kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Gazeti la Chama Tawala limefungiwa kwa kuandika taarifa ya isiyokuwa sahihi kuhusu Mkuu wa Nchi na Amirijeshi Mkuu wetu ambayo imesababisha taharuki za kisiasa, kikanuni na kikatiba kwa taifa. Haiwezekani gazeti la Chama tawala likosee taarifa kuhusu Mwenyekiti wa chama wao na Mkuu wa taifa kwa bahati mbaya tu.
Waswahili wanasema "kunguru hana kibyongo ukimuona ana kibyongo kainama kuokota kitu", kazi yako ni kujiuliza mapema kabla hajaruka kuwa kainama anaokota nini? Kifaranga? Panzi? Msoga? au nguo yako ya ndani?
Hawamtaki kiongozi au watataki aendelee? wameandika kwa makusudi au waliteleza? waliandika wenyewe au kuna mtu/watu wako nyuma yao na ni wangapi? Dhamira (motive) ya kuandika habari ile ilikuwa ni nini?
Ni heri kukosea kwenda kugagua tena mlango uliofungwa ujue kama umefungwa kuliko kukosea kuacha kukagua tena mlango ambao haikufungwa ukidhani kuwa umefungwa.
Hii ni hatari kubwa kuliko akina Mbowe. Adui wa ndani ni mbaya sana kuliko adui wa nje.
Ushauri wangu binafsi, vunja baraza la mawaziri ulisuke upya