi, inaelekea ni nyingi sana mpaka anaamua kuzipima kwenye mizani!!”. Hapana mume wangu” Alijibu mkewe,”Usiende sasa hivi ni usiku sana, wewe lala kwanza upumzike kisha kesho asubuhi ndio uende, lazima watuambie kila kitu, hawawezi kuficha siri hii”. “sawa mke wangu nimekuelewa” alisema Kassim, “nitaenda huko asubuhi”.

Mwisho wa Sura ya Kwanza

SURA YA PILI:

KUINGIA MTEGONI​

Je Kassim alikuwa na furaha juu ya mafanikio ya ndugu yake? Hapana! Hakuwa na furaha bali ni wivu. Kassim hakulala usiku ule na alikuwa hafikirii chochote isipokuwa Alibaba na Dhahabu tu usiku kucha.

“Sio haki kabisa!” alijisemea Kassim. “Nimefanya kazi kwa bidii miaka yote hii kuhakikisha kwamba napata hela za kutosha, na mpaka sasa mimi ni tajiri, lakini Alibaba alikuwa kazi yake ni kukata kuni na kuuza mjini na kupata hela kidogo sana. Amepata wapi dhahabu hizi? Nani atakuwa amempa? Lazima nijue tu na mimi nipate za kwangu”.

Jua lilipochomoza tu, Kassim aliamka huku amekunja sura. “Sio vizuri kabisa!” Alisema. “nitaenda kuzungumza naye nijue kila kitu, ndugu hawawezi kufichiana siri kiasi hiki.”

“Vizuri sana!” alijibu mke wake. “Tena nenda na ile mizani ukamuoneshe sarafu ya dhahabu iliyonata kule chini, hii itasaidia kumfanya atambue kwamba tumeshagundua siri zao.”

“Hilo ni wazo zuri!” alisema Kassim. “kwahiyo nenda jikoni kailete haraka niwahi huko.”

Basi Kassim kwa mwendo wa kasi na wa tamaa kubwa sana kama mtu anayewahi sehemu fulani muhimu sana, alivuka mtaa wa pili mpaka kwa kijijumba kidogo cha ndugu yake Alibaba, kisha akapiga hodi.

Alibaba akaja kumfungulia na ikawa ni ajabu sana kumuona kaka yake pale.

“Habari yako, Kassim”. Alisalimia Alibaba. “Tafadhali ingia ndani na uniambie mbona ni asubuhi sana upo hapa kwangu?”

“Najua siri yako, Alibaba!” alijibu Kassim. “Unasema kwamba wewe ni masikini mkata kuni, lakini kumbe una dhahabu nyingi sana mpaka unazipima! Umezipata wapi ndugu yangu?”

Alibaba akajifanya kama hajui kitu na kushangaa. “Dhahabu?” alisema Alibaba. “una maana gani? Mimi sina dhahabu, mimi ni masikini kama unavyonijua, mimi naenda msituni kila siku kukata kuni, tajiri hafanyi hivyo, ningekuwa tajiri ningekuwa na maisha mazuri, ningekaa katika jumba kubwa la kifahari, ningekuwa nakunywa maziwa na asali”

Baada ya Alibaba kumaliza kusema hayo, Kassim alinyanyua ile mizani usawa wa uso wa alibaba na kutabasamu. “Mkeo aliazima hii jana” Kassim alimwambia Alibaba. “Alisema kwamba alitaka akapimie nyama. Mke wangu alishangaa sana kusikia hivyo, alijua kuwa nyinyi ni masikini sana hamuwezi kununua nyama, hivyo alipata hamu ya kujua kama kweli ni nyama basi ni ya aina gani, hivyo akapaka asali chini yake ili kipande kidogo kikiganda ajue ni nyama ya aina gani mlionunua, lakini kumbe sio nyama ni dhahabu kama unavyoona nimekuja kukuonesha imeganda kwenye asali hapa chini. Unaona sasa, tunajua siri zenu, kumbe mlikuwa hampimi nyama bali ni dhahabu. Nataka uniambie kila kitu kuhusu hizi dhahabu.”

75361533.png


Alibaba hakuwa na la kujitetea na hata mkewe pia alibaki hana la kusema kutokana na kwamba kila kitu kimejulikana na ushahidi wa hilo umeonekana.

Alibaba aliamua kumueleza ukweli wote kuhusu dhahabu zile, alimpa stori yote kuhusu wale watu 40 wenye farasi, na maajabu ya pango lile jinsi linavyofunguka kwa kutamka yale maneno ya ajabu na kufunga kwa kutamka yale maneno ya ajabu, pia alimueleza kuhusu vitu vilivyopo ndani ya pango lile.

“Hiyo ndio stori nzima ya dhahabu hizi” alisema Alibaba.

“Sasa na mimi pia nataka hizo dhahabu!” Alisema Kassim kwa tamaa. “nielekeze hilo pango lilipo na mimi niende”

“Nitakuelekeza hilo pango lilipo”, alijibu Alibaba. “lakini kumbuka kwamba kachukue dhahabu kidogo tu zilizobaki niachie ni za kwangu”.

Kassim akakubali. Alibaba akamuelekeza maeneo lilipo hilo pango. Kassim akaondoka mpaka kwakwe kwaajili ya maandalizi ya kwenda huko pangoni siku inayofuata.

***** MWISHO WA SEHEMU YA TATU *****
 
SEHEMU YA NNE

Kutoka sehemu ya tatu:

Kassim alipoenda kwa ndugu yake na kumshawishi amwambie mahala alipozitoa dhahabu zile, Alibaba hatimaye alimweleza ukweli wote. Sasa Kassim amerudi kwake kujiandaa na safari ya msituni mahala ambapo pango linapatikana.

ENDELEA SEHEMU YA NNE


Asubuhi ilipofika kabla ya jua kuchomoza, Kassim alimuaga mke wake na kuelekea msituni. Alienda huko na punda kumi wenye masanduku makubwa sana mgongoni, Kassim alikuwa ni mwenye tamaa, hakutaka dhahabu kidogo kama walivyokubaliana na ndugu yake, alitaka achukue zote.

Alifuata maelekezo yote ya Alibaba mpaka akafika kwenye jiwe kubwa la rangi ya kijivu, hiyo ndiyo ilikuwa alama. Aliwasimamisha punda wake nje ya pango.

“Sasa ngoja niseme yale maneno” alijisemea Kassim. “Fungukaaaa sesmiii”. Mara pango likafunguka. Kassim alikuwa na shauku na furaha alipoona hivyo, akakimbilia haraka sana ndani ya pango. Alipokuwa ndani ya pango akasema, “Fungaaaaa sesmiiii!!” na hapo pango likajifunga.

