Alikotoka Prof. Lipumba na CUF 1995-2017

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
FIPy97Gw23sXVR9N53qCLTZYqe0cDit-N048teRwS-E_-lMZME59LOgr_44qaVuDXIEY0MGLlknMHsfDyc91FGudEVeqhZ_FLnmptx5A4Ty96lAxQ6CYLZQqSIxzfb1YEPgj5C5nB5djuaTMvniwd5KLIXMWaAvRvybRvtUpiJeU1lLKTrG7ibiUNAAqT_FLXpDx6CY9EGsqIwOXPLqNSerBmqueWinU0egmaVsysnj45epVMMfP7e9j-Xk9EiH2LUIwL4fMiqmacR5XrYpV7HyR_vFy9Pm36l3X_ztUfUOa6YA-XqDy0d632GRbbODqNNL0oK5swhVWnTydE7oJG7K4RMgGgB6XzHI1l0qw6uO_cOS41VtWRY-WkdZ8ExeS-fbF03jM1IMKPVWgdlN4vLKzsfNLpxBYEU_0qvUBQGpSZ8apWCp2UuXv0jYUr132iN5O5RLU8UYmsGo-Z_7SzTGiihxhxEMwCxCT85FCwMUqJHEX0hZDaQTbtoKrALzBpLVWVK01tEIALSBY4f-4eqnNNgN-5omDzRfnxe5Pxa3dVB264-D_MT8tdAZwBA4-O2VPcVkJRAfDeBt7dwDl_ZBCJVk8JqQhLnNsPzcJEAvQwinHWg46Bg=w492-h696-no

Huo hapo juu nii ukurasa mmoja kutoka shajara yangu ya mwaka wa 1995. In Shaa Allah tutarejea katika niliyoandika katika ukurusa huo miaka 22 iliyopita. Kwa sasa hebu tuangalia haiba ya siasa ya Prof. Lipumba ambae ndiye niliyemuandika katika ukurusa huo.

Nasoma katika mitandao ya kijamii kuwa Prof. Lipumba amekwenda Tanga na amepigwa pande na wananchi wa Tanga kiasi kuwa msafara wake unasindikizwa na ‘’convoy,’’ kubwa ya askari wenye silaha akapita Tanga wima kuelekea Pangani kufanya mkutano wake.

Wanasema siku moja ni nyingi katika siasa.

Kuanzia mwaka wa 1995 hadi kufika leo mwaka wa 2017 miaka 22 imepita na kwa hakika ni miaka mingi kwa Prof. Lipumba kiasi ya kuwa hapa nilipo nikiangalia nyuma najihisi kama Rip Van Winkle aliyelala miaka takriban 20 na siku alipoamka akakuta kila kitu katika mji wake kimebadilika.

Naamini Prof. Lipumba na yeye hakuwa mbali na fikra hizi nilizokuwanazo mimi kuwa imekuwaje hali ya siasa ikambadilikia kiasi hiki kuwa inahitaji nguvu za ziada kumuingiza Tanga wakati alikuwa akiingia Tanga na kutoka apendavyo na kupokewa na maelfu ya wananchi.
Hakuna asiyejua kuwa alikuwa Prof. Lipumba ndiye aliyeitia nguvu CUF Tanga na Tanzania Bara kwa ujumla.

Sasa turudi katika ukurasa wangu wa shajara ambao picha yake iko hapo juu.
Ilikuwa Jumatano tarehe 18 Oktoba 1995 tuko katika harakati za Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi Tanzania.

CUF mgombea wake wa urais Tanzania Bara ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kijana msomi wa uchumi wa Princeton University Marekani.

Vipi ghafla aliingia katika siasa kipindi kile ni kisa cha kujitegemea na iko siku In Shaa Allah tutakieleza.

Siku hii ya Jumatano Oktoba 1995 katika shajara yangu niliandika maneno haya ambayo kwa wanaojua Kiingereza watayasoma hapo juu.

Leo nikiangalia nyuma nashindwa kupata jibu ni kitu gani kilichonifanya mimi niwe naandika kwa Kiingereza badala ya lugha yangu Kiswahili.

Tafsiri ya maneno hayo ni hii hapo chini:

‘’Nimeondoka na basi. Nilipanga kwenda hadi Segera na kutoea hapo nipande basi linalotoka Dar es Salaam kwenda Tanga. Lakini tulipokuwa Korogwe, nikaona, ‘’convoy,’’ yetu ya kampeni inaingia Korogwe kwa hiyo nikashuka pale. Tulifanya mkutano pale na baada ya mkutano nikaondoka na Tamim na Kassim katika Musso kuelekea Tanga. Prof. Lipumba alifanya mikutano miwili Muheza na Pangani.

Tulikusudia kutafuta mahali pa kuificha gari yetu. Tulipanga Rose Inn. CUF Tanga ina nguvu kubwa. Tulifanya mkutano mkubwa sana. Lipumba alinambia mkutano huu ulikuwa mkubwa kupita yote.

Baada ya mkutano tulialikwa kwa Mama Ummy kwa chakula nk. Sikuweza kuamini macho yangu. Ule msafara na umma wa watu waliozunguka ile nyumba wakiimba wakati sisi tukiwa ndani tukikirimiwa.

Nilipiga picha nyingi.

Mariam Shamte wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC akaja kuwahoji Juma Duni Haji na Prof. Lipumba. Jioni tulifanya mkutano na wazee kisha na wafanyabiashara.

Uwanja wa Tangamano ulifurika siku ile pomoni.

