Kwani risala ile iliandaliwa na mtu mmoja na haikuonwa na mtu yeyote wa pili katika uongozi huo wa wakusoma? Asionewe kwa kusakamwa peke yake, Rais wao na top layer wa juu lazima waliijua risala hiyo yenye laana. Kwa hiyo serikali nzima iwajibike. Labda watatoa somo hata kwa viongozi wa kitaifa wa kizazi kipya Tanzania kujua kwamba kuwajibika ni muhali kama hata anayekuwakilisha atabofoa. Mzee Ruksa alitoa mfano na dunia ikamzawadia kwa uadilifu wake, sio kaka yetu L.....sa aliyedai kajiuzuru lakini akaanza kunung'unika huko nje kuashiria hakuwa tayari kujiuzuru.