ALIPATA division II sasa AMEKUWA TANZANIA ONE

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
4,162
Reaction score
796
Mwanafunzi bora wa kwanza kitaifa katika matokeo yaliyorekebishwa ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2012, Said Irando kutoka Shule ya Sekondari Feza ya jijini Dar es Salaam, ameeleza kushangazwa na matokeo hayo kwa kuwa hakuyatarajia.

Mwanafunzi huyo ambaye tayari ameshaanza masomo ya Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Feza, alisema kuwa ingawa alisoma kwa bidii lakini hakudhani kama angeweza kushika nafasi ya kwanza kitaifa na kwamba anamini mafanikio yake kitaaluma yana ‘mkono wa Mungu'.


"Sikutegemea kabisa kuwa mwanafunzi bora, ingawa nilisoma kwa bidii kubwa nia yangu ilikuwa ni kutaka kufaulu tu; Ni Mungu amenisaidia," alisema Irando.

Alisema kujituma katika masomo, mazingira mazuri ya kusomea na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia ndiyo yaliyomwezesha kusoma na kufanya vizuri.




Irando ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto watatu, alisema kurekebishwa kwa matokeo ya kidato cha nne kulibadilisha alama za matokeo yake kutoka Daraja la kwanza akiwa na alama tisa hadi saba, zilizomfanya kuwa mwanafunzi bora kitaifa na mwafunzi bora wa kwanza kati ya wavulana kumi bora pia kitaifa.




Mwanafunzi huyo alibainisha kuwa pamoja na wazazi wake kuwa ni wafanyabiashara, yeye anatamani kuwa mhandisi ingawa bado hajajua atakuwa mhandisi katika tasnia gani.

"Natamani sana kuwa mhandisi hiyo ndiyo ndoto yangu ingawa bado sijajua nitakuwa mhandisi wa sekta gani," alisema Irando.




Irando alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi J.K Nyerere ambako alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu, lakini wazazi wake waliamua kumpeleka Shule ya Sekondari Feza.

Naye mwanafunzi Joshua Azza kutoka Sekondari ya Wavulana Marian ambaye ameshika nafasi ya saba kitaifa kati ya wanafunzi kumi bora baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama 11, alisema ameyapokea matokeo hayo kwa furaha akiamini atatimiza lengo lake la kuwa daktari wa upasuaji.




"Natarajia kuwa daktari wa upasuaji, kwa matokeo haya nadhani nitafanikiwa," alisema Azza ambaye wazazi wake wote ni walimu alipozungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Saidi Nchimbi kutoka Sekondari ya Feza, ambaye ameshika nafasi ya nane kati ya wanafunzi kumi bora kitaifa, alisema kuwa siku zote alikuwa akisoma kwa uwezo wake wote na kwamba alikuwa akitamani kufaulu kwenye mitihani yake yote aliyopewa.

Nchimbi amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama nane. Katika matokeo ya awali mwanafunzi huyo alikuwa na alama 11.



[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
NAFASI
[/TD]
[TD="width: 84"]
NAMBA
[/TD]
[TD="width: 156"]
JINA
[/TD]
[TD="width: 48"]
JINSI
[/TD]
[TD="width: 228"] JINA LA SHULE NA MKOA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
1
[/TD]
[TD="width: 84"] S0189-0063[/TD]
[TD="width: 156"] SAID JUMA IRANDO[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
2
[/TD]
[TD="width: 84"] S4459-0028[/TD]
[TD="width: 156"] ALEX ELIFAS[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] JUDE MOSHONO S S (ARUSHA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
3
[/TD]
[TD="width: 84"] S0189-0039[/TD]
[TD="width: 156"] JASPER GEOPHREY KAJIRU[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
4
[/TD]
[TD="width: 84"] S2549-0086[/TD]
[TD="width: 156"] MOSES J BOSCO[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] ALPHA SECONDARY S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
5
[/TD]
[TD="width: 84"] S4213-0074[/TD]
[TD="width: 156"] YOHANA L MAYENGA[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] MARIAN BOYS' S S (PWANI)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
6
[/TD]
[TD="width: 84"] S0239-0072[/TD]
[TD="width: 156"] NGUSE NGULUMBI[/TD]
[TD="width: 48"]
F
[/TD]
[TD="width: 228"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
7
[/TD]
[TD="width: 84"] S4213-0044[/TD]
[TD="width: 156"] JOSHUA Z AZZA[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] MARIAN BOYS' S S (PWANI)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
8
[/TD]
[TD="width: 84"] S0189-0062[/TD]
[TD="width: 156"] SAID ATWAYA NCHIMBI[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
9
[/TD]
[TD="width: 84"] S0867-0134[/TD]
[TD="width: 156"] LUPYANA L KINYAMAGOHA[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] PANDAHILL S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 66"]
10
[/TD]
[TD="width: 84"] S0101-0350[/TD]
[TD="width: 156"] PETER SEREKA KICHOGO[/TD]
[TD="width: 48"]
M
[/TD]
[TD="width: 228"] AZANIA S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
2. Wasichana Kumi (10) bora Kitaifa
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 422"]
[TR]
[TD="width: 65"]
NAFASI
[/TD]
[TD="width: 86"]
NAMBA
[/TD]
[TD="width: 196"]
JINA
[/TD]
[TD="width: 216"]
JINA LA SHULE NA MKOA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
1
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0072[/TD]
[TD="width: 196"] NGUSE NGULUMBI[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
2
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0078[/TD]
[TD="width: 196"] SAMMOTA CHUNGU[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
3
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0075[/TD]
[TD="width: 196"] RAHMA MKWATA[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
4
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0018[/TD]
[TD="width: 196"] DIANA MGAYA[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
5
[/TD]
[TD="width: 86"] S1060-0066[/TD]
[TD="width: 196"] REBECCA J MWAMBEGELE[/TD]
[TD="width: 216"] ST.MARY'S S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
6
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0010[/TD]
[TD="width: 196"] BELDA THOMAS[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
7
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0002[/TD]
[TD="width: 196"] AGNES NTAPARA[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
8
[/TD]
[TD="width: 86"] S0248-0045[/TD]
[TD="width: 196"] JOANGELINE J BAMWENZAKI[/TD]
[TD="width: 216"] MARIAN GIRLS S S (PWANI)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
9
[/TD]
[TD="width: 86"] S0298-0011[/TD]
[TD="width: 196"] FATMA M MOSHI[/TD]
[TD="width: 216"] FEZA GIRLS' S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
10
[/TD]
[TD="width: 86"] S0239-0045[/TD]
[TD="width: 196"] JESCA CHENGULA[/TD]
[TD="width: 216"] ST. FRANCIS GIRLS S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

