Nilimsikiliza kwa makini sana! Nikiwa kama mtu aliyepita pita kwenye saikolojia na uchumi, Namuunga mkono. Moja ya kauli zake ni "WAZAZI WANATUMIA HELA NYINGI KUWATENGENEZEA WATOTO WAO UMASIKINI". Kwa kuweka msisitizo kwenye elimu ya vitabuni, Taifa limekuwa na wahitimu wengi wasiopata nafasi za kuajiriwa. Hali hii huwafanya wahitimu kuwa na maisha duni.
Nasikitika sana!, tena sana kwa kuwa watu wnapindisha mtizamo wa Julius. Julius anataka kuwe na shule ambazo zitatoa elimu ya sanaa kama muziki, mpira, n.k sambamba na elimu ya vitabuni. Uchumi wa dunia ya leo unategemea huduma, sio viwanda kama zamani kidogo. Mataifa mengi yanapata faida kubwa kwa kutoza kodi kwenye huduma za sanaa kama maigizo, muziki n.k.
Huu mfumo wa elimu ya kukremu haitusaidii kitu. Wote tunawwajua waimbaji, wanamichezo n.k wa hapa Tanzania wenye mafanikio makubwa kwa jitihada zao binafsi, ila kwa sasa wanatoa ajira na kuchangia pato la Taifa.
Nimewahi kupita Makongo High School. Pale Makongo kuna wanafunzi 'vilaza' kabisa, lakini kwa kuwa wanavipaji, wamepewa nafasi za kusoma, si mnawafamu Dogo Janja n.k.
Aliendelea kwa kusema, "mimi si wa kwanza kuandika, nenda kaulize Baraza la Mitihani utaambiwa", yeye anaonekana kwa kuwa ametangazwa kwenye vyombo vya habari. Pia alisema, "kama nikakaa kimya, tutakaa kimya mpaka lini?"
LET US THINK CRITICALLY, SIO KUWA WATUMWA WA VITABU.