40213597.png


Kulikuwa na hazina nyingi sana! Kassim alishusha na kupandisha pumzi kwa nguvu kwa jinsi alivyokuwa haamini macho yake. Kulikuwa na mapande ya dhahabu, sarafu zinazong’aa sana na vito vyenye thamani na rangi nzuri nzuri.

Kila kitu kilikua kinawakawaka kwa mng’aro uliosababishwa na mwanga kutoka nje kwa kupitia matundu madogo ya pango lile. Kassim akachukua bangili zilizotengenezwa kwa madini ya rubi, na akachukua pia mkanda ambao umepambwa na almasi zenye kung’aa sana. Vilevile akachukua mkufu uliotengenezwa kwa madini ya safaya. Rangi yake ni kama rangi ya mbingu. Uzuri gani wa vitu vile ulikuwa siku hiyo!

Kassim alibeba kila kitu anachotaka mle pangoni mafungu kwa mafungu na kuzipeleka karibu na mlango wa pango ili iwe rahisi kuzipeleka kwa wale punda wake kumi wakati atakapolifungua pango lile. Ilikuwa ni kazi ngumu sana. Pia hakutosheka akarudi tena kuchukua sarafu za dhahabu, alibeba mafurushi mengi makubwa makubwa ya sarafu za dhahabu mpaka kwenye mlango wa pango lile. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kukusanya kila kitu na kusogeza kwenye mlango wa pango.

“Sasa ni wakati wa kuondoka”, alijisemea Kassim. “sitaki kukaa hapa muda mrefu mwishowe wale wezi wanikute humu watakaporudi! Nimeshapata mali nyingi sana ya kutosha kujaza masanduku yote kumi yaliyobebwa na punda wangu. Nitarudi kesho na siku inayofuata na inayofuata hivyohivyo mpaka mali yote hii niimalize, lakini kwa leo inatosha wacha tu nirudi nyumbani”

Kwahiyo basi, Kassim akaanza kusema yale maneno ya siri yakufungulia pango lile ili atoke nje. “Fungukaaaaa ……….!!!” Lakini alisahau neno linalofuata! Alijaribu tena, “Fungukaaaa…..uummh!!!” , loh! masikini Kassim kasahau kabisa neno linalofuata. Akajaribu kwa mara nyingine tena. “Fungukaaaa…eeee ssssiiisss!!!, hapana sio hivyo, ah nimeshasahau neno lile! Mlango uliendelea kuwa umefunga kwa kuwa neno lile Kassim hakuweza kulikumbuka ambalo ndio la kufungulia lango lile. Kassim akaanza kutetemeka kwa hofu. Akaanza kuvuja jasho. Alikuwa na hazina nyingi pale kashazikusanya lakini hazitasaidia kitu chochote endapo mlango utashindwa kufunguka.

“Muda wote nilikuwa nafikiria mali tu na kusahau neno la siri!”, alilia Kassim. Alijilaumu sana. “ Sasa nimekamatika leo” alisema Kassim. Alitupa begi la dhahabu alillokuwa amelibeba na kulipiga teke kama mpira wa miguu. “nilifikiri nitakuwa tajiri sana, kumbe ni marehemu mtarajiwa” Alijiwazia Kassim.

Mara Kassim akasikia sauti ambayo ilibadilisha damu yake kuwa barafu. Alisikia sauti za kwato za farasi zikija kwa vishindo kutoka mbali kidogo. Walikuwa ni farasi wapatao arobaini (40) na walikuwa wameshakaribia kufika kwenye mlango wa pango lile.

“Fanyeni haraka! Tuziweke hizi hazina ili tuondoke haraka tukatafute tajiri mwingine wa kumuibia!” Kiongozi wao alisema. Na huku wenzake wakiwa wakicheka. Walikuwa wanakuja kuweka mali pangoni ambazo wametoka kuziiba.

54624831.png


Lakini walipokaribia kufika katika jiwe kubwa la pango, kiongozi wao akaona kitu ambacho kilimkasirisha sana. Kulikuwa na punda kumi waliokuwa wamesimama nje ya pango lile wakiwa na masanduku makubwa juu ya migongo yao.

“Kuna mtu anajaribu kutuibia mali zetu!!”, kiongozi wao alisema. “Lazima tumkomeshe mara moja!!”. Wale wezi walipiga makelele ya hasira huku wakipiga makofi, punda wote kumi walishikwa na hofu na kukimbilia msituni. Kwa taratibu kabisa wezi wote walishikilia panga zao kali huku wakikaribia lango la pango lile.

Fungukaaaaa sesmiii!!!”, alisema Kiongozi wao. Lango kubwa la jiwe likaanza kufunguka. Ghafla Kassim alitoka mbio nje kulekea kwa kiongozi wa wale wezi huku akipiga makelele na kumkamata na kuanza kupigana. Alijitahidi sana kupigana ili aweze kuokoa maisha yake, lakini mmoja kati ya wale wezi alimchoma panga tumboni na hatimaye Kassim akaanguka na kufa palepale.

33613345.png


Wezi wale arobaini walimuacha Kassim chini na kuingia pangoni, “angalia hii mifuko ya dhahabu hapa mlangoni!!” alisema mmoja wa wale wezi, “huyu alikuwa amepanga kuzichukua hizi zote na kuzipeleka kwa wale punda wake kumi!”.

“Alikuwa peke yake huyu?” Aliuliza kiongozi wao. “kwasababu baadhi ya dhahabu zipo hapa mlangoni na zingine hazipo kabisa humu pangoni!, huenda ni zaidi ya mtu mmoja alikuwepo humu pangoni wakiiba hazina zetu! kwahiyo watu wawili wamegundua neon letu la siri la kufunguli apango hili!!”

“Sasa sijui tufanye nini” alisema mmoja wa wale wezi.

“Tumemuua mmoja!” Alisema kiongozi wao. “ Na huyu mwingine tutamtisha kwa njia moja ama nyingine, hatathubutu tena kutuibia chochote hapa!!”. Alinyanyua upanga wake juu hewani huku akitoka nje ya pango.

“Chukua hii maiti ya huyu jamaa mkaining’inize juu ndani ya pango!!” Alisema kiongozi wao. “Mwili wake utakuwa ni onyo kwa yeyote atayekuja humu ndani!”. Ilikuwa inatisha sana.