  1. Wavulana Kumi (10) bora Kitaifa
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 429"]
[TR]
[TD="width: 65"]
NAFASI
[/TD]
[TD="width: 90"]
NAMBA
[/TD]
[TD="width: 202"]
JINA
[/TD]
[TD="width: 216"]
JINA LA SHULE NA MKOA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
1
[/TD]
[TD="width: 90"] S0189-0063[/TD]
[TD="width: 202"] SAID JUMA IRANDO[/TD]
[TD="width: 216"] FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
2
[/TD]
[TD="width: 90"] S4459-0028[/TD]
[TD="width: 202"] ALEX ELIFAS[/TD]
[TD="width: 216"] JUDE MOSHONO S S (ARUSHA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
3
[/TD]
[TD="width: 90"] S0189-0039[/TD]
[TD="width: 202"] JASPER GEOPHREY KAJIRU[/TD]
[TD="width: 216"] FEZA BOYS'S S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
4
[/TD]
[TD="width: 90"] S2549-0086[/TD]
[TD="width: 202"] MOSES J BOSCO[/TD]
[TD="width: 216"] ALPHA S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
5
[/TD]
[TD="width: 90"] S4213-0074[/TD]
[TD="width: 202"] YOHANA L MAYENGA[/TD]
[TD="width: 216"] MARIAN BOYS' S S (PWANI)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
6
[/TD]
[TD="width: 90"] S4213-0044[/TD]
[TD="width: 202"] JOSHUA Z AZZA[/TD]
[TD="width: 216"] MARIAN BOYS' S S (PWANI)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
7
[/TD]
[TD="width: 90"] S0189-0062[/TD]
[TD="width: 202"] SAID ATWAYA NCHIMBI[/TD]
[TD="width: 216"] FEZA BOYS' S S (DAR ES SALAAM)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
8
[/TD]
[TD="width: 90"] S0867-0134[/TD]
[TD="width: 202"] LUPYANA L KINYAMAGOHA[/TD]
[TD="width: 216"] PANDAHILL S S (MBEYA)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
9
[/TD]
[TD="width: 90"] S0101-0350[/TD]
[TD="width: 202"] PETER SEREKA KICHOGO[/TD]
[TD="width: 216"] AZANIA S S (DAR ES SALAAM)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 65"]
10
[/TD]
[TD="width: 90"] S0692-0065[/TD]
[TD="width: 202"] NORBERT S KIMARYO[/TD]
[TD="width: 216"] ROSMINI S S (TANGA)
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


source mwananchi na Necta
 
Mbona sikuona list kama hii kwenye yale matokeo ya awali? Au. Nilikuwa shimoni?
 
Kwani ktk matokeo ya awali hakukua na Tanzania One? Kama kuna watu walipata Division one ktk matokeo ya awali, inamaana wao waliwekewa matokeo ktk mfumo wa zamani? Haiwezekani mtu aliyekua na division two awe Tanzania one wakati kuna watu walikua na division one kabla. Walichofanya Necta ni kutumia grade za zamani hivyo wote walikua wamepunjwa sawa na haiwezekani tena kwa aliye chini awe juu, acha ukilaza, tumia hata akiri ya kuzaliwa tu utaona ukweli.
 
mkuu mbona title inasema alipata div 2 alafu ndani unasema alipata one ya tisa?
 
It is Contradictory.
Kwanza title ina makosa, kilichoandikwa ndani hakiendani na title.
Pia haiwezekani matokeo yarekebishwe then aliye chini ampite wa juu yake!!! Otherwise ni utata mtupu.
 
Nahisi mleta mada alimaanisha kuwa jamaa alipata div II form two!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…