Hapakuwa na hata nafasi ya mtu kuweka baiskeli yake. Siku ile Prof. Lipumba aliungurma akawakumbusha watu wa Tanga historia yao na jinsi walivyopoteza kila kitu. Aliwauliza uko wapi mpira wa Tanga waliokuwa wakijivunia? Yuko wapi Shakila na taarab ya Tanga? Uko wapi mkonge na viwanda vilivyokuwa vikiwapa ajira watu wa Tanga?

Mkutano huu wa Tanga Uwanja wa Tangamano uliitia hofu kubwa CCM na haukupita muda Mwalimu Nyerere akafikaTanga katika juhudi ya kukinusuru chama chake na kumnusuru William Mkapa mgombea wa CCM asikose kura za Mkoa wa Tanga.

Katika mkutano aliohutubia Mwalimu Nyerere Uwanja wa Tangamano, Mwalimu alionya kumwagika kwa damu nchini endapo Watanzania watapiga kura kwa misingi ya dini zao.
Sijui kitu kipi kilimfanya Mwalimu Nyerere aseme maneno hayo.

Yeye mwenyewe mwaka wa 1955 katika uwanja huo huo wa Tangamano alihutubia umma mkubwa wa wananchi mara ya kwanza alipokuja Tanga baada ya kuundwa kwa TANU na umma mkubwa kama ule uliokuja kumsikiliza Prof. Lipumba ulijazana pale kumsikiliza.

Hakika hofu kubwa ilikuwa imewaingia CCM na waliweza kusoma nyakati katika kuta bila shida yoyote.

Prof. Lipumba alikuwa ameamsha matumaini mapya kwa jamii iliyokuwa imetengwa na kubaki nyuma toka uhuru upatikane mwaka wa 1961.

Nimekaa na kurejesha fikra zangu mwaka wa 1995 ambako kwa mara ya kwanza Prof. Lipumba aliingia Tanga na kuuteka mji na kuanzia hapo CUF ikawa na nguvu kubwa Tanga, nguvu ambayo ilifikia kileleni katika uchaguzi wa mwaka wa 2015 kwa CUF kuchukua kiti cha ubunge Tanga Mjini na kuongoza katika serikali za mtaaa.

Leo watu wa Tanga hawataki kuiona sura ya Prof. Lipumba katika mji wao. Hakika siasa ni mchezo mchafu na kadri unavyokuwa mchezaji mchafu na ndivyo mchezo wenyewe unavyozidi kunoga.
 
Burudani na hadth tosha kwa watu wenye mawazo machache kama PRO PESA Li-PUMBA
 
Prof. Lipumba anakataliwa Tanga kwa sababu ya kukubali kutumika. Ukishakubali kutumika unakuwa kama TP muda wowote watu wanajua utatupwa na anayekutumia
 
Ahsante sana Mzee wangu Mohamed Said kwa kuipa chakula fikra ya baadhi yetu kwa haya machache kuhusu Safari ya Prof Ibrahim Lipumba.Binafsi sikuwa nalifahamu hili ila kuanzia sasa nimefahamu.

Unaposema "Hakika siasa ni mchezo mchafu na kadri unavyokuwa mchezaji mchafu na ndivyo mchezo wenyewe unavyozidi kunoga".Una maana gani/ipi?.

Siyo kwamba sisi ndiyo wabaya na siyo siasa?.Nieleweshe tafwadhali.
 
Dahafrazeril,
Huo ni msemo mashuhuri na maana yake ni hiyo hiyo.
 
Miaka ile ya 1995 watu wa Tanga walimuona Lipumba kama kondoo. Lakini 2017 wamemuona sio kondoo bali ni chuwi aliejivisha ngozi ya kondoo. Tokea lini mpinzani akapewa convoy ya polisi wakienda kufanya mikutano?[emoji15] Hivi ushawahi kumuona Mbowe, Lissu, Lema au Zitto Kabwe na convoy ya polisi?[emoji15]

Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
dhambi ya usaliti inamtafuna...ila akiamua kutulia lipumba ni mtu makini sana.

Huna akili ya ku assess umakini wa Professor, usijikweze!

Kama usaliti ni dhambi inayotafuna Aliemsaliti Mzee Abood Jumbe Mwinyi angeshatafunika Mwili Mzima
 
Babu yangu alipata kuniambia "usimuamini Mnyamwezi wa pande za....... hata siku moja...."

Maana unyamwezini kuna koo zinaaminika na zingine haziaminiki hata zingekuwa za uchifu...

Tatizo Tanzania tunapeana uongozi bila kujua koo za wezi, wazandiki, wachawi, roho mbaya, hiyana, ufisadi, hila na laghai, sifa, kujipendekeza, visasi nk.

Mwalimu alipata kusema kwa mshangao.... "mkara....!!!" ina maana kuna dosari kwa wakara ambayo ilitambuliwa na wahenga kuwa kabila ile ikipewa wadhifa kuna madhara!!!

HATUJIFUNZI!!!
 
Babu yangu alipata kuniambia "usimuamini Mnyamwezi wa pande za....... hata siku moja...."

Maana unyamwezini kuna koo zinaaminika na zingine haziaminiki hata zingekuwa za uchifu

Usimuamini Baba anaekurupuka ku generalize Jambo kwa style hiyo
 
Mkuu angalia kuna tofauti ya babu na baba!!! mkuu hakusema wote "kuna koo!!" isijekuwa unatoka ukoo wa bwana yule (ilolangulu!!)
 
Back
Top Bottom