Alijifanya kidume, nimemlaza lock up

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,058
Reaction score
2,195
Alijifanya kidume, anajua kupigana. Kanipiga kofi na teke la mbavu bila sababu za msingi, nikasema hunijui wewe kama na mapenzi yaishe tu. Nikaenda kumchukulia RB, polisi wamemkamata wamemlaza lock up.

Sasa hivi eti ndio akili zinamkaa sawa anajifanya kunitumia wajumbe wamuombee msamaha.
 
Haya mambo ya wapendanao huwa sitii neno sana. Unashupaza shingo kuongea kesho unawakuta watu pamoja na wanajifunika shuka Moja.

Ila huyo mwenzetu kapitiliza, hizi Karne watu hawapigani mateke, makofi na ngumi. Mkishindwana mnaagana kiroho safi Kila mtu anaendelea na mambo yake.
 
Naomba kujua hizo sababu zisizo za msingi mpaka yeye kuchukua hatua hiyo.
 
Wanajifunika shuka moja huku wakiwa wanakusema mkuu. Mapenzi Ni mchezo wa hovyo sana
 
Sasa ndio uilete hii habari kwenye jukwaa la Ajira na Tenda?
 
Huyo ni bwege, ingia huku uone, hakuna rangi utaacha ona mpaka unyooke na Police hawatakusaidia, hakuna mwanaume anapiga mwanamke hivi hivi tu bila sababu
 
Nimewahi kukaa ndani nikiwa Chuo baada ya kumtukana abiria kwenye daladala kumbe alikuwa polisi mpelelezi wale wasiovaa sare.

Jamaa aliniweka Kawe Polisi kama kunikomoa kwa siku tano. Nilioyaona kule ndani ya hizo siku tano naweza kusema hivi kama mpenzi wako muwe mmegombana hata kufikia kupigana na hali yoyote ile akifikia kukupeleka ndani nakushauri uachane nae. Mie kwa uzoefu wangu wa kule hata mtu anifanyie visa gani siwezi kumpeleka ndani nitakaa nae nitamwonya

Kule ni sawa na mtu kukupeleka Jehanamu. Sasa kama mpenzi wako au mkeo anakupeleka Jehanamu huyo hafai kabisa

Siku naoa nilimwambia mke wangu siku ukinipeleka ndani ujue ndio mwisho wa ndoa yetu na nikitoka ni bora uwe umeshatangulia kwenu mapema sana
 
Ndani ni kubaya kweli. Nilijiona mimi ni baunsa ila nikaingia nikakutana na mtu mfupi zaidi yangu na ana mwili zaidi yangu. Hata hivyo mambo mengi ya rumande yanakuzwa washkaji walikuwa peace.

Anyway, hakuna namna utampiga mwanamke kisha akakupeleka rumande halafu nikakuonea huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…