101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,057
- 2,221
Tarehe 20/06/2023 nilipigiwa simu na watu wa AliExpress Ofisi za Dar es Salaam wakanieleza kuwa mzigo wangu umeshafika Dar, niende ofisi zao za Dar mtaa wa migombani nyumba namba 8, plot namba 65 nikauchukue. Dah, nilidhani masihara, sijawahi sikia kama AliExpress wanaofisi hapa Tanzania.
Siku iliyofuata nilifunga safari hadi mtaa wa migombani maeneo ya Morroco pale nikafika na kukuta kweli kuna ofisi, nikataja namba ya mzigo wangu mhudumu akaingiza kwenye computer akaona upo store akawasiliana na mtu wa store nikapatiwa mzigo wangu bila shaka wala wasiwasi.
Tuliopo Dar es Salaam tuagize mizigo bila ya wasi wasi wa kupotea au kuibiwa kwa sasa kwa sababu mizigo haipitii posta tena, inafika moja kwa moja katika ofisi za AliExpress Dar.