mushkhan moshi
Member
- Oct 4, 2016
- 49
- 81
Msanii anaye hit kwa sasa na hit song inayo kwenda kwa jina la seduce me Alikiba amezungumza kwa mara ya kwanza na kufunguka mengi
Alikiba amesema kila mtu anajua ubaya ambao unafanyika juu yake na ndio maana kwa kutambua hilo mashabiki wake wameweza kumuelewa na kum sapoti
Aidha alikiba amesema kuwa hujuma ambazo amefanyiwa na wenzake kutaka kuzima muziki wake wamekurupuka kwa kuwa yeye anafanya mziki mzuri na hashindani nao kwa kuwa wakushindana nao hawapo
Alikiba amesema kuwa licha ya kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutoelewana na mwanaharakati mange kimambi kwa kuwa alikiba ni kada wa ccm huku mange kimambi ni maji na moto kwa ccm .Alikiba amesema kuwa mange kimambi kwa sasa wanaelewana na shabiki yake mkubwa sana
Kwa muda wa weekend nzima mwanaharakati mange kimambi ameacha shughuli zake za kisiasa na kuamua kum sapoti alikiba kwa kupost clip mbali mbali za mashabiki wa Alikiba wakionesha ujuzi wao wa kucheza.
Kupitia hatua hiyo nyimbo ya alikiba imefanikiwa kutawala mitandaoni na kuvunja record ya kuwa na views wengi kwa muda mchache kuwahi kutokea bongo
Sent using Jamii Forums mobile app