Alichosema Ronaldo Nazário kuhusu kauli ya CR7 ndio Mchezaji Bora wa Muda wote

Alichosema Ronaldo Nazário kuhusu kauli ya CR7 ndio Mchezaji Bora wa Muda wote

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Ronaldo Nazário (R9) has always spoken highly of Messi, calling him a ‘unique’ talent and one of the greatest ever. He admired Maradona’s magic and was deeply inspired by his legacy. When it comes to Cristiano Ronaldo, R9 respects his incredible work ethic and goal-scoring ability but has often said he sees more of himself in players like Mbappé. A true legend recognizing greatness across generations.

==============

“Watu wanakuwa wabinafsi, Cristiano Ronaldo amekuwa na historia nzuri, ni kati ya Wachezaji Bora, sikubaliani naye kuwa yeye ndio bora kwa muda wote lakini naheshimu maoni yake, kwangu bora ni Pelé, Messi na Maradona, wengine ni Zico, Romário, Cristiano Ronaldo, Van Basten, Zidane, Figo, Rivaldo, Ronaldinho…”

Ronaldo Nazário (R9)
Februari, 2025

===================

“Naamini kila Mtu anaweza kusema anachokitaka, kama anadhani yeye ni bora wa muda wote… ni sawa, kwangu mimi Mchezaji Bora wa Muda wote ni Ronaldo Nazario de Lima.”

Karim Benzema (37)
Februari 2025

Hizi ni kauli zilizitolewa na Mshambuliaji wa Al-Ittihad, Karim Benzema (37) pamoja na mstaafu Ronaldo de Lima kwa wakati tofauti kuhusu kauli ya Cristiano Ronaldo (40) anayeichezea Al-Nassr aliyoitoa mwezi uliopita (Februari 2025) akijielezea kuwa yeye ndiye Mchezaji Bora wa Muda Wote kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye mchezo wa soka
 
R9 ni takataka
- ana chuki binafsi na cr7

Hii simaanishi kuwa nakubaliana na kauli ya CR7 kuwa yeye ni GOAT. Japokuwa ana hoja.
 
R9 kipaji Bora pengine kuliko vyote kuwahi kutokea lakini kilichoangushwa na ulaji usio wa nidhamu, majivuni, na kutokujali !
But kimafanikio r7 Yuko mbali kumzidi mshikaji
 
R9 kipaji Bora pengine kuliko vyote kuwahi kutokea lakini kilichoangushwa na ulaji usio wa nidhamu, majivuni, na kutokujali !
But kimafanikio r7 Yuko mbali kumzidi mshikaji
Kuna sehemu walisema pia madawa aliyokuwa anatumia, yalikuwa yanasababisha kuongezeka uzito ndio maana R9 wa kabla na baada ya majeruhi ni watu wawili tofauti
 
Kuna sehemu walisema pia madawa aliyokuwa anatumia, yalikuwa yanasababisha kuongezeka uzito ndio maana R9 wa kabla na baada ya majeruhi ni watu wawili tofauti
Oh maskiini huyo utotoni alikimbiza vibaya..nililetewaga jezi full na sista imeadikwa Ronaldo na picha yake pia akiwa na jezi ya selecao..
Rip sista..
 
Sasa hapo kaonesha chuki gani? Kasema anaheshimu maoni ya cr7, kisha nae akatoa ya kwake.

kwa mujibu ya maelezo ya R9 ni kuwa Neymar yuo kwenye to 10 ya all time hapo ndio upimbi wake unapodhihirika
 
kwa mujibu ya maelezo ya R9 ni kuwa Neymar yuo kwenye to 10 ya all time hapo ndio upimbi wake unapodhihirika
If Neymar is available in his top 10 list of the players, it's because he's Brazilian, Nothing else.
 
CR7 huwa hamumuelewi anachomaanisha,kuna utofauti kati ya kipaji cha mpira na ule wa kuutafuta. Kiukweli CR7 hana kipaji cha mpira ila juhudi binafsi na mapenzi ya mpira vimemfanya afike hapo alipo, ndio maana anajiita GOAT haijawahi kutokea mchezaji hana kipaji,akajipambania,kwa juhudi zake binafsi,mazoezi mpaka kuwika duniani kote,tofauti na hao akina messi,ronadinho,delima,pele neymar ambao kiuhalisia wana kipaji cha mpira,wani mpira unawafuata,sio CR7 mpira anaufuata. nakubaliana na CR7 kuwa ni GOAT.
 
Wewe utakuwa wa 2000 humjui CR7 wewe!! CR7 hakuwa nakipaji ??? Siriazi?? Ww utakuwa umemjua CR7 wa Madrid ,Juve na Al- Nassir!! Yaani yakataka Kama Neymer unamlinganisha na CR7 !! Kweli aiseee jiangalie bhana
 
hujanielewa, kuna wachezaji wamezaliwa na bahati ya mpira mkuu,kama akina ronadinho,delima,pele, messi hata asipoenda mazoezini,gmy nk akiingia atakichafua vema tu,ndo hao akina messi, lakni cr7 tangu utoto wake ni mtu wa juhudi sana mazoezi gmy na uwanjani unamuona kabisa huyu anakipaji cha kutafuta yeye mwenyewe si cha kuzaliwa nacho. Chukulia mfano hapa bongo, kibu d na aziz ki, kibu d akiacha kwenda mazoezini kiwango kinaisha kwa sababu mpira anaufuata, tofauti kabisa na mwenzi KI ambaye mpira unamfuata. mimi mimeanza kufuatilia mpira 1997 mkuu, naelewa ninachokwambia.
 
R9 ni takataka
- ana chuki binafsi na cr7

Hii simaanishi kuwa nakubaliana na kauli ya CR7 kuwa yeye ni GOAT. Japokuwa ana hoja.
Kitoto cha 2000 ambacho hakijamshudia R9 akisakata kabumbu kinamuita takataka
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom