DOKEZO Alihukumiwa Miaka 30 jela kwa ubakaji miezi mitano iliyopita, leo tupo naye mtaani, hili limekaaje?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wakili msomi Pascal Mayalla hii imekaaje ?
 
Alibaka kweli? Polisi na vyombo vinavyohusika na Sheria nao pia huwa wanaangalia ...hasa Kanda ya ziwa na pwani kesi nyingi za ubakaji huwa nizakubambikiwa, na hii hutokea kwa lengo la kumkomoa muhusika, .....narudia tena 80% ya kesi za ubakaji huwa ni za uongo hata polisi na mahakama waliishalifahamu hili tena ikitokea mtuhumiwa akawa ni mtu mwenye uwezo wa kiuchumi na anajua kujieleza hao hao polisi na mahakama huwa wanatengeneza mazingira mtuhumiwa atoroke au kesi itapigwa danadana mpaka anaetuhumu achoke kufuatilia kesi.
 
Kesi ikifikia kwenye rufaa,na mshitakiwa kushinda,mshtaki,hawezi kufungua kesi upya?
Hakuna kitu Kama hicho katika Mifumo ya Maamuzi ya kimahakama UNLESS kuwe sababu Maalumu sana ambazo Mahakama itaona kwamba zinafaa.
Pia inategemea na aina ya Kesi yenyewe na level husika ya Mahakama iliyoamua Kesi yenyewe.

Kwa Taratibu za Mahakama, endapo kama Mtu haridhiki na maauzi fulani ya Mahakama mtu huyo anapaswa AKATE RUFAA kwenda Mahakama ya Juu Zaidi ili Uamuzi wa Mahakama ambao tayari umetolewa na Mahakama ya chini uweze kutenguliwa, na wala siyo kurudi tena kwenda Mahakama ya chini zaidi na kuanzisha tena Kesi nyingine mpya kwa jambo lile lile dhidi ya Mtu yule yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…