AliKiba: Sijaachana na mke wangu bali nimempa ruhusa ya kurudi kwao

AliKiba: Sijaachana na mke wangu bali nimempa ruhusa ya kurudi kwao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba ,mwananchi habari,Redio Clouds,muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba ,

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba amesema hajaachana na mkewe bali amemruhusu arejee kwao Kenya kufanya kazi kama alivyomuomba.

Amesema licha ya uamuzi wake huo, siku za hivi karibuni walikuwa na mgogoro lakini wameumaliza.

Tetesi za kuvunjika kwa ndoa hiyo zilianza Julai, 2019 lakini hivi karibuni zilishika kasi zaidi.

Akizungumza jana Alhamisi Septemba 19, 2019 katika kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa na Redio Clouds, Ali Kiba amesema yanayosemwa kuhusu ndoa yake, yenye ukweli ni asilimia moja tu.

Amesema ukweli huo wa asilimia moja ni kuwa hivi sasa haishi na mkewe, ulitokea mgogoro kati yao lakini wameumaliza.

"Katika kila ndoa hakukosi mgogoro, na kwangu ndivyo ilivyotokea lakini namshukuru Mungu tuliyamaliza na sasa tupo sawa."

"Nawashauri watu wasipende kufurahia kuvunjika kwa ndoa za wenzao kwa kuwa jambo hilo Mungu ndio analiunganisha, " amesema Ali Kiba. .

Amebainisha kuwa amelazimika kutoa ufafanuzi kuhusu ndoa yake kwa kuwa ukimya wake unaweza kuleta athari katika familia yake.

"Mimi ninasafiri mara kwa mara na mke wangu huwa anabaki mwenyewe. Mara ya mwisho nilikuwa naenda Ulaya, hakufurahishwa na akaniuliza ninaonaje akarudi kazini kwa kuwa amesoma na ana vyeti vyake."

" Nikaona isiwe tabu nimruhusu kwani anachoongea kina ukweli. Sasa atakaa tu bila kufanya kazi hadi lini, hivi ninavyoongea yupo kwao Mombasa lakini bado tunawasiliana vizuri tu," amesema msanii huyo.

Ameongeza, "Hata leo (jana) nimeongea naye na sijawahi kumpa talaka licha ya changamoto zilizotokea hapo katikati."
 
Mungu ni mwema sana kama hawajaachana. Kiba aache kupambana na social media.
 
Ushauri kwa AliKiba

Kama ni kweli mkeo alikuwa ana malalamiko kuhusu kuwepo kwa ndugu hapo kwako basi alikuwa sahihi sana

Unapokuwa na uwezo ni bora uwapangishie au kuwajengea ndugu zako kuliko kuishi nao kwenye nyumba unayoishi na mkeo. Ndoa ni ya wawili na inapaswa muishi wawili kujenga familia yenu kwa uhuru wa kimahaba, kihisia, kimichezo nk. Mtu huwezi kuwa huru na ndoa yako kama unaishi na ukoo wako wote kwako na hata maendeleo hayawezi kupatikana kama mlivyotarajia kwa kuwa kuna watu watakuwa wanaingilia ndoa yenu aidha kwa ushauri, mwongozo na vitu vingine.

Vitabu vya dini vinasema mwanaume na mwanamke wataacha wazazi wao na wao wataambatana kama mwili mmoja. Sasa wewe beba ukoo wako wote kwako uone kama mtabaki wamoja katika ndoa yenu.
 
wewe ndio unampa ushauri alikiba?

kwa TAARIFA yako jamaa ushauri anao sema hapendi tu kujionyesha
 
wewe ndio unampa ushauri alikiba?

kwa TAARIFA yako jamaa ushauri anao sema hapendi tu kujionyesha
Nimemshauri kama kijana mdogo ambaye ni mpya katika ndoa. Sio kila unaloshauriwa lazima ulifuate ana haki ya kulichukua au kuliacha. Halafu na wewe unashangaa nini mtu kutoa ushauri kwenye platform hii?
 
Kwan hata kama n ww ungekubali
Kusema umewacha
 
Bravo Ali, huo ndio uanaume ndoza Zina changamoto lakini mwanaume wa kweli ni yule anayeweza kutatua changamoto hizo
 
Back
Top Bottom