Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,745
ALIYEHUKUMIWA MIAKA 30 JELA BILA KOSA AOKOLEWA NA JAJI.
Na Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241 Na Bashir Yakub, WAKILI.
Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Jaji L.M. MLACHA anasema kuwa katika pitia pitia yake katika mafaili mbalimbali ya kesi akakutana na faili moja ambalo hakulielewa elewa.
Kutokana na hilo akaamua kulipitia kwa umakini kuona kuna nini ndani. Ni hapo alipokutana na kisa cha mfungwa Selemani Maganga Munge ambaye alikuwa jela akitumikia kifungo chake cha miaka 30.
Selemani Maganga Munge alituhumiwa na kuhukumiwa na mahakama ya wilaya ya Kilombero Morogoro kwa kosa la kumbaka Marry Joseph Kachima.
Katika kupitia faili lile, Jaji Mlacha aligundua wazi kuwa ndugu Selemani alifungwa kwa kuonewa. Aligundua makosa makubwa saba yaliyofanywa na hakimu aliyehukumu kesi hiyo yaliyopelekea haki ya Selemani ya kutokuwa na hatia kupotea.
Hata hivyo katika makosa hayo saba aliyogundua Jaji, nitaongelea kosa moja tu, kosa la sita. Kosa hilo alilofanya hakimu aliyemhukumu Selemani ni kuwa, anayesemwa kuwa alibakwa (Mary Joseph) hakuwa ametoa maelezo kuwa alibakwa, bali maelezo yake yote aliyotoa alikuwa ameeleza kuwa walikuwa wamekubaliana.
Pamoja na maelezo haya ya Marry bado mahakama ilimkuta Selemani na hatia ya kubaka na kuamuru aende jela miaka 30. Jaji Mlacha alijaribu kuangalia umri wa Marry kuwa pengine alikuwa na umri chini ya miaka 18, ambapo katika mazingira kama hayo hata kama huyu aliyebakwa akisema niliridhia nakukubali, bado hatia ya kubaka inabaki palepale kwa sababu ni mdogo na sheria inatambua kuwa hana uwezo wa kutoa ridhaa.Pamoja na kuwaza hivyo,bado akakuta Marry alikuwa na umri wa miaka 23.
Kutokana na hayo Jaji Mlacha ananukuu maelezo ya Marry aliyotoa polisi kama ifuatavyo, (Marry anasema)".... ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 00;30hrs HIVI YULE MTU NILIYEMPATIA NAMBA YANGU YA SIMU ALINIPIGIA SIMU TUKAONGEA KWENYE SIMU, TUKAKUBALIANA TWENDE TUKALALE LODGE... TULIENDA HADI KWENYE HIYO LODGE, AKAINGIA NDANI AKANIAMBIA NISUBIRI NJE. NIKASUBIRI AKATOKA AKANIAMBIA HAPA WANAZINGUA TWENDE KWENYE LODGE NYINGINE... TULIELEWANA TWENDE TUKATOM...NE KWA KUTUMIA KONDOMU NA ALIKUBALI.. NIKASEMA SASA HIVI NI USIKU NIRUDI NYUMBANI......NAKULALA HAPA HAPA... AKANIPANUA MIGUU AKAINGIZA UUME WAKE.. NDIPO NIKAMWAMBIA NAOMBA NILALE VIZURI..."
Maneno haya ndiyo maelezo aliyotoa Marry polisi na kuletwa mahakamani kama ushahidi.
Kilichomshangaza zaidi Jaji Mlacha ni kuwa wakati kesi ikisikilizwa mahakamani Marry ambaye ndiye mtendewa hakuletwa mahakamani kutoa ushahidi wake.
Hii ni hata baada ya Selemani kuomba Mary aletwe mahakamani aje aseme kama kweli alimbaka au walikubaliana, bado Mary hakuletwa mpaka akuhukumiwa miaka 30 jela.
Badala yake mashahidi walioletwa mahakamani walikuwa ni maaskari waliomkamata kwenye tukio, na wale waliochukua maelezo yake polisi.
Kutokana uozo huu uliougundua katika faili hili, Jaji Mlacha aliliitisha mara moja kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 44(1) (a) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu,Sura ya 11,R;E 2002 ili kuifanyia kesi nzima Mapitio(Revision).
Mapitio hayo yakasajiliwa kama Mapitio Namba 16 ya Mwaka 2020 na Mfungwa Selemani Maganga Munge akaamriwa aletwe ili mapitio hayo yasikilizwe.
Siku ya kusikilizwa Selemani alipoulizwa kama ana lolote la kueleza hakueleza chochote bali aliiachia mahakama ifanye inavyojua.
Upande wa serikali/Jamhuri nao uliitwa chini ya Wakili wake Imelda ambapo nao walipotakiwa kueleza chochote walikiri kuwa Selemani hakuwa na hatia na hivyo hakutakiwa kufungwa.
Kutokana na maelezo hayo na yale Jaji aliyoyaona, basi tarehe 5/8/2020 Mahakama kuu kanda ya Dar Es Salaam chini ya Jaji L.M Mlacha ikatoa amri ya kuachiwa huru mara moja Selemani Maganga Munge na siku hiyohiyo akaachiwa huru.
Selemani Maganga Munge sasa hivi yuko huru na amerudi mtaani kuendelea na maisha yake kama kawaida.