Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Sio jambo la kusema polepole kuwa Tanzania ni nchi ambayo inajitafuta. Uzi huu haulengi kuainisha sababu lakini " nchi hii ni nchi maskini ya wakulima na wafanya kazi haijawa ya matajiri "
Sasa katika pita pita zangu nashangaa kuona Watanzania huku mitandaoni wanafurahia baadhi ya nchi matajiri kusitisha misaada ya kimataifa, ambapo sisi Tanzania ni miongoni mwa nchi wanufaika.
Sina lengo la kusengenya lakini sitashangaa mtu huyo huyo anayefurahia halipi kodi, pengine hana kazi anakaa nyumbani kusubiri chochote kitakacholetwa n.k
Kama tujuavyo population ya Tanzania imekaa kitegemezi, kama tunafurahia kutopewa misaada basi kila mtu atoke afanye kazi tuongeze walipa kodi .
JAMBO LA MSINGI KATIKA MAKALA HII
Hapa tuainishe mambo ya msingi katika kukabiliana na kukatishwa kwa misaada
1. Serikali ibane matumizi
2. Wananchi wabane matumizi
3. Chochote tulichonancho kama nchi kisimamiwe na kitumike vizuri
5. Kila mtu apambane mara mbili zaidi kuinua uchumi wake
6. Saa za kufanya kazi ziongezwe katika taasisi na viwanda vya uzalishaji
7. Iundwe wizara mpya ya ubunifu wa kisayansi na ugunduzi wa fursa
8. Taasisi ambazo hazina tija sana au ulazima sana zifutwe au kuunganishwa
9. Kila mtu apambane kupunguza population tegemezi ikiwa ni pamoja na kuzingatia vilivyo uzazi wa mpango
10. Baadhi ya wanawake waache ujinga wakusema "kazi yetu sisi ni kuzaa kwa uchungu" watoke huko majumbani wakafanye kazi
11. Vyombo vinavyokabiliana na Rushwa, ufisadi, na ukaguzi viongeze utendaji maradufu
Mwisho nikipata mawazo mapya nitakuja kuwaambia