Alichofanya Kagere ndiyo akili ya mchezaji anayejitambua

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Dada yake Mo Dewji alikuwa amekutana na Meddie Kagere, baada ya kusalimiana dada akaanza mtania Meddie.

"Wewe unawaonea dagaa tu kambale huwawezi"

Meddie akacheka kidogo na kuuliza, "Ina maana Yanga na zile team afcon ni dagaa? Basi nitajie team unayotaka niifunge hapa TZ kwa sasa"

Ndiyo dada kusema Azam wana team nzuri na najua mechi yao na Simba itakuwa tough...wapige bao. Ukifanikiwa ntajua wewe kidume nakupa 50,000,000/="

Meddie alicheka sana akasema "angalau ungenambia Ruvu Shooting, hao Lamba Lamba ntawalamba tu, weka mpunga tayari"

Ndiyo kilichotokea. Meddie akawagonga AZAM kimoja.

Akapewa mpunga wake 50,000,000. Hapo ndipo alipoonesha ukomavu wake. Hii pesa angekuwa mtu mwingine asiyejielewa angeenda itumia peke yake.

Lakini Kagere alikumbuka kitu kimoja. Kuwa siku ya mechi hakucheza peke yake. Ule mpira alioufunga hakutoka nao nje ya uwanja akaingia nao ndani akakimbia na hatimaye kufunga. Alifikiria nje ya mawazo ya kuwa yeye ndiyo alifunga lile goal.

Kagere alikumbuka simba ndo ilishinda lile goli ambalo yeye alilimalizia. Hiyo pesa akaitoa kwa team igaiwe kwa kila mchezaji aliyekuwa ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

Kwa kitendo hicho unadhani nani atamnyima pasi Kagere? Kama anaona yupo kwenye nafasi ya kufunga kwa nini asipewe pasi ashinde maana hana ujivuni. Anatambua kuwa Simba ni team na Simba si yeye.

Anatambua kuwa ushindi wa Simba unaanzia kwa kipa uwanjani mpaka mshambualiji anatambua pia unaendelea mpaka kwa wachezaji ambao wapo nje ya uwanja kwa mechi hiyo.

Huu ndo ukomavu tunaozungumzia. Mchezaji unapaswa ufikirie kwa mapana, si kwa ubinafsi. Unapaswa usijifikirie wewe, unapaswa ufikirie team nzima. Hiyo ndiyo maana ya ukomavu wa mchezaji.
 
Hivi zile 10M Kaseja alitafuna peke yake
 
Hizi habar za kupewa milion 50.000.000.nizakweli mana co pesa ya mchezo mchezo
 
kuna mbumbumbu wanaamini hiyo pesa alipewa Kagere kweli, hahaha hiyo pesa ilikuwa ya timu nzima tena imetokana na mapato ya viingilio. Kweli MO anajua kucheza na akili za mbu mbu mbu
 
kuna mbumbumbu wanaamini hiyo pesa alipewa Kagere kweli, hahaha hiyo pesa ilikuwa ya timu nzima tena imetokana na mapato ya viingilio. Kweli MO anajua kucheza na akili za mbu mbu mbu
Endelea kujifariji unashiba kwa upepo wenzako wananawiri.
 
Simba tunaishi kitimu. We angalia hata clips sa You Tube. Ushawahi ona clips za Yanga nje ya mechi?
 
Watapata wapi?ile majuzi wamekula mihogo na chai asubuhi wakammalizia mwenzao yondani akashindwa fanya mazoezi. Wabinafsi sana hawa jamaa.


Simba tunaishi kitimu. We angalia hata clips sa You Tube. Ushawahi ona clips za Yanga nje ya mechi?
 
We bwege ulihusika kummalizia yondani chai na mihogo juzi.akashindwa kufanya mazoezi. Muwe na utu kwa wenzenu.siyo mihogo ikiwekwa chini kama mtu kachelewa alikuwa naoga ndo basi



kuna mbumbumbu wanaamini hiyo pesa alipewa Kagere kweli, hahaha hiyo pesa ilikuwa ya timu nzima tena imetokana na mapato ya viingilio. Kweli MO anajua kucheza na akili za mbu mbu mbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…