Simulizi za Shafih
New Member
- Aug 27, 2022
- 2
- 0
Niliamka asubuhi na mapema sana kuwahi kazini. Nadhani ungeniona mida nnatoka nyumbani ungeamini mimi nnaondoka asubuhi sana kwelekea kazini lakini hapana sio kawaida yangu.
Niliondoka asubuhi ile sababu ya kukosa usingizi usiku kucha nikiwa nawaza huku maisha ya familia yangu huku mke wangu akiwa amelala usingizi naamini alilala lakini sio kama siku zote nae pia alikua na mawazo pia hasira baada ya kutaka hela ya kusuka nikamwambia sina.
Alilala akiwa amenuna nnamini laiti angejua hali ya mfukoni kwangu asingejaribu kuniongelea jambo lolote kuhusu hela.
Usiku ule nilikuwa ninaumizwa na sauti ya mwanangu Zuwena ambae usik ule baada ya kurudi kazini alifuata mapaka nilipokua na kunikumbatia na huku akinitizama usoni japo alikua mtoto mdogo lakini alionekana anajambo linamuuliza sana moyoni mwake aliongozana na mimi mpaka ndani huku akionekana kukosa furaha kabisa.
Nilikaa kwenye kiti yeye akakaa pembeni yangu huku akinitizama usoni hakukaa sana alielekea chumbani kisha kutoka na yeboyebo zake za shule zilikua zimechakaa kabisà niliziangalia nilijisikia vibaya sana nilitamani nifanye jambo wakati ule ule nilishindwa alizishika mkononi huku akitizama sakafuni nilizichukua na kiziweka chini kisha akaniambia
"Baba nnakuomba uninunulie yeboyebo nyingine hizi zimechakaa"aliongea huku akikaa tena karibu yangu na kulaza kichwa mapajani pangu. Nilimwitikia huku nikifikiria ntawapi hela
Kumbuka kila siku alikuwa anapewa adhabu sababu ya kuvaa yeboyebo ila yeye anaomba anunuliwe tena yeboyebo niliwaza sana ina maana huyu mtoto anajua hali yangu au anapenda kutandikwa au shuleni wameruhusiwa kuvaa yeboyebo. Yote haya nilikua nnaywaza mpaka nikakosa usingizi usiku ule nilichokua nnakiwaza pàpambazuke niondoke kabla hajaamka ili nisione chozi lake ambalo niliamini ni haki yake na hata yeue hapendi hali ile.
Sikumwamsha nimuage kama siku zote niliondoka asubuhi sana na kuelekea kazini huku nikiwa nakumbuka baadhi ya watu niliokua nnawadai niliamini jioni ya siku ile ningerudi na furaha au zaidi ya furaha zawena.
Nilifika kazini na kuanza kazi huku nikisali sana mipango yangu ya siku ile itimie ila mambo hayakua hivyo mpaka jioni nilikua na 2000 niliitoa mfukoni nakuitizama mara mbili mbili na kuirudisha mfukoni nilijua lazima yangetokea makubwa nyumbani kwangu kwani niliamini uvumilivu wa familia yangu juu yangu umezidi sasa ningepoteza heshimà yangu yote ilikua ni sababu ya hela huku nikijiambia ipo siku na mimi ntapata.
Safari ilianza na baada ya kupanda daladala kuelekea nyumbani siku ile nilikua nnaona dereva anakimbiza sana gari na kwangu ni karibu sana yote sababu ya nyumbani baada ya dakika 15 nilikuwa ninakaribia kituo cha ninaposhukia nililipa nauli kisha nikashuka katika gari nililokua nimepanda tulishuka abiria wawili mwenzangu akiwa mwanamke alikua amebeba mtoto mgongoni japo umri wake hakuwa mtu mzima sana. Tulihitaji kuvuka barabara yule dada anilisogelea na kuniita
"Samahani kaka habari ya saa hizi" alinisalimia
"Poa tu vipi"nilimwitikia huku nikiangalia magari ilinivuke.
"Sahamani kaka nnashida nnaomba kama una 2000 unisaidie nikamnunulie mwanangu maziwa nilimfuata baba yake sijamwona"aliongea kwa huzuni sana.
Niligeuka kumtizama mara ya pili nikwamwambia ngoja tuvuke barabara. Nilikua nimewaza ghafla juu ya mwanamke yule na jinsi alivyoteseka na mwanae nikawaza mimi pia ñilivyoteseka na mawazo nilomwonea dada huruma ila sikuweza kumsaidia nilijifikiria sna.
Baada ya kuvuka barabara nilitoa zile noti mbili za 1000 nikampa moja alinishukuru sana. Niliitikia na kuondoka nikamwacha bado amesimama akinitizàma. Niliwaza nyumbani nitayamaliza vipi.
Siku ile Zuwena alikua tofauri na nilivyokua nnatarajia alikuwa na furaha sana hadi nikahisi kuna kitu kimetokea. Alinifuata na baada ya kukaa alikuja akiwa ameshika viatu vipya mkononi. Nilijiuliza hizi pesa wamepata wapi hata mke wangu alika nafuraha sananiliingiwa na wasiwasi.
Baada ya kupata chakula cha jioni ndipo mke wangu akanieleza kua bwana rashidi alileta zile hela tulizokua tumemkopesha.
Nilikaa kimya na kumshukuru mungu pia hata hivyo sikukumbuka kama tulimkopesha mtu fedha. Nilishukuru sana Mungu nikaitoa ile 1000 na kumpa mke wangu na kumwambia hii ndio iliyopatikana leo sijui yasingetokea haya ingekuaje.
Alinitizama kwa dakika kadhaa na kunikumbatia kwa hisia. Nilifurahi sana kuona nina mwanamke mvumilivu.
Ushauri, usisite katika kusaidia wengine
MW I S H O

Upvote
1