Hivyo basi, wezi wakachukua kamba na kuuning’iniza mwili wa Kassim juu ndani ya pango na kisha wakatoka kulekea kwenye farasi wao tayari kwa safari ya kwenda mjini tena kuiba.

“Pango letu limeshakaribia kujaa dhahabu” Alisema kiongozi wao. “Na muda si mrefu tutapata nyingine zaidi!”. Baada ya kusema hayo wakaondoka zao wote.
 
SEHEMU YA TANO


Sura ya tatu

MAITI PANGONI

Kutoka sehemu ya nne:

Baada ya Kassim kwenda pangoni kwaajili ya kujipatia dhahabu na mali nyingi, kwa bahati mbaya alisahau neno la siri la kufungulia lango la pango wakati yuko ndani, hivyo alishindwa kutoka nje ya pango na hatimaye kukutwa na wezi wale wenye mali zao na kumuua. Baada ya kumuua wezi wale wakagundua kuwa sio Kassim peke yake anayejua mali zao na kuziiba, bali kuna mtu mwingine. Hivyo wakaamua kuuning’iniza mwili wa Kassim pangoni ili yule mwingine atakayekuja iwe ni somo kwake na onyo.

ENDELEA SEHEMU YA TANO


Siku nzima mke wa Kassim alikaa dirishani akimsubiria mumewe atoke huko pangoni. “Uko wapi Kassim?” alijisemea mwenyewe,”Uko wapi?, kwanini usingebaki na mimi huku? Kwanini ulienda pangoni kutafuta dhahabu?” yote haya alijisemea ingawa hajui kilichotokea huko pangoni.

Mpaka jua lilipozama, mke wa Kassim akaona sasa si muda wa kukaa na kusubiri, lazima kutakuwa na tatizo tu. Akakimbia haraka kwa Alibaba na kugonga mlango.

Alibaba alipofungua tu, aliingia ndani na kuanza kulia. “Alibaba nisaidie, kaka yako tangu alipoondoka asubuhi leo hajarudi mpaka sasa hivi kutoka pangoni! Aliondoka kabla jua halijachomoza vizuri na punda kumi, aliniambia anaenda huko kuchukua dhahabu, nilikaa dirishani kumsubiria siku nzima, nadhani kuna jambo baya limemtokea huko, tafadhali nisaidie, Alibaba! Tutafanya nini?”

“Usihofu,” alijibu Alibaba, “Nitakwenda na punda huko msituni kumtafuta. Nenda nyumbani na unisubirie, nitarudi muda sio mrefu na nakuahidi kwamba nitakuja na kaka yangu.”

Hivyo basi Alibaba alichukua punda wake watatu na kuelekea msituni. Wakati anaendelea kwenda msituni, Alibaba alikuwa akimtafuta kwenye miti miti huku akiita jina lake, lakini hakuona wala kumsikia mtu yeyote. “simpati Kassim, wala punda wake kumi pia siwaoni” Alibaba alijisemea. “Kassim aliweza kujua lile pango lilipo? Je aliweza kupata dhahabu? Mh! Huenda mkewe akawa yuko sahihi labda mumewe kuna jambo baya limemtokea.”

Alibaba alipokaribia pangoni, aliona michirizi ya damu ardhini. “hii ni ishara mbaya!” alifikiria. Kisha akasema, “nitaenda pangoni nikaangalie kama Kassim yupo mle ndani”. Aliwaacha punda wake watatu chini ya mti kisha akasogea mpaka karibu na lango la pangoni kisha akasema lile neno la siri, “Fungukaaaa sesmiiiii!!!

Lango lilipokuwa likifunguka taratibu, Alibaba aliona kitu chenye kushtua sana. Aliona mwili wa mtu ukining’inia juu ya pango, alipokaribia kuutazama kwa karibu zaidi akaona kuwa ni kaka yake, Kassim. Alibaba alianguka chini kwa magoti na kuanza kulia. “Masikini Kassim!!” alisema! “alikuwa ni mwenye tamaa, lakini ni kaka yangu. Ona sasa kundi la wezi limemuua kwasababu ya tamaa!!”

Alienda ndani ya pango zaidi na kupata dhahabu zilizofungwa na nguo kubwa nyeupe. Alizitoa dhahabu zile na kuchukua ile nguo kubwa kisha akaufunga mwili wa kaka yake latika nguo ile, kisha akaubeba mwili wa kaka yake mpaka kwenye punda mmoja kati ya wale watatu aliokuja nao. Kisha akaufunika mwili ule na baadhi ya kuni ili usionekane na watu njiani. Alibaba hakutaka watu wajue kuhusu hazina zile ndani ya pamoja na wezi 40. Kisha akarudi ndani ya pango.

“Nitachukua kiasi kidogo cha dhahabu zaidi,” alisema Alibaba, “kiasi cha kujaza makapu manne niliyokuja nayo na wale punda wangu.”

Alijaza dhahabu kwa punda wawili kisha akazifunika na kuni kisha akasema neno la siri la kufungia pango, “Fungaaaaa sesmiii!!!” na kisha akaondoka.

Alipofika nyumbani, mkewe Alibaba alikuwa akimsubiria. “Kaka yangu amekufa,” Alisema Alibaba. “Nataka niupeleke mwili wake kwa mkewe sasa hivi.”

“Oooh masikiti Kassim, kimetokea nini huko?” Alisema mke wa Alibaba. “aliweza kwenda pangoni na kuchukua dhahabu?”

“Alikwenda pangoni,” alisema Alibaba. “lakini aliuliwa. Nafikiri wezi waliwahi kurudi na kumkamata. Walimuua kwasababu alitaka kuiba mali zao.”

“Oooh masikini,” alisema mke wa Alibaba. “lakini alitaka dhahabu kidogo tu, na hiyo imemgharimu maisha yake.”

“Usimwambie mtu yeyote kuhusu hili,” alisema Alibaba. “Sasa wacha mimi niupeleke mwili wa Kassim kwa mkewe, lakini, wakati mimi nimeondoka, chukua hizi dhahabu nilizokuja nazo na uzifukie pamoja na zile zingine.”

Mke wa Alibaba akachukua dhahabu na jembe tayari kwa kwenda kuzifukia, na huku alibaba alimchukua yule punda alioubeba mwili wa kaka yake na kwenda kwa mkewe.
 
