Alinishauri mwenyewe ila sasa ananitangaza vibaya kwa watu

Si huyu nitakapomshauri akawajaze watoto wa mtaani? Atakacharangwa mapanga, then ukamuuguze.

Kama upo tayari? Nitampa go ahead.
Hahahahaa.

Usimpe go ahead jamani asiumizwe bureee.

Muache awake hela.
 
Ulivyopewa ushauri uliufanyia kazi au uliuchukua na kwenda kuutekeleza? Kama uliufanyia kazi sioni sababu ya wewe kulalamuka hapa. Inajulikana boda boda ni kazi inayodharaulika haijalishi inakuingizia kipato kiasi gani.
 
Kaongea ukweli au hajaongea ukweli?
 
Kuna kitu cha tofauti umekionyesha katika kazi yako sio bure[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Achana naye, hata kama ukiacha boda boda hata acha kuongea angeavyo, nawe hutaacha kupata pesa.

Kikubwa, piga hatua tu, badala ya kuwa boda wa kawaida wewe kuwa zaidi ya hao...
 
Jifunze kupuuza itakusaidia sana hasa kwenye jambo ambalo unaona lina faida kwako
 
MJUMBE YUPO SAHIHI.
Wewe una degree ila ni bodaboda ndio ukweli huo.
Wewe piga kazi kwa ubora kuonyesha kuwa kweli umesoma. Vaa helmet, oga vizuri, nyosha nguo, nyoa vizuri, kuwa muaminifu kwa wateja, tunza siri za wateja. Hapo utaona matunda ya hiyo kazi.
Pia ongea na makampuni hasa supermarket uwe unafanya delivery ya bidhaa zao kwa wateja.
 
Mpe lift ya ya bodaboda halafu kitakachofuata kama mko dar atajikuta muhimbili inabidi akatwe mguu mmoja, ila ufanye kwa umakini kiathirike chombo na abiria tu
 
Unafaidika na hiyo shughuli au la?
 
Huyo mjumbe amekupa changamoto usimchukie kukusema, endesha boda kama sehemu ya safari kufikia unapotaka kufika.
 
Unashauriwa na mjumbe duh
 
Chapa kazi
 
Achana naye mjinga huyo wewe mradi unakamata mkwanja!!! Fanya kazi yeyote itakayokuingizia pesa.
 
Msamee na muombee. Lakini rai yangu kwako ni kuendelea kupambana pasipo kukata tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…