Alipo "Abubakari Salumu (Sure boy)" ndipo mpira ulipo

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425

Picha: Abubakari Salumu (Sure boy)

Naam, kiungo bamia kiungo lainishi fundi huyu kutokana na kupenda kula urojo kule zenji kwa mzee kaju, basi wachezaji wenzake wakambatiza jina la "babu kaju"

Kutokana na Khalid Aucho kupata kadi mbili za njano basi ataukosa mchezo wa fainali Yanga dhidi ya Usm Alger utakaopigwa pale kwa mkapa.

Sure boy kiungo bamia mwamba kabisa huyu, naposikia jina lake napata kumbukumbu ya mechi ya Club Africane vs Yanga iliyopigwa pale Tunis na Yanga kuondoka na ushindi wa goli moja.

Mwamba sure boy alilitendea haki dimba la Kati alipiga mpira mwingi mno yaani "ulipo mpira sure boy yupo"
Aliwafanya viungo/waarabu wa Kati wa club African kutepeta maana mwamba alipiga mpira mwingi mpaka ukamwagika.

Nategemea makubwa kutoka kwakwe endapo atapata nafasi ya kuanza kwenye fainali ya tar 28/05/ kwa mkapa.

"Why not us" Yanga ni mwendo wa makombe.
 
Huyu jamaa Kuna match akikuchezea utapenda buree, anajituma sana na manpower yake SI mchezo
waarabu anaajua namna gani ya kuwajambisha.
 
Pigia mstari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…