SEHEMU YA SITA

MAZISHI YA KASSIM


Kutoka sehemu ya tano:

Alibaba aliamua kwenda msituni ili kumtafuta kaka yake, lakini kwa bahati mbaya akakuta kaka yake alishauliwa na wezi wale 40 na maiti ya kaka yake huyo kuning’inizwa juu ya pango ndani. Kwa huzuni kubwa sana Alibaba aliichukua maiti ile pamoja na dhahabu kidogo kutoka pangoni na kuifikisha nyumbani kwakwe kwanza kabla ya kuipeleka kwa mke wa marehemu kaka yake. Baada ya kufika nyumbani Alibaba akaampa mkewe dhahabu zile afukie wakati yeye anaipeleka maiti ya kaka yake kwa mkewe.

ENDELEA SEHEMU YA SITA


Alibaba alipofika mlangoni kwa nyumba ya Kassim akagonga mlango, mfanyakazi wa Kassim aitwae Marjane akaja kumfungulia. Alibaba alimtazama Marjane kwa hali ya kuwa na matumaini fulani kwasababu alikuwa ni msichana muaminifu sana na alimuamini sana.

Marjane alipouona mwili wa bosi wake, ghafla akanyanyua mikono mpaka mdomoni na akatumbua macho kwa mshtuko na hofu.

“Kassim alikwenda msituni kwenda kuchukua dhahabu” alisema Alibaba kumwambia Marjane, “na dhahabu zile ni za wezi ambao walimfuma Kassim pangoni na kumuua.”

“ila nina wazo” aliendelea kusema Alibaba, “nitauficha mwili huu kwenye ghala chini, halafu tutasingizia kwamba Kassim anaumwa na ameamua kupumzika chumbani kwake. Halafu baada ya siku tatu tutasema kwamba Kassim amefariki kutokana na ugonjwa. Sasa nenda ukamwambie bosi wako (mke wa Kassim) kuhusu habari hizi mbaya. Ila usimwambie mtu yeyote mwingine kuhusu jambo hili.”

Alibaba akauficha mwili wa Kassim katika ghala kisha akarudi kwenye kijumba chake kidogo.

“Sasa Kassim ameshafariki” Alibaba alimwambia mkewe, “mke wa kassim hatataka kuishi peke yake. Nafikiri bora tuhame hapa twende tukaishi kwake na tuondoke na dhahabu zetu zote. Pia, nyumba ya Kassim ni kubwa kuliko hii yetu. Na Marjane mfanyakazi wake atatusaidia kazi sote pamoja na tutamlipa dhahabu kidogo.”

Hivyo basi, ilipofika jioni, Alibaba, mkewe na mtoto wao aitwae Khalid walihama na vitu vyao vyote mpaka kwenye nyumba ya Kassim. Ilipofika usiku, Alibaba akarudi kule nyumbani kwake kwa zamani na kufukua zile dhahabu kisha kwa siri akazipeleka kwenye makazi yao mapya.

Asubuhi ya siku iliyofuata, Marjane msichana wa kazi akaenda kwenye duka la dawa. Duka lilikuwa limejaa watu wengi wa mjini pale. Marjane kwa makusudi akaongea kwa nguvu ili kuhakikisha kila aliye pale anasikia.

“Nahitaji msaada wako!!” alisema Marjane kwa kulia, “anaumwa sana!!! Naomba nipatie vidonge ili nikampatie aweze kupata nafuu!”

Muuza duka alikuwa akitengeneza dawa, kamuangalia Marjane. “Nani anaumwa - Na nini kinamsumbua zaidi?” Aliuliza muuza dawa.

“Ni bosi wangu, Kassim. Anaumwa sana,” Marjane alijibu huku akitokwa na machozi. “hawezi kula wala kuongea na anapata maumivu makali sana. Unaweza kunipatia vidonge tafadhali?”

Muuza duka akachukua chupa ndogo iliyokuwa na vidonge vyeupe kisha akampatia Marjane. “ hizi zitampa nafuu, mpe vidonge viwili kila baada ya saa mbili.”

“Ahsante sana!” alisema Marjane. Kisha akaenda nyumbani na kusubiri.

Kesho yake asubuhi, alirudi kwa muuza dawa tena. Kwa mara nyingine tena akaongea kwa nguvu ili kila aliye pale dukani asikie anachokisema.

“Bosi wangu Kassim hajapata nafuu hata kidogo!” alisema Marjane kumwambia muuza dawa. “badala yake sasa hali inazidi kuwa mbaya, unaweza kunipatia dawa nyingine ili aweze kupata nafuu?”

Muuza dawa alitikisa kichwa kwa kusikitikia hali ya Kassim. “Pole sana, kwa kusikia hali ya Kassim kuwa mbaya kiasi hicho” alisema huku akichukua chupa ya dawa na kumpa Marjane. “Mpe hii anywe vijiko viwili itamfanya apate usingizi na maumivu yatapungua.”

“Ahsante sana” alijibu Marjane na kuondoka kwenda nyumbani.

Jioni ya siku inayofuata, jua lilipokuwa linazama, baadhi ya watu walikuwa wakipita katika nyumba ya Kassim, wakasikia kilio kikali sana. Alikuwa ni mke wa Kassim.

“Kassim amefarikiii!!!” alilia mke wa Kassim. “Masikini mume wanguuuu!! Umefarikiii!! Nitafanya nini mimiiiii!!!

Marjane akaenda kwa fundi wa nguo aitwaye Mustafa. “Mustafa!” Marjane alisema huku akimuwekea sarafu ya dhahabu mkononi kwake. “Nimesikia watu wakisema kuwa wewe ni fundi nguo mzuri sana hapa mjini. Nina kazi ngumu sana nataka kukupa. Kumetokea ajali na kuna mtu amefariki kwa ajali hiyo, hivyo basi, nataka umtengenezee suti nzuuuri sana ili tuweze kumzika vizuri. Tutakulipa vizuri sana ila usimwambie mtu yeyote kuhusu hili. Mtu huyo ameuliwa kwa kukatwa na mapanga hivyo hakikisha hakuna mtu atakayeweza kuona alama yeyote ile.”

Mustafa akaangalia ile dhahabu aliyowekewa mkononi. “Nitaifanya usiwe na wasiwasi” alisema. “Lakini nitahitaji dhahabu nyingine zaidi ili niweze kuifanya hii kuwa ni siri.”

“Utapata zaidi dhahabu, usijali” alijibu Marjane. “Lakini lazima uifanye kuwa ni siri. Sitakwambia kuwa mtu mwenyewe ni nani na anaishi wapi. Nitakapokupeleka kwake lazima uvae kitambaa machoni ili usiweze kujua ni wapi.”

