Nimeipenda sana hii presentation ya H.B
A-Y anabidi awe makini sana kujua atokako na aendako,juzi juzi nimesoma kwenye mitandao kuwa anakwenda Souz kufanya video ya thamani ya 10,000/- $.Kama anaweza jufanya mambo haya anashindwaje kumlipa producer/rafiki yake kwa kazi aliyomfanyia !?.
Wasanii wengi wanapotea kwa kutojua na kuthamini kazi za watu waliochangia mafanikio yao.Tulishuhudia Mr. Nice alipoanza kuporomoka pindi alipoanza malumbano na producer wake Kameta.
A-Y akumbuke soon atapotea na atamwacha H.B anasonga mbele ,uzoefu unaonesha maproducer wanashine kwa muda mrefu zaidi ya wasanii.Hivyo ni vyema akajenga urafiki zaidi ya kujenga uadui.