Aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka amejinyonga akiwa mahabusu

Aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka amejinyonga akiwa mahabusu

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Fundi magari na Mkazi wa Kiluvya, Kisarawe, Seleman Mirai Kibiki (49), amejinyonga akiwa mahabusu ya Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani akisubiri kupelekwa gerezani mara baada ya kutiwa hatiani na Mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka na kulawiti Mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka saba February 13,2024 huko Kiluvya kwa Komba, Wilaya ya Kisarawe.

Soma Pia: Asha (47) ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mvulana wa miaka 15

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, Pius N. Lutumo amesema “Mara baada yakusomewa hukumu hiyo August 13,2024, Seleman aliingia chooni kisha kujinyonga kwa kutumia shati lake ambalo alilifunga kwenye nondo za dirisha la choo hicho, mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kwa uchunguzi wa Daktari na jana kukabidhiwa kwa Ndugu kwa ajili ya mazishi”

Chanzo: MillardAyo
 
Wabakaji na wauwaji mara nyingi huwa hawana maisha mazuri jela
Usitegemee utalelewa ukibaka na kuuwa
Inaweza kuwa kauwawa na wenye hasira mbaya na tukio hilo

Hata jela nyingi duniani watu kama hawa huuwawa na wafungwa wengine
Kama alifanya hivyo kajihukumu au kahukumiwa
 
Back
Top Bottom