“Vizuri sana!” alijibu Mustafa fundi nguo. “Nitafanya kama ulivyosema.”

“Sawa basi, chukua sindano yako na uzi” Marjane alimwambia. “kisha twende huko pamoja sasa.”

Marjane akachukua kilemba change na kumfunga fundi vizuri machoni kuzunguka kichwa chake. “Unaweza kuona chochote?” alimuuliza.

“Sioni chochote” fundi alimjibu.

“Vizuri!! Sasa twende nyumbani sasa hivi” alimwambia.

Marjane alimuongoza Mustafa mpaka nyumbani kwa Kassim na kumpeleka hadi kwenye ghala ambapo ulihifadhiwa mwili wa Kassim. Kisha akamfungua kile kitambaa machoni na kuuona ule mwili.

“Unataka nimtengenezee huyu suti!!? Ni kazi ngumu sana.” Alisema Mustafa. “Nahitaji dhahabu nyingine zaidi!”

“Utapata,” alijibu Marjane na kuweka sarafu mbili nyingine za dhahabu kwenye mkono wa Mustafa. “Lakini unatakiwa uanze kushona sasa hivi kwasababu tunataka kumzika huyu usiku huu huu.”

Mustafa akachukua sindano na uzi wake na kuanza kushona.

Mustafa alishona kwa muda mrefu sana huku Marjane akimsubiri kwa wasiwasi. Mustafa alipomaliza kushona suti nzuri ya hariri alifungasha vifaa vyake kisha Marjane akamfunga tena machoni kile kitambaa na kumuongoza tena kurudi hadi nyumbani kwake.

Walipofika, Marjane akamfungua kile kitambaa na kukiweka begani kwake. “Sasa unaweza kuendelea na kazi zako zingine.” Alisema Marjane kumwambia Fundi Mustafa, “sahau kila kilichotokea siku ya leo.”

Wakati Marjane akiondoka alipofika mbali kidogo akasimama nyuma ya kibanda cha muuza mafuta na kumuangalia Mustafa. Alitaka kuhakikisha kwamba Mustafa hamuangalii na kumfuatilia kule anapoenda, lakini Mustafa aliendelea tu na kazi yake ya kushona.

Kisha Marjane akarudi nyumbani kwa Kassim ambapo Alibaba na mkewe na mke wa Kassim walikuwa wakimsubiria.

“Tunaweza kumzika sasa” Marjane alisema.

Alibaba na wake wawili wakaanza kumvisha nguo Kassim na kumpeleka mpaka makaburini. Imamu akasoma dua za kumuombea Kassim na wanawake watatu wale wakaanza kulia kwa huzuni. Alibaba aliangalia chini ardhini na kufuta machozi yaliyokuwa yakimtoka kwa huzuni ya kumpoteza kaka yake.

Baada ya mazishi, mke wa Alibaba akasema, “tunaishi katika nyumba ya Kassim, lakini tutafanya nini kuhusu lile duka lake? Nani atakuwa akiliangalia?”

Alibaba akafikiri kwa muda kidogo. “Nitampatia duka hilo mtoto wetu Khalid,” alisema.
 
SEHEMU YA SABA

DHAHABU ZAIDI KWA MUSTAFA



Kutoka sehemu ya sita:

Kwa siri kabisa, Alibaba na familia yake pamoja na mke wa Kassim na mfanya kazi wao Marjane walijitahidi kufanya siri kubwa sana juu ya kifo cha Kassim. Walifanya kila aina ya utaratibu wa mazishi na kuweza kufanikiwa kumzika Kassim.

ENDELEA SEHEMU YA SABA


Kule msituni nako, wale wezi 40 walikuwa wakiendelea kupeleka dhahabu zao kwenye pango kama ilivyo kawaida yao, siku hiyo walikuwa katika hali ya furaha. “Hebu tukifika tuangalieni kama dhahabu zetu zote zipo!” alisema yule kiongozi wao, “hakuna mtu atakayethubutu kutuibia tena. Ile maiti tulioining’iniza mtu yeyote atakayeingia na kuiona ataogopa sana na ndio itakuwa fundisho!”

Wale wezi walicheka kwa furaha huku wakiwa njiani na farasi wao wakielekea pangoni. Walipofika kwenye lango la pango lile la ajabu wakashuka kwenye farasi wao wote na kusimama mbele ya lile lango la mwamba. “Fungukaaaaa sesmiiii!!!” alisema yule kiongozi wao. Lango likafunguka, na yule kiongozi wao akaingia ndani kidogo huku akitazama kona zote za lile pango.

“Umepotea!!!, mwili umepoteaaa!!!” alisema kiongozi wao huku akipiga mguu chini kwa hasira, kisha akawageukia wale wezi wenzake na kuwatazama. “Niliwaambieni tu!! Hapa kuna mwizi mwengine!!” alisema kwa hasira, “tumemuua mmoja, lakini mwenzake aliporudi alikuja kuuchukua mwili wa mwenzie”.

Yule kiongozi wao alipoendelea kuangalia pangoni, akaona kitu ambacho ndio kilizidi kumpatia hasira, aliona dhahabu nyingi zimepotea zaidi ya mara ya kwanza.

“Lazima tutafute na tumjue huyu mtu mwingine ni nani na tujue anaishi wapi” alisema huku wakiingia ndani ya pango, “na tukimpata lazima na yeye tumuue”

“Lakini tutamjuaje huyu mtu?” mmoja wa wale wezi aliuliza.

“kwa sababu ameichukua maiti ya mwenzie, lazima mmoja wetu aende mjini” alisema kiongozi wao, “akifika mjini ajaribu kusikiliza fununu za watu wakiongelea habari ya msiba au kupotea kwa mtu. Tukishajua mahala ambapo pana msiba au mahali ambapo huyo mtu ametangazwa kupotea, itakua rahisi kumpata huyo mwingine”

“Nitakwenda!” mmoja wao alisema, “nitatafuta mpaka nimjue huyo mtu ni nani na mahali anapoishi.”

“Una akili sana! Na ni mjanja” alijibu kiongozi wao, “hii ni kazi muhimu sana!”

“Nina uhakika nitampata huyo mtu!” alisema yule mwizi.

“Hivyo jitahidi uende!” alisema kiongozi wao. “lakini lazima ubadilishe sura yako kwa kuziba na nguo mdomoni na pia vaa kanzu ndevu kisha ujifanye wewe ni msafiri tu. Waambie watu kwamba wewe ni mgeni hapo mjini. Chukua dhahabu kidogo kwaajili ya kuwashawishi watu wakupe taarifa unayotaka, ongea nao vizuri na uskilize kwa makini sana wanachokisema.”

Baada ya kusema hayo wakatoka nje ya pango kisha yule kiongozi akasema neno la siri “fungaaaa sesmiii!!”. Kisha lile lango likajifunga kwa nguvu.

Siku iliyofuata, yule mwizi akavaa kama alivyoagizwa. Alivaa kanzu ndefu na koti kubwa lenye kofia kama jaketi la mvua. Akaanza safari ya mjini mpaka sokoni, akaongea na wafanyabiashara mbalimbali hapo sokoni. Akapata taarifa nzuri tu kuhusu mauzo ya kamba, nyama, kuku na vinginevyo pale sokoni, kisha akenda kwenye mgahawa nakuulizia bei ya mkate, kisha akaenda kwenye bustani mbalimbali za pale mjini. Alizungumza na matajiri na pia alizungumza na masikini, alizungumza na mamia ya watu pale mjini lakini hakuweza kupata taarifa yoyote pale mjini. Hakuna mtu yeyote aliyezungumza kuhusu mauaji, wala hakuna yeyote aliyezungumza kuhusu hazina za pangoni.

“Nimezungumza na mamia ya watu lakini hakuna hata mmoja aliyenipa taarifa ya kile ninachokitafuta.” Yule mwizi alijisemea mwenyewe. “hakuna hata mtu aliyezunguzia juu ya mtu aliyekufa. Bora tu nirudi kwa kiongozi wangu nimwambie kwamba nimeshindwa. Lakini atakuwa na hasira sana.”

Yule mwizi alizunguka mchana kutwa mpaka akachoka. Akaamua kukaa chini karibu na kibanda cha fundi nguo na kuangalia viatu vyake na akaona vimetoboka chini kwa shida ya safari ya mchana kutwa.

Alivivua viatu vile. Kulikuwa na mzee mmoja ndani ya kibanda kile cha fundi nguo, yule mwizi akavipeleka kule ndani.

“Angalia matundu haya kwenye viatu vyangu” mwizi alimwambia yule mzee huku akimuonesha. “Sasa hivi jua litazama, lakini naona kama macho yako hayaoni vizuri mzee, hivi unaona kweli?”

“Ooh!ndio naona matundu haya” alisema Mustafa (fundi nguo). “Macho yangu mazuri tu, mimi ndio fundi nguo maarufu hapa mjini, naona vizuri kiasi cha kuweza kuweka uzi kwenye sindano na kushona. Hakuna mtu hapa mjini anayeweza kushona vizuri kunishinda.” Aliendelea kusema. “Na ukizingatia siku chache zilizopita nilikuwa na kazi ngumu sana, nilishona suti ya maiti mmoja katika ghala lenye giza. Ilikuwa ni msichana mmoja wa kazi alikuja na kunipeleka nyumbani kwao kwaajili ya kazi hiyo. Hivyo alinichukua mpaka kwake.”

“Maiti!!?” yule mwizi alisema kwa mshangao fulani.
 
SEHEMU YA NANE

Kutoka sehemu ya saba:

Baada ya yule mwizi kuhangaika mchana kutwa na hatimaye kupumzika katika kijiduka cha fundi mshona nguo, katika kujisifu utaalamu wake, fundi anajikuta anatoboa siri na kumfanya yule mwizi kuwa makini sana kutaka kujua habari hii.

ENDELEA SEHEMU YA NANE


Yule mwizi akamsogelea fundi kwa karibu zaidi na kutaka kujizuia na ule mshangao aliouonesha aliposikia kuhusu maiti. “Tafadhali hebu niambie huyo maiti alikufa vipi?” mwizi alimuuliza fundi.

“siwezi kukwambia zaidi kuhusu maiti huyo” fundi alijibu. “Ni siri na nimemuahidi msichana wa watu kuwa nitaitunza siri hii.”

Mwizi akachukua sarafu moja ya dhahabu kutoka katika lile vazi lake refu na kumuonesha fundi nguo. “Unaitwa nani mzee wangu?” Mwizi aliuliza. “Mustafa” fundi nguo akajibu.

“Vizuri, Mustafa, sitaki kujua jina la aliyefariki” mwizi alisema huku akitabasamu, “sitaki kujua kitu chochote kuhusu yeye, wewe nipeleke tu nyumbani kwake na nitakulipa vizuri sana.”

Mustafa alifikiri kwa muda mfupi kidogo. Kisha akachukua ile sarafu ya dhahabu.

“Nitajaribu” Mustafa alisema, “lakini yule msichana alinichukua hali ya kuwa amenifunga macho na kitambaa hivyo sitaweza kupajua.”

“Twende sasa hivi,” alisema mwizi. “Utajifunga macho na kitambaa vilevile kama ulivyofanya mwanzo. Vilevile utalazimika kurudi nyumbani katika hali hiyohiyo ili usipajue nyumbani hapo ukaonekana ni mvunjaji wa ahadi. Hata kama utakua huoni wakati tunaenda lakini utatumia harufu za maua na sauti za wanyama kuweza kutambua njia. Jitahidi sana na nitakulipa vizuri sana.”

Alipomaliza kusema hayo akachukua sarafu nyingine ya dhahabu na kumuongezea Mustafa. “Nitajaribu,” alisema Mustafa huku akitabasamu.

Mustafa akamalizia kushona viatu vya mwizi huyo kisha akafunga kibanda chake. Mwizi akachkua kitambaa kirefu cha njano na kumfunga Mustafa kuzunguka kichwa ili azibe macho yake.

“Sawa kabisa!, sasa jifanye kama ulivyofanya mwanzo” alisema mwizi, “Mimi niwe kama yule msichana wa kazi, sasa jaribu kutafuta sauti njiani na harufu harufu ambazo ulikuwa ukizisikia wakati unapelekwa na yule msichana mara ya kwanza.”

Waote wawili wakaanza safari. Mwizi alimshika mkono Mustafa ili aweze kumuongoza vizuri njiani.

Baada ya muda mfupi, Mustafa akasimama na kusikilizia harufu. “Nyama ya kuku!” alisema. “Kuna mtu anapika nyama ya kuku kwaajili ya chakula cha jioni. Inanukia vizuri sana, hii nyumba wanapenda sana nyama ya kuku jioni, sasa nina uhakika hii ni njia yenyewe.”

Dakika chache baadaye, Mustafa akasema, “nasikia sauti za punda maeneo fulani kushotoni kwetu, hiyo ndio njia inatakiwa tuifuate.”

