Alikiba anadai kuna baadhi ya wasanii wananunua viewz YouTube, lakini kwake anaona kama utoto tu

kifimbocheza_

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2017
Posts
1,119
Reaction score
1,095
Hitmaker wa ngoma ‘Seduce Me’, Alikiba amefunguka na kudai kuwa ni kweli kuna mchezo wa wasanii kununua views katika mtandao wa YouTube.

Kauli ya msanii huyo inakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu wimbo wake mpya ‘Mvumo wa Radi’ kupata tatizo katika mtandao wa YouTube ambapo idadi ya views ilisimama na baadaye kushuka.

Katika mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema suala hilo lipo tena sana ila kwake ni kitu ambacho hakina maana.

“Tunajua kabisa kuna hizi bisness za kuweka maroboti katika hizi YouTube, watu wanajifanya wana views wengi na nini. Hivi vitu vipo, tena vipo!, vipo sana tu!, vipo tena sana boss!,” amesema.

“Eeeh, wananunua lakini kwa mimi binafsi naona ni utoto, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu, kwanini nidanganye watu,” amesisitiza.

Katika hatua nyingine Alikiba amesema kile kilichotokea katika ngoma yake ‘Mvumo wa Radi’ halijaathiri muziki wake wala biashara yake yoyote ile.

“Haijaathiri chochote, watu wamepata walichokuwa wanataka na sio mimi nategemea pesa kutoka YouTube viwership, hapana!. Ninachotaka kwangu ni mashabiki wangu waridhike waelewe kabisa wana-deal na msanii wa aina gani,” amesema Alikiba.

Ngoma ya Alikiba, Mvumo wa Radi kwa sasa ina views zaidi Milioni 1.1 katika mtandao wa YouTube, ilitoka May11, 2018.

Source, Bongo5
 
Uyu jamaa uwaga faraa sana yaan ye keshabambwa ha ha ha
 
Lakini namba hazi danganyi labda Alikiba atoe ushahidi wa sanii kununua views...lakini hadi sasa ushahidi unaonesha wazi kuwa Alikiba ndiyo ana nununua views ndio maana you tube walishikilia account yake na kuondoa views fake...
Kwa hiyo Alikiba sio mtu sahihi wa kuongelea watu au kuwaponda wanao nunua views kama wapo....maana hata yeye ushahidi unaonesha kuwa alikuwa ana nunua....
 
Anahaha kutafuta boost tu huyoo,this time wamemstukia
Clouds waendelee kupiga tuuuuu redio si yao.
TUMEKATAA KUWA KAAA
 
Ali Kiba anamaanisha Diamond ananunua viewers. Sawa, Kiba inaelekea huyu Diamond hata kwenye show zake huwa ananunua mashabiki. Wait, hata show zenyewe ananunua pia, lakini kinachonishangaza hela anapata wapi? Anyway, anauza karanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…