Aliyekutwa amefariki Marekani mwaka 2020 abainika alikuwa Mtanzania

Aliyekutwa amefariki Marekani mwaka 2020 abainika alikuwa Mtanzania

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
marekani.jpeg


Wapelelezi nchini Marekani wamefanikiwa kuutambua mwili wa kijana aliyekutwa amefariki dunia kwenye fukwe huko Galveston sland, Texas miaka mitatu iliyopita.

Polisi wa Galveston wameutambua mwili huo ulikuwa wa Calvin Mbwambo (26), na kudai kuwa ni Mtanzania aliyekuwa masomoni nchini Marekani.

Mwili wa Calvin ulipatikana siku ya Mama Duniani mwaka 2020, lakini Wapelelezi hawakuweza kumtambua ni nani kwa kuwa hakuwa na utambulisho wowote. Kwa kipindi chote hicho waliendelea kufanya uchunguzi wa DNA na cha kwanza walibaini kuwa mwili huo haukuwa wa raia wa Marekani.

Pia walikagua nyaraka na rekodi za Serikali zinazowahusu Wanafunzi wa kigeni ambao hawajulikani walipo na alama za vidole zilionesha ni kweli mwili huo ulikuwa wa Calvin.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zinaeleza kuwa tayari polisi wa Galveston, Marekani wameitaarifu familia ya
Calvin Mbwambo iliyopo Tanzania kuhusu kifo cha ndugu yao.

Chanzo cha kifo cha Calvin bado hakijafahamika na taarifa za polisi zinaonesha hakuna dalili kuwa alifanyiwa ukatili wowote kabla ya kifo chake.

Mkasa wa kifo cha Calvin ulioneshwa hadi kwenye kipindi cha ABC13, Unsolved huko Marekani.
 
Polisi nchini Marekani wametambua mwili wa kijana aliyekutwa amefariki dunia kwenye fukwe za Galveston Island, Texas miaka mitatu iliyopita. Mwili huo umethibitishwa kuwa ni wa Calvin Mbwambo (26), raia wa Tanzania aliyekuwa akihudhuria masomo nchini Marekani.

Mwili wa Calvin ulipatikana siku ya Mama Duniani mwaka 2020, lakini awali haukuweza kutambuliwa kwa kuwa hakuwa na kitambulisho. Uchunguzi wa DNA ulifanywa kwa muda wote huo, na hatimaye matokeo ya kwanza yalibainisha kuwa mwili huo si wa raia wa Marekani. Polisi pia walikagua nyaraka na rekodi za Serikali zinazohusiana na wanafunzi wa kigeni, na alama za vidole zilithibitisha utambulisho wa Calvin.

Familia ya Calvin Mbwambo iliyopo Tanzania imeshataarifiwa na polisi wa Galveston kuhusu kifo cha ndugu yao. Walakini, bado chanzo cha kifo cha Calvin hakijafahamika na uchunguzi wa polisi unaonyesha hakuna dalili za ukatili wowote kabla ya kifo chake.

Mkasa wa kifo cha Calvin umeshughulikiwa kwenye kipindi cha ABC13, Unsolved huko Marekani.
 
Huku kwetu wale wa kwenye viroba walizikwa upesiupesi bila kutafuta ni wakina nani!
 
Back
Top Bottom