Dakika chache baadaye, alisimama na kusema,”hiyo sauti ninayoisikia ni ya mtoto analia, hako katoto kila siku jioni lazima kalie tu, labda hakataki kwenda kulala mapema, nafikiri hiyo ndio njia yenyewe huko na nafikiri tunakaribia kufika mahala husika sasa.”

Waliendelea na safari kidogo tena, Mustafa akasimama na kuvuta harufu na kusema, “nakumbuka hii harufu ni ya maua mazuri sana ambayo nayapenda sana, hii harufu niliwahi kuisikia sehemu moja tu ambayo ndio ile nyumba tunayoitafuta. Nafikiri hapa ndipo mahala tunapohitaji rafiki yangu. Hii ndio nyumba yenyewe, hii ndio nyumba ambayo nilikuja kushona suti ya yule marehemu tuliyekuwa tukimzungumzia.”

Harufu ile ya maua mazuri ilikuwa ikitokea kwenye dirisha zuri la nyumba ya Kassim. Mustafa ameweza kumuongoza mwizi mpaka pale kwenye ile nyumba.

“Una uhakika kwamba hii ndio nyumba yenyewe?” mwizi aliuliza.

“Ndio kabisaaaa nina uhakika kabisa hapa ndipo penyewe.” Mustafa alijibu. “Ila tu siufahamu huu mtaa hivyo hata nyumba yenyewe siwezi kuijua ni ya nani.”

“Hiyo haijalishi. Umenielekeza vya kutosha” alisema mwizi. “umekuwa na msaada mkubwa sana kwangu. Sasa chukua hii sarafu nyingine tena ya dhahabu na nitakuongoza urudi kwenye kibanda chako cha kushonea nguo.

Mwizi akatoa kipande cha chaki kutoka mfukoni kwake na kuweka alama kwenye mlango wa nje wa nyumba ile.

“Hapa sasa nimeshamaliza kazi” alijisemea mwizi. “Nimeweka alama hii mlangoni ili iwe rahisi kwangu kuja. Kwa maana nyumba zote mtaa huu zinafanana, hivyo haitakuwa rahisi kukumbuka. Hii alama ya chaki mlangoni ndio itanikumbusha nitakapokuja kwa mara ya pili. Hapo tutaweza kuvamia na mapanga yetu na kumuua huyu mwizi wa pili wa hazina zetu kule pangoni”

Mwizi akamchukua Mustafa na kumrudisha kibandani kwake kisha akaanza safari ya kurudi msituni kuungana na wezi wenzake. “kiongozi wangu atafurahi sana kwa kazi yangu!” alijisemea huku akicheka. Alipokuwa njiani juu ya farasi wake akawa anawaza jinsi wenzake watakavyokuwa na furaha kupata habari njema ile.

Asubuhi iliyofuata, yule msichana wa kazi Marjane alianza kuandaa chai ya asubuhi kwaajili ya Alibaba na familia nzima. Alichukua birika yenye kahawa na kuandaa machungwa pamoja na sahani na vikombe. Lakini akagundua kwamba hakuna mkate jikoni.

“Itabidi tu nikanunue mkate haraka” alijisemea huku akichukua mfuko na kuelekea madukani hapo mjini. Alipokuwa akirudi, wakati anakaribia mlangoni, akaona alama nyeupe asiyoielewa, akasogea kwa karibu zaidi na kuitazama, ni alama ya chaki imechorwa mlangoni.

“Hii alama haikuwako hapa jana!” alijisemea. “Nani atakuwa ameweka alama hii hapa mlangoni? Na itakuwa ina maana gani hii alama?” Marjane alisimama pale muda kidogo huku akitafakari na kukuna kidevi chake kama mtu anayetafuta ufumbuzi wa jambo fulani.

“Simjui nani aliyeweka hii alama hapa.” Alisema. “sijui pia aliyeweka alikuwa ana maana gani- lakini nafikiri hii alama itakuwa si alama nzuri kabisa. Najua nini cha kufanya.” Akaingia ndani na kuchukua kipande cha chaki. Kisha akatoka nje na kuzunguka mtaa mzima na kuweka alama kama ile mlangoni katika kila mlango wa nyumba zote za mtaani pale.

“Hii lazima itamchanganya huyu anayetaka kufanya ubaya katika nyumba yetu.” Alijisemea huku akitabasamu. Kisha akarudi ndani kumalizia kuandaa chai. Hakumwambia yeyote kuhusu ile alama ya chaki.
 
SEHEMU YA TISA

Kutoka sehemu ya nane:

Sasa nyumba ya Kassim imeshajulikana na mwizi ambaye alikuja mjini kuitafuta, kutokana na kuwa nyumba zote za mtaa ule zilikuwa zikifanana, mwizi akaona ni njia nzuri aweke alama ya chaki kwenye mlango wa nyumba ya Kassim ili asipotee atakaporudi mara nyingine. Lakini hata hivyo, Marjane anakuja kuona alama hiyo na kuamua kuweka alama hiyohiyo katika kila mlango wa nyumba zote zilizopo katika mtaa ule.

ENDELEA SEHEMU YA TISA


Yule mwizi akarudi msituni akimpiga farasi wake ili azidishe mwendo na awahi kufika. Alipokaribia kufika tu kule msituni walipo wenzake akaanza kupiga kelele za kushangilia, “Nimeshaipata nyumba!, nimeipata nyumba!”

Kiongozi wa wale wezi akageuka kumtizama aliyekuwa akija mbio na farasi. Alipomuona ni yule mwenzao akatabasamu.

“Vizuri sana!” akasema kiongozi wao. “Sasa tunaweza kwenda kumtafuta aliytetuibia dhahabu zetu!”.

Yule mwizi akashuka kwenye farasi wake.

“Ilinichukua muda mrefu sana” alisema yule mwizi. “niliongea na mamia ya watu mjini. Nilikwenda sokoni, mpaka kwenye vibanda vya kuuzia kahawa, nilikwenda sehemu mbalimbali lakini hakuna hata mtu mmoja aliyefahamu kuhusu habari ya mtu aliyekufa. Baadaye nikaenda katika kibanda cha mzee mmoja mshona nguo.

“hapo sasa ndipo bahati yangu ilipotokea” aliendelea kuelezea. “Fundi cherehani – jina lake Mustafa – akaniambia kwamba alishona suti ya marehemu katika nyumba moja hapo mjini. Nikamuomba anipeleke hapo nyumbani, lakini akaniambia kwamba alipelekwa huko hali ya kuwa amefungwa kitambaa machoni ili asipajue. Hivyo na mimi ikabidi nimfunge hivyohivyo na kaniongoza mpaka kwenye hiyo nyumba. Aliweza kunifikisha kwenye hiyo nyumba kwa kusikiliza sauti na harufu mbalimbali. Nimeweka alama ya chaki kwenye mlango wa nje wa nyumba hiyo ili iwe ni rahisi kuijua nyumba hiyo tukirudi tena.”

Wale wezi waliposikia hivyo walijipongeza kwa kugongana mikono na miguu.

“Sasa tunaweza kumkamata yule mwizi mwengine!” kiongozi wao alisema. “Twendeni mjini tukiwa katika makundi mawili au matatu tu ili watu wasije kutushtukia. Kisha akamgeukia yule mwizi aliyeigundua nyumba ya Kassim na kumwambia “nitaenda kwenye hiyo nyumba na wewe. Kisha nitaamua nini cha kufanya. Sote tutakutana mjini.”

Hivyo basi wezi wote wakaondoka katika makundi matatu tofauti. Kiongozi wa wezi na yule mwizi wakafika kwenye mtaa ambao nyumba ile ilikuwepo. Mwizi akaonesha kwa kidole chake na kuongea kwa furaha.

“Hii hapa!” alisema mwizi. “Hii ndio nyumba yenyewe. Umeona alama ya chaki mlangoni?”

Kiongozi wa wezi akaenda mpaka karibu na mlango na kuangalia alama ya chaki. “Ndio, Naiona alama ya chaki.” Alisema. “Lakini hebu angalia - naona kuna alama nyingine tena ya chaki kwenye mlango wa nyumba nyingine- na ile nyingine pia – na ile pia!!!” akawa anatembea nyumba hadi nyumba na kuona kila nyumba mlango wa nje una alama ile ile. Hali hiyo ilimuudhi sana na kumfanya amkasirikie yule mwizi aliyewaleta huku.

“Wewe ni mpumbavu sana!!” Kiongozi alisema. “hii imekuaje sasa, kwanini kuna alama ya chaki katika milango ya kila nyumba, ni nani ameziweka?”

“Sijui Mkuu!” alijibu yule mwizi akiwa hana furaha. “Mimi niliweka lama kwenye mlango mmoja tu”

“Wewe ni mjinga sana! Umeshindwa kazi yangu.” Alifoka kiongozi. “Sasa kwa hali hii kila mlango una alama hiyo hiyo, sisi tutajuaje hiyo nyumba yenyewe. Aaaghh! Turudi tu kazi imekushinda”

Asubuhi ya siku iliyofuata, wezi wote walikuwa kwenye kikao kingine tena kule msituni.

“Mmoja wetu alishindwa kufanya kazi yangu.” Kiongozi wao aliwaambia. “Lakini ni lazima tuitafute hiyo nyumba. Nani mwingine anaweza kujaribu?”

Wote walikaa kimya Kwa muda mfupi kidogo. Kisha mwizi mwingine akajitokeza mbele. “Mimi nitakwenda,” Alisema. “Nina uhakika nitaipata hiyo nyumba. Nitaenda kuongea na yule yule fundi nguo, Mustafa”

Haraka sana yule mwizi mwingine akaelekea mjini mpaka kwa fundi Mustafa. Muda sio mrefu yulemwizi akafanikiwa kukiona kibanda cha Mustafa. Yule mwizi akampa mkono wa salamu Mustafa na kumuonesha sarafu ya dhahabu.

“Najua uliwahi kushona suti ya marehemu fulani katika nyumba moja hapa mjini.” Alisema yule mwizi. “na jana ulimpeleka rafiki yangu katika hiyo nyumba, na kaweka alama ya chaki katika mlango ili asiweze kuipoteza katika kumbukumbu yake. Lakini kwa bahati mbaya kuna mtu aligundua hiyo alama na kuweka alama kama hiyo katika kila mlango wa nyumba, hivyo tumeshindwa kuifahamu. Naomba unipeleke katika hiyo nyumba uliyoshona suti ya marehemu, lakini, mimi nitaweka alama ya chaki nyekundu kwenye fremu ya dirisha, alama hiyo itakuwa ndogo sana kiasi ambacho hakuna yeyote atakayeweza kuiona.

Mustafa akaiangalia ile sarafu ya dhahabu. “Ukinilipa vizuri, nitakupeleka.” Alisema.

“Nitakulipa vizuri.” Mwizi alimjibu. “lakini utavaa kitambaa machoni kama ulivyofanya mwanzo.”

Mwizi akachukua kitambaa chekundu na kumfunga nacho Mustafa machoni na kisha wakaanza safari.

Baada ya muda mfupi, Mustafa akasimama na kuvuta harufu. “samaki!” Mustafa alisema. “napenda sana harufu ya samaki akipikwa! Mke wangu huwa ananipikia samaki kila Jumamosi. Hapa lazima tukate kushoto.”

Dakika chache baadaye, akasema Mustafa. “Huyo mbwa anabweka! Nafikiri ana njaa na anataka chakula chake cha jioni. Tuifuate hiyo sauti kisha tutakata kulia.”

Kisha tena baadaye kidogo akasema, “Naukumbuka huu muziki, kuna mtu huwa anapenda sana kuchezea zumari na filimbi maeneo haya kama nilivyosikia mara ya kwanza. Nafikiri tunakaribia kufika.”

Mwishowe kabisa kwa mshangao, “Waridi! Oooh! Napenda sana harufu ya haya maua, na hapa nina uhakika ndipo kwenye hiyo nyumba, tumeshafika.”

Harufu ya maua hayo yalikuwa yakitoka kupitia kwenye dirisha moja la nyumba ya Kassim. Hiyo ndiyo nyumba ambayo Alibaba, mkewe, mtoto wake, mke wa Kassim pamoja na mfanyakazi wao Marjane walikuwa wakiishi.

“Ahsante sana!” alisema Yule mwizi. “umenifanyia kazi nzuri sana mzee wangu.” Kisha akampa sarafu zaidi za dhahabu.

Mwizi alitabasamu huku akienda kwenye dirisha la nyumba hiyo na kuweka alama ndogo sana ya chaki nyekundu kwenye fremu ya dirisha hilo.

“Hakuna mtu atagundua alama hii ndogo sana,” alijisemea mwizi. “Kiongozi atanifurahia sana!” Kisha akamrudisha Mustafa kwenye kibanda chake cha kushonea nguo naye akarudi kuelekea msituni.
 
Back
Top Bottom