Alichoandika George Ambangile YOUNG AFRICANS 6-0 CBE (7-0)Agg

Alichoandika George Ambangile YOUNG AFRICANS 6-0 CBE (7-0)Agg

The introvert

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2023
Posts
701
Reaction score
1,522
ANAANDIKA MCHAMBUZI,GEORGE AMBANGILE.
.
.

✍🏻Yanga wamecheza hii mechi utasema vile mechi ya mkondo wa kwanza alifungwa

1: Sharp wakiwa na mpira na bila mpira

2: Aggressive ( matumizi ya nguvu katika sehemu sahihi )

3: Kushinda mipambano yao ( win duels )

4: Recovery runs + Counter pressing : wakipoteza mpira , pale wanapotakiwa kuweka presha kwenye mpira wanafanya hivyo haraka na pale pressing yao ikishindikana wanarudi nyuma haraka sana

✍🏻Uwepo wa Yao na Boka ( na wachezaji wa pembeni kuwa namba 10 kiuhalisia ) inafanya Yanga wakiwa na mali :-

A: Nyuma wanakuwa watatu ( Job , Bacca na Mkude )

B: Pacome na Chama kwenye halfspaces zote ili kuwapisha Yao na Boka kuwa wingers juu ya uwanja

C: Hii inafanya Yanga kushambulia na takribani wachezaji 6 katika mstari wa mwisho wa ulinzi wa CBE na ndio maana pale walipokuwa wanapoteza mpira ilikuwa rahisi kwao kukabia juu huko huko.

✍🏻Nafikiri CBE walikuwa wanacheza kama vile wanajua hapo ndio walipofikia , cha kufanya ni kupambana na kupunguza idadi ya magoli , lakini haikuwa hivyo kwao :-

1: Physically walizidiwa sana
2: Wanapasiana lakini hawana runners wengi

NOTE

1: Siku zote msingi namba moja wa Yanga ni safu yao ya ulinzi ( halafu timu kiujumla bila mpira hakuna abiria uwanjani )

2: Yao na Boka : Mmoja technically yupo clean sana ( Yao ) na mwingine running power yake kubwa ( Boka )

3: Fuad yule jezi namba 10 wa CBE anajua boli

4: Chama yale ndio maeneo anayoyapenda ... anakwaza 😀🔥

5: Benchi la Yanga 🔥 : Magoli tatu toka benchi : Aziz KI volley 🔥

6: Mzize uwepo wa Dube na Baleke kauchukulia personal sana🔥

7: Mudathir .. anakula nini ? Always on the move 🔥

FT: Yanga 6-0 CBE ( 7-0 Agg )
1726948308853.jpg
 
Yanga ni timu bora sana ikicheza kitimu bila mchezaji mmoja mmoja kulazimisha kufunga. Yanga is unstoppable ikicheza kitimu.

Yanga ihakikishe kila mchezaji anafurahi kutoa assist ikibidi kuwekwe Bonus kubwa kwa kila assist itakayozaa bao. Pesa ya goli la Mama itumike kulipa kila assist japo laki 2 kwa kila assist.

Benchi la ufundi la Yanga lisisitize wachezaji kupendana na kuweka mbele maslahi ya timu. Iwahakikishie ajira watupe raha zaidi.
 
Back
Top Bottom