Babumawe
JF-Expert Member
- Sep 12, 2014
- 2,556
- 2,571
Jamani eeeh kwanza habarini za muda huu
kiukweli tangu nianze kuujua na kuula wali aise hakuna kitu nakikubali kama ukoko, Narudia tena kwa msisitizo hakuna kitu nakikubali kama ukoko sijajua kama nina tatizo au na sitaki kujua.
Yaani tangu nipo mdogo ilikuwa kitu cha mchele kikikaribia kuiva najisogeza jikoni navizia kwanza kile kiukoko cha juujuu kile yani kile ndo kinakuwa introduction nakigonga kile halafu narudi zangu kwenye makochi nasikilizia koko lenyewe lile la chini yaani lile funga kazi. Yani hapo nitazuga zuga nangalia TV ili niwe wamwisho ili nilie kwenye sufuria ili nifanye mchakato wa ukoko.
Halafu ukoko haunaga muda maalumu , mda wowote tu unaweza ukagonga fresh. Usiombe asubuhi sasa uamke na kiporo cha ukoko halafu unafanya kama kukinyunyizia maharage hivi pembeni chai ya rangi tena ukipata chai iliyopikwa na mchaichai yani hapo unaweza ukawa unakula huku unatoa machozi ya furaha.
Sasa jaribuni hii, wali uwe wa nazi halafu chukua ukoko wa juu changanya na koko la chini kisha nyunyuzia chuzi la maharage la nazi halafu njoo na majibu hapa.