Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Mpo salama!
Moja ya kanuni ninayoitumia ni pamoja na kufundishwa na waalimu waliofaulu. Iwe kwenye taaluma, biashara, Siasa, mahusiano, Kiroho, miongoni mwa mambo mengine..
Kamwe usijifunze Kwa Watu waliofeli, mtu aliyefeli asiwe Mwalimu, role model, au mshauri wako. Kikawaida Watu waliofeli hufanikiwa katika mawazo Wakati waliofaulu hufanikiwa katika Matendo yaani Matokeo.
Aliyefaulu anajua kutokufaulu pia. Yaani anajua Pande zote Mbili Kwa sababu kufaulu kunakuja Kwa kufeli au kushindwa mara nyingi.
Wakati aliyefeli anajua kufeli tuu. Hajui kufaulu kukoje. Ameshindwa.
Kabla ya Nuru kulikuwa na Giza. Aliyenuruni hujua yaliyogizani. Lakini aliyegizani hajui yaliyonuruni. Kwa sababu Nuru hufukuza Giza.
Tajiri anaweza kukuambia kuhusu Umaskini Kwa sababu anaujua vizuri kuliko Maskini Mwenyewe. Tajiri anauwezo wa kukueleza utajiri Kwa sababu anauishi. Lakini Maskini hawezi kukueleza utajiri ambao hajawahi kuumiliki, wala hawezi kuuelezea umaskini Kwa namna itakayokufanya uukimbie.
Shuleni waalimu ili wawe waalimu ni lazima wawe walifaulu. Huwezi kuwa Mwalimu bila kuwa umefaulu.
Ikiwa hukufaulu basi utaitwa Mwalimu wa Uongo Kwa sababu unafundisha mambo usiyoyaelewa wala kuyajua.
Wengi husikiliza na kuwafanya Watu walioshindwa kuwa waalimu au washauri wao. Ndio maana hupoteza kujiamini.
Elewa kuwa kushindwa kwako kutategemea uwezo wako Kwa asilimia 50% lakini uwezo wa waalimu wako 50%. Yaani Huko unakojifunzia.
Kabla mtu hujamshauri kuhusu Jambo Fulani jaribu kujiuliza Jambo unalomshauri wewe mwenyewe umelifaulu?
Na Kabla hujaomba ushauri Kwa MTU, jaribu kujiuliza unayemuomba ushauri amefaulu katika Jambo Hilo?
Wanasema huwezi chuma embe kwenye mchungwa. Huwezi chuma ushindi Kwa mtu aliyeshindwa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam