Aliexpress wamefungua ofisi Dar

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,221
Tarehe 20/06/2023 nilipigiwa simu na watu wa AliExpress Ofisi za Dar es Salaam wakanieleza kuwa mzigo wangu umeshafika Dar, niende ofisi zao za Dar mtaa wa migombani nyumba namba 8, plot namba 65 nikauchukue. Dah, nilidhani masihara, sijawahi sikia kama AliExpress wanaofisi hapa Tanzania.

Siku iliyofuata nilifunga safari hadi mtaa wa migombani maeneo ya Morroco pale nikafika na kukuta kweli kuna ofisi, nikataja namba ya mzigo wangu mhudumu akaingiza kwenye computer akaona upo store akawasiliana na mtu wa store nikapatiwa mzigo wangu bila shaka wala wasiwasi.

Tuliopo Dar es Salaam tuagize mizigo bila ya wasi wasi wa kupotea au kuibiwa kwa sasa kwa sababu mizigo haipitii posta tena, inafika moja kwa moja katika ofisi za AliExpress Dar.
 
Ungepiga picha hiyo ofisi quite wakati unapokea mzigo ungekuwa ushahidi mzuri sana, ila sawa ngoja wengine wajaribu watupe feedback
 
Kama ni kweli basi nitaagiza, maana mara nyingi nilikuwa natumia kununua bidhaa, lakini Posta ilikuwa ndio kikwazo kikubwa sana.
 
Kwahiyo wa Mikoani tunafanyaje?
 
Ha ha hawajafungua ofisi dar. Ila kuna kampuni ya wakenya wamechukua kazi ya logistics kuleta mizigo Eat Africa. Wana watu wao kila mkoa. Na wana changamoto zao kubwa kwenye mizigo na mawakala wao kwakuwa hawajawa stable. Faida yao kubwa mizigo inawahi kiasi kulinganisha na posta. Almost siku 14, posta round off 21
 
Kwahiyo mimi leo nkiagiza kitu naenda kukichukua kwa hao migombani sio posta tena?
 
Kwahiyo mimi leo nkiagiza kitu naenda kukichukua kwa hao migombani sio posta tena?
Watakupigia simu wana viofisi kadhaa lakn pia kule aliexpress unaweza muelekeza muuzaji asiwatumie hao au awatumia maana wao wanaingianpia kwenye AE standard shipping so huwa ni uchaguzi wa muuzaji atume posta au kwa hao, ila unaweza muelekeza muuzaji unachotaka wewe
 

Nikiagiza mzigo wakati wa kuuchukua ofisini kwao kuna charges nalipia?
 
Naweza kuagiza mzigo kutoka India kupitia kwao nikaupata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…