Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Dr. Ulimboka alikuwa anatetea haki ya huduma za Afya kwa wote lakini malipo yake alitekwa na kuumizwa sana. Toka tawala zilipofumbia macho kutekwa na kuteswa kwake ndipo wanasiasa wakaona njia pekee yakuwatisha wananchi wanaotaka haki nikuteka ring leaders.
Hali ya utekaji ikaanza kushamiri na ilipofika awamu ya tano ndipo ikaidhinishwa rasmi na kuwa sheria mioyoni mwa waliotawala. Wakaanza na RAIA mwisho wakaumizana wenyewe kwa wenyewe.
Kwa kuwa walishaumizana wenyewe kwa wenyewe kinachotokea sasa ni kila anayepata mwanya anaunda mpango wa siri wa kulipiza kisasa kwa kuumizwa kwake au kuumizwa ndugu yake.
Watekelezaji wa mipango hii njia pekee wanayotumia nikujifanya watii kwa mamlaka na kuwaona wanaohoji kama wahalifu. Kama damu ya mtu ingekuwa haina connection na Mungu basi utekaji ungeacha. Lakini kwa kuwa waliodhulumu nafsi wameandikiwa kuadhibiwa hadi kizazi cha saba basi naamini hakuna mtawala atakayeweza kutubu dhambi hizi.
Kila mtawala atajikuta anazungukwa na watu ambao nafsi zao zina hatia. Atajikuta anazungukwa na nafsi zisizotulia, na anazungukwa na nafsi ambazo hazina usingizi.
Sometimes watawala wetu wanashindwa kuishi baadhi ya ofisi kutokana na miungu iliyopo ndani ya ofisi hizo. Sometimes wanajaribu kujiagua lakini hata waaguzi nao wanashindwa kuwawekea kinga yakudumu.
Tunapoona hali kama hii ya ubaguzi na uondoaji wa uhai inajitokeza katika Taifa tusimwachie mtawala. Tuondoe tofauti zetu nakulia pamoja. Leo mwanaccm anaposhangilia mwana ACT kutekwa au kufa anashangilia kifo cha ndugu yake bila kujua.
Hakuna mtu anazaliwa na chama cha siasa bali watu wanazaliwa na binadamu. Sisi binadamu ni ndugu lakini hatuna mahusiano ya damu na vyama vya siasa.
Ugopa sana kutukuza undugu wa vyama vya siasa ukaacha undugu wa damu. Ogopa sana kutukuza undugu wa dini ukaacha undugu wa damu.
Undugu wa dini na vyama au taasisi uishia kwenye uasi ambao ufanywa kwa kwa ndugu wa damu. Kutekwa kwa Ulimboka hakukuacha kero katika sekta ya afya bali kulichochea mjadala wa huduma mbaya za afya nchni. Sawa na kutekwa kwa wafanyabiashara ambavyo hakukuzi uchumi bali kunawafukuza.
Tusipoamua kurudia undugu wa damu unaoongozwa na falsafa ya BINADAMU WOTE NI SAWA NA WANA HAKI YA KUISHI, tusitegemee kufuta utekaji kwa undugu wa siasa na dini.