Wanachama 2370 waliokua ACT Wazalendo wakiongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kiwani kwa miaka 20, Hija Hassan Hija, wamekabidhi kadi za ACT na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akiweka bayana kuwa aligombea makamu uenyekiti kwenye chama chake cha awali kumpinga Ismail Jussa ambapo amedai kuwa Jussa alimuahidi kuwa atakoma na hatokuwa mwenyekiti
Hayo yamejiri leo, Februari 15, 2025, Visiwani Pemba, wakati wa mkutano wa kumpokea na kumtambulisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye ni mgombea pekee wa nafasi ya urais wa Zanzibar 2025 kupitia tiketi